Aliyetufikisha Uchumi wa Kati ni Kikwete na siyo Magufuli, acheni kudanganya!

Bado hadi 2025 mtaona kila rangi!

Naona sasa hivi hamdemki tena kwa mama! Kawapiga makwenzi kwenye uteuzi wa madc hadi Lisu kule kwa amstwrdam kaumia sana!

Na 2025 tutawalaza na viatu
Corona inakuwa hatari zaidi pale unapo ibeza
 
hizi propaganda ziingine wacha wengine tupite tu.
 
Acha utopolo wewe inflation ni dalili ya uchumi mbovu na kuonyesha kuwa kune deficit in trade kuwa import ni kubwa kuliko export ilifika kipindi watu wanatumia dollar kufanya miamala humu ndani Tanzania halafu unasema uchumi umekuwa sasa Tanzania ilikua na tofauti gani na Somalia isiyokuwa na serikali mpaka wanatumia pesa za kigenj
 
Sawa Ridhiwani.
 

si tulikubaliana hatupo uchumi wa kati ama mmekubali saahv?
 
ni sawa tu, koz lengo lako la kuandika uzi huu ni sawa na wale wanaosema JPM ndio katujisha kati, so pambana nalo ikifika 2025 ndio tutajua mbivu na mbichi
 
Povu la nini; mipango siyo inayoleta matokeo, bali ni utekelezaji ndio unaoleta matokeo. Hata kama mipango iliaza na kikwete haikusimamiwa naye; failures tatu kubwa ya Kikwete ni kuwa (a) Hakuwa kiongozi decisive (b) hakutaka kuchukua responsibility na (c) aliongoza nchi bila kuwa na lengo thabiti ambalo angependa kuliona bali alitaka bora siku ziende.

Mambo mengi yaliyotaka ujasiri katika utekelezaji, kama vile usimamizi dhidi ya matumizi mabaya za raslimali za nchi, Kikwete hakuyagusa, ndipo twiga wakawa wanasafirishwa kwenda nje,m na hata makinikia yalianza kipindi hicho. Kikwete aliwahi kusikika akiwaomba walioiba mali za umma (kama ITPL na escrow) wazirudishe kwa hiari yaoile: hiyo siyo namna ya kuendesha serikali, kwani sheria zipo, na ni kazi ya serikali kuzisimamia. Vile vile wakati wa utawala wa Kikwete kuna kipindi bajeti ya ikulu iliishiwa pesa kabisa; ikabidi wapewe supplementary kutokana na matumizi yasiyokuwa na malengo.

Kuhusu responsibility, siku moja kwenye mkutano na wazee wa dar es Salaama, Kikwete aliskika akilalamika kuwa kwa nini "hawajengi" flyovers kupunguza foleni Dar es salaam. Hilo neno hawajengi ilikuwa na maana ya yeye kujitoa kwenye responsibility hiyo, na wala pia haikuwa priority yake, alitegemea wengine ndio wafanye.

Kikwete alikuwa anazungumza maneno mazuri bila kujali utekelezaji wake, wakati Magufuli alikuwa anaongea maneno makali na vile vile kufuatilia utekelezaji wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…