Aliyetangaza nchi haina njaa ndiye alisema atahamisha wizara yake ndani ya wiki moja

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
9,038
17,932
Wana JF,

Wakati Mh.Rais anatangaza kwamba atahamisha serikali Dodoma, waziri mwenye dhamana ya kilimo, uvuvi na mifugo magazeti ya tarehe 27/july/2016 yalimnukuu akitangaza atahamisha ofisi yake wiki inayofuata akipokea mwangwi wa Waziri Mkuu ambaye naye alizitaka kuhamia Dodoma itakapofika Septemba mwaka jana. Kilichotokea mpaka leo wizara ipo pale Temeke Veterinary. ya Waziri Mkuu?

Kwa mtiririko ule ule, Rais kasema wanaosema kuna njaa ni wafanyabiashara na Waziri Mkuu naye amerejea kwamba taifa halina njaa na Waziri wa kilimo ufugaji na uvuvi yule yule aliyetangaza kuhamia Dodoma kwa spidi ya ajabu ametangaza kwamba taifa halina njaa na akawashangaa wanaosema njaa ipo.

Je, tumtegemee na tumuamini waziri ambaye hapo awali ameonyesha hana uwezo wa kutimiliza kile asemacho/hana credibility?

Wizara ya Kilimo yatangaza kuhamia Dodoma wiki ijayo
 
Huu ndio wakati wa kuhalalisha gongo kwa hisani ya watu wa Marekani. Mambo yanayoendelea nchini mwetu si ya kuyatilia maanani maana yatakuumiza kichwa na kiroba bei juu.

Ngoja nikajidunge komoni kwa Mama Tuntufye mawazo yapungue
 
Awamu zote hazikuwahi poteza mvuto mapema kama awamu hii!
Mungu tu atufanyie wepesi hii miaka mitatu iliyobaki
 
Awamu zote hazikuwahi poteza mvuto mapema kama awamu hii!
Mungu tu atufanyie wepesi hii miaka mitatu iliyobaki
Kiongozi wa Nchi anachukia mtu tajiri by nature, alisema Matajiri wataishi Kama mashetani, hakujua 100% ya masikini hutegemea mkate wao toka kwa matajiri! we are real tired.
 
Hivi matumizi ya bange, shisha, mirungi na madawa mengine ya kulevya kwann yasiruhusiwe tu... Maana naona kama vio.. gozi wetu awamu hii wanatumia wote. Fatilia matamko yao, analo liongea leo kesho atalikataa yy mwenyewe au atapigwa na mdogo zaidi yake.
 
Back
Top Bottom