Aliyesema wanaume hawaaminiki ni nani?

Aliyesema wanaume hawaaminiki ni nani?

Barieda

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Posts
1,811
Reaction score
2,484
Habari za jioni wakuu?
Moja kwa moja kwenye maada, nahitaji kujua mwanamke aliyesema Wanaume hawaaminiki ni nani?

Hii kauli imeleta madhara makubwa sana kwenye ndoa na hata mahusiano yetu, ndoa hazidumu na ushirikiano wa kiuchumi baina ya wanandoa umepungua kiasi kikubwa sana, si ajabu pindi mwanaume anapambana kutafuta hela ya kulisha, kusomesha watoto na kujenga nyumba mwanamke naye anapambana kununua kiwanja chake anajenga nyumba yake kwa kile kinachodaiwa wanaume hawaaminiki.

Naomba kujua je ninani huyo? Alikuwa na nia gani? Kama yupo hai naomba aje atengue kauli yake ili anusuru ndoa na mahusiano yetu, kwenu wadau.
 
Aliyesema ni mwanamke, akijaribu kutupumbaza maana wanajulikana kama hawaaminiki toka enzi na enzi za Adam
Kwan hakujua kuwa kauli yake ingeleta madhara makubwa namna hii?
 
Ni kweli hawaaminiki maana mimi wanaume wote niliokuwa nawatumia kama reference nikikutana na kauli kama hizi wameniangusha vibaya mnooo. Ila huwa wanasema 'there are exceptions to every general rule' sijui kama nimepatia ila ni kitu kama hicho...ukikutana ma mwanaume wa tofauti jua ni msemo huo umetimia
 
Sasa unatuuliza sisi mkuu..

Wahenga hao..we endelea kuwaamini kesho uje na uzi mwingine unaosema ALIYESEMA BANGI MBICHI NI MBOGA NI NINI..[emoji28][emoji28][emoji28]

Maana maswali yako ni utata...
 
Mkuu wewe ukianza kutafuta aliyesema ni nani itasaidia nini?

Wewe anza kuwa muaminifu. Mjenge mke wako akuamini.

Akikuamini yeye inatosha hata kama hawa wengine walio baki wakisema wanaume sio waaminifu...
 
if you got honest,loving n caring man shukuru Mungu.
Wanaume wengi tunajielewa na tunatambua wajibu wetu kama wanaume kwenye familia, tunawapenda wake zetu na kuwajali, tatizo ni sumu iliyolishwa kwa nyie viumbe wa Mungu.
 
Ni kweli hawaaminiki maana mimi wanaume wote niliokuwa nawatumia kama reference nikikutana na kauli kama hizi wameniangusha vibaya mnooo. Ila huwa wanasema 'there are exceptions to every general rule' sijui kama nimepatia ila ni kitu kama hicho...ukikutana ma mwanaume wa tofauti jua ni msemo huo umetimia
Mkuu wanaume walikufanyaje?
 
Habari za jioni wakuu?
Moja kwa moja kwenye maada, nahitaji kujua mwanamke aliyesema Wanaume hawaaminiki ni nani?

Hii kauli imeleta madhara makubwa sana kwenye ndoa na hata mahusiano yetu, ndoa hazidumu na ushirikiano wa kiuchumi baina ya wanandoa umepungua kiasi kikubwa sana, si ajabu pindi mwanaume anapambana kutafuta hela ya kulisha, kusomesha watoto na kujenga nyumba mwanamke naye anapambana kununua kiwanja chake anajenga nyumba yake kwa kile kinachodaiwa wanaume hawaaminiki.

Naomba kujua je ninani huyo? Alikuwa na nia gani? Kama yupo hai naomba aje atengue kauli yake ili anusuru ndoa na mahusiano yetu, kwenu wadau.
tena nyumba zinaisha na kupangishwa bila upande wa pili kujua!
 
Acha Mungu mwenyewe awaonyeshe vinavyotakwa watawaamini wame wao!
wakijua kwanini mme anampeleka kwake mkewe, wataona kwamba wamelazimishwa tangu mwanzo wa maishao kuamini wame wao.
 
Back
Top Bottom