Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Kamanda wa Polisi, anasema kwamba dereva alitoroka ama kutoroshwa na kwamba polisi hawajui yuko wapi na wanamtafuta??? Nadhani kesho watasema "wamempata" akiwa hajachubuka hata 'nywele'.... Je, atakua ni dereva yule yule aliyekuwamo katika tukio? Je, waliomtorosha (kutoroka) ni kina nani?
Hilo gari halikua lina overtake gari lolote bali lililifuata gari la mheshimiwa Mbatia....
Sumaye muda huo alikua amekwisha kupita eneo la ajali, nyuma ya mbatia alikua Zitto na Mathayo David Mathayo.. Zitto alifika enep la tukio takriban dakika tano. Inawezekana kabisa aliona kila kitu wakati ajali inatokea lakini si vyema kwa sasa kwa yeye kuzungumzia tukio hilo humu.
TUTAFAKARI.....
OMBI... Kwa wale wenye kumbukumbu ya ajali ya Sokoine kule Morogoro atupe, ikiwa ni pamoja na alipo sasa dereva Dube na mazingira ya ajali ile. Hii itatusaidia kuepuka ajali za VIONGOZI wetu kwa siku za usoni.
Hilo gari halikua lina overtake gari lolote bali lililifuata gari la mheshimiwa Mbatia....
Sumaye muda huo alikua amekwisha kupita eneo la ajali, nyuma ya mbatia alikua Zitto na Mathayo David Mathayo.. Zitto alifika enep la tukio takriban dakika tano. Inawezekana kabisa aliona kila kitu wakati ajali inatokea lakini si vyema kwa sasa kwa yeye kuzungumzia tukio hilo humu.
TUTAFAKARI.....
OMBI... Kwa wale wenye kumbukumbu ya ajali ya Sokoine kule Morogoro atupe, ikiwa ni pamoja na alipo sasa dereva Dube na mazingira ya ajali ile. Hii itatusaidia kuepuka ajali za VIONGOZI wetu kwa siku za usoni.
Ajali ya Mhe. Mbatia Sumaye, Zitto chupuchupuAjali ya Mhe. Mbatia Sumaye, Zitto chupuchupu
2007-10-25 16:23:06
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Waziri Mkuu mstaafu Mheshimiwa Fredric Sumaye, Mbunge Machachari wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. David Mathayo ni miongoni mwa watu walioponea chupuchupu kupatwa na ajali iliyotokea jana jioni na kusababisha kifo cha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Marehemu Salome Joseph Mbatia.
Bw. Sumaye, Zitto na Mathayo walikuwa kwenye magari tofauti wakiongozana katika barabara moja na gari la Mhe. Mbatia lililopata ajali, bila wao kufahamiana.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo wanasema lori aina ya Fuso liligongana uso kwa uso na gari la Mhe. Mbatia, ndilo lililopoteza mwelekeo na kusababisha ajali hiyo.
Kwa vile magari yaliyokuwa yamewabeba waheshimiwa hao yalikuwa yakiongozana, basi kama lori hilo lisingegonga gari la Mheshimiwa Mbatia huwenda lingeyavaa magari ya waheshimiwa wengine.
Akizungumza na Alasiri kwa njia ya Simu leo asubuhi, Mheshiwa Zitto amesema gari lililokuwa limembeba marehemu Salome Mbatia lilikuwa mbele yake wakiongozana barabarani, lakini hakujua kuwa aliyekuwamo alikuwa ni Naibu Waziri Salome Mbatia.
Gari hilo lilikuwa mbele yangu, nililiona lakini kwa vile marehemu alitumia gai binafsi, sikujua kuwa aliyekuwemo alikuwa ni Mhe. Mbatia,
akasema Zitto.
Akasema Mheshimiwa Zitto kuwa yeye alifika ndani ya muda wa dakika tano baada ya gari la Mheshimiwa Mbatia kupata ajali, lakini kwa jinsi gari hilo lilivyokuwa limepata ajali hakuwe .
Zitto amesema muda mfupi baadaye wakati wakiendelea kuwatoa majeruhi kwenye magari,likafika gari lingine alilokuwemo Bw. Mathayo, ambaye alimtambua moja kwa moja Naibu Waziri Salome Mbatia, kwa vile alikuwa na taarifa za safari yake hiyo na alilijua gari hilo lililopata ajali.
Mheshimiwa Mathayo ndiye aliyemtambua Marehemu Mbatia,
akasema.
Kwa mujibu wa Bw. Zitto wakati wakiendelea kuiondoa miili ya marehemu kwenye magari, pia likafika gari lingine alilokuwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Fredrick Sumaye ambaye pia aliungana nao katika kusaidia kuitoa miili ya marehemu kwenye magari ambayo yalikuwa yamepondeka vibaya.
Bw. Zitto akasema baada ya kuona ajali hiyo akaamua kukatiza safari yake na gari lake likatumika kuwakimbiza majeruhi wengine hospitalini.
Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw. Advocate Nyombi amesema dereva wa gari aina ya Fuso liligongana na Gari la Naibu Waziri huyo na kusababisha kifo chake amenusurika.
Kamanda Nyombi ameiambia Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi kuwa aliyekufa papo hapo katika ajali hiyo ni Utingo wa Fuso hilo aliyemtaja kwa jina la Castory Kilagwa, 22, ambaye ni ndugu wa mmiliki wa Fuso hilo.
Amesema hata hivyo Dereva huyo inadaiwa kuwa alikimbia au aliondolewa haraka eneo la tukio, na hivyo hajulika alipo na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.
Kamanda Nyombi amesema Polisi imemkamata mmiliki wa Fuso hilo aliyemtaja kwa jina la Jackson Kilagwa ili awaaidie kumpata dereva wake.
Tunaamini hawezi kumkabidhi mtu mali yake ya thamani kiasi kile bila kujua mahali anapoishi, ndio sababu tunamshikilia mmiliki wa gari hilo ili atusaidie kumpata dereva wake,
akasema Kamanda Nyombi.
Akizungumzia taratibu za usafirishaji wa mwili wa Marehemu Naibu Waziri Salome Mbatia, Kamanda Nyombi amesema anachosubiri ni maelekezo kutoka ngazi za juu.
Akasema taarifa aliyopewa awali ni kuwa ndege ya Serikali ingewasiri Njombe leo saa 3:00 asubuhi kuuchukua mwili huo, lakini mpaka wakati akiwasiliana na gazeti hili ilikuwa bado haijafika.
Nimeambiwa ndege ingefika saa 300 asubuhi, lakini mpaka sasa sijaiona na hivyo nasubiri taarifa nyingine kutoka ngazi za juu,
akasema Kamanda Nyombi.
SOURCE: Alasiri