Aliyesababisha kifo cha Salome Mbatia akamatwa

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Kamanda wa Polisi, anasema kwamba dereva alitoroka ama kutoroshwa na kwamba polisi hawajui yuko wapi na wanamtafuta??? Nadhani kesho watasema "wamempata" akiwa hajachubuka hata 'nywele'.... Je, atakua ni dereva yule yule aliyekuwamo katika tukio? Je, waliomtorosha (kutoroka) ni kina nani?

Hilo gari halikua lina overtake gari lolote bali lililifuata gari la mheshimiwa Mbatia....

Sumaye muda huo alikua amekwisha kupita eneo la ajali, nyuma ya mbatia alikua Zitto na Mathayo David Mathayo.. Zitto alifika enep la tukio takriban dakika tano. Inawezekana kabisa aliona kila kitu wakati ajali inatokea lakini si vyema kwa sasa kwa yeye kuzungumzia tukio hilo humu.

TUTAFAKARI.....

OMBI... Kwa wale wenye kumbukumbu ya ajali ya Sokoine kule Morogoro atupe, ikiwa ni pamoja na alipo sasa dereva Dube na mazingira ya ajali ile. Hii itatusaidia kuepuka ajali za VIONGOZI wetu kwa siku za usoni.
Ajali ya Mhe. Mbatia Sumaye, Zitto chupuchupu

2007-10-25 16:23:06
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Waziri Mkuu mstaafu Mheshimiwa Fredric Sumaye, Mbunge Machachari wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. David Mathayo ni miongoni mwa watu walioponea chupuchupu kupatwa na ajali iliyotokea jana jioni na kusababisha kifo cha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Marehemu Salome Joseph Mbatia.

Bw. Sumaye, Zitto na Mathayo walikuwa kwenye magari tofauti wakiongozana katika barabara moja na gari la Mhe. Mbatia lililopata ajali, bila wao kufahamiana.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo wanasema lori aina ya Fuso liligongana uso kwa uso na gari la Mhe. Mbatia, ndilo lililopoteza mwelekeo na kusababisha ajali hiyo.

Kwa vile magari yaliyokuwa yamewabeba waheshimiwa hao yalikuwa yakiongozana, basi kama lori hilo lisingegonga gari la Mheshimiwa Mbatia huwenda lingeyavaa magari ya waheshimiwa wengine.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya Simu leo asubuhi, Mheshiwa Zitto amesema gari lililokuwa limembeba marehemu Salome Mbatia lilikuwa mbele yake wakiongozana barabarani, lakini hakujua kuwa aliyekuwamo alikuwa ni Naibu Waziri Salome Mbatia.

`Gari hilo lilikuwa mbele yangu, nililiona lakini kwa vile marehemu alitumia gai binafsi, sikujua kuwa aliyekuwemo alikuwa ni Mhe. Mbatia,` akasema Zitto.

Akasema Mheshimiwa Zitto kuwa yeye alifika ndani ya muda wa dakika tano baada ya gari la Mheshimiwa Mbatia kupata ajali, lakini kwa jinsi gari hilo lilivyokuwa limepata ajali hakuwe .

Zitto amesema muda mfupi baadaye wakati wakiendelea kuwatoa majeruhi kwenye magari,likafika gari lingine alilokuwemo Bw. Mathayo, ambaye alimtambua moja kwa moja Naibu Waziri Salome Mbatia, kwa vile alikuwa na taarifa za safari yake hiyo na alilijua gari hilo lililopata ajali.

`Mheshimiwa Mathayo ndiye aliyemtambua Marehemu Mbatia,` akasema.

Kwa mujibu wa Bw. Zitto wakati wakiendelea kuiondoa miili ya marehemu kwenye magari, pia likafika gari lingine alilokuwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Fredrick Sumaye ambaye pia aliungana nao katika kusaidia kuitoa miili ya marehemu kwenye magari ambayo yalikuwa yamepondeka vibaya.

Bw. Zitto akasema baada ya kuona ajali hiyo akaamua kukatiza safari yake na gari lake likatumika kuwakimbiza majeruhi wengine hospitalini.

Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw. Advocate Nyombi amesema dereva wa gari aina ya Fuso liligongana na Gari la Naibu Waziri huyo na kusababisha kifo chake amenusurika.

Kamanda Nyombi ameiambia Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi kuwa aliyekufa papo hapo katika ajali hiyo ni Utingo wa Fuso hilo aliyemtaja kwa jina la Castory Kilagwa, 22, ambaye ni ndugu wa mmiliki wa Fuso hilo.

Amesema hata hivyo Dereva huyo inadaiwa kuwa alikimbia au aliondolewa haraka eneo la tukio, na hivyo hajulika alipo na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.

Kamanda Nyombi amesema Polisi imemkamata mmiliki wa Fuso hilo aliyemtaja kwa jina la Jackson Kilagwa ili awaaidie kumpata dereva wake.

`Tunaamini hawezi kumkabidhi mtu mali yake ya thamani kiasi kile bila kujua mahali anapoishi, ndio sababu tunamshikilia mmiliki wa gari hilo ili atusaidie kumpata dereva wake,` akasema Kamanda Nyombi.

Akizungumzia taratibu za usafirishaji wa mwili wa Marehemu Naibu Waziri Salome Mbatia, Kamanda Nyombi amesema anachosubiri ni maelekezo kutoka ngazi za juu.

Akasema taarifa aliyopewa awali ni kuwa ndege ya Serikali ingewasiri Njombe leo saa 3:00 asubuhi kuuchukua mwili huo, lakini mpaka wakati akiwasiliana na gazeti hili ilikuwa bado haijafika.

`Nimeambiwa ndege ingefika saa 300 asubuhi, lakini mpaka sasa sijaiona na hivyo nasubiri taarifa nyingine kutoka ngazi za juu,` akasema Kamanda Nyombi.

SOURCE: Alasiri
Ajali ya Mhe. Mbatia Sumaye, Zitto chupuchupu
 
huyo dereva katorkea baada ya kufikiswa hospitalini au?, au ndio tuseme pale pale hakuumia hata kidogo kiasi cha kuweza kujichanganya na watu wengine na kutojuulikana kama ni dereva wa hilo fuso?
 
Mungu ni mkuu na mwema sana!!! naamini ataendelea kumlinda mh. Zitto na kila aina ya hila na ubaya unaolengwa kwake!!

It looks as if he was the target!!
 
Hilo gari halikua lina overtake gari lolote bali lililifuata gari la mheshimiwa Mbatia....

TUTAFAKARI.....

OMBI... Kwa wale wenye kumbukumbu ya ajali ya Sokoine kule Morogoro atupe, ikiwa ni pamoja na alipo sasa dereva Dube na mazingira ya ajali ile. Hii itatusaidia kuepuka ajali za VIONGOZI wetu kwa siku za usoni.
http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2007/10/25/101174.html

Acheni conspiracy theories hapa. Hiyo ajali, imetokea, imetokea. Huyo mbatia siku yake ndio ilikuwa imefika. Wote tutakufa, na hatujui tutakufa kwa jinsi gani na tutakutana wapi na ziraeli.

Kwani watanzania wangapi wanakufa kila siku kwa ajali za barabarani?? Kwani huyo marehemu ana tofauti gani na za kibanadamu na mwanakijiji wa chole samvula???
 
Halisi.OMBI... . Hii itatusaidia kuepuka ajali za VIONGOZI wetu kwa siku za usoni.

Why viongozi alone?? What about the general public??? This is utterly non-sense.
 
Mungu ni mkuu na mwema sana!!! naamini ataendelea kumlinda mh. Zitto na kila aina ya hila na ubaya unaolengwa kwake!!

It looks as if he was the target!!

Acheni kuzunguka zunguka. Mnataka kusema huyo dereva alikuwa amepewa task ya kuondoa roho ya zitto?? Mnaanza kuhukumu hata uchunguzi haujafanyika. Mmoja hapo juu anasema eti hilo fusso lilifuata moja kwa moja gari la marehemu. Naomba kumuuliza, ajali huwa zinatokea vipi?? is it not the case kwamba magari inabidi yakutane uso kwa uso ili ajali iweze kutokea??? Sasa ajali ingetokeaje kama kila dereva angeendelea kubaki kwenye lane yake???
 
Hii ni assassination attempt that went wrong, I said it, yes I said it!
 
ajali ni nyingi sana Tanzania,wote tunatakiwa tuwe makini,mfano wenye malori/mabasi makubwa ,Taxi ,Ajirini madreva wenye uzoefu na ikiwezekana muwape mafunzo,Sisi kama binadamu tunatakiwa tujali utu na sio faida mbele.
Kwa abiria inabidi tuwe na uwezo wa kuwakatalia madreva tunawaowatilia wasiwasi na umakini wao kwenye barabara.wote tukisaidiana pamoja na viongozi wetu,tunaweza kupunguza ajali hizi barabarani.
 
Hii ni assassination attempt that went wrong, I said it, yes I said it!

Mwafrika huwezi kusema hii ni assasination attempt. Hilo nakupinga kwa sababu hatuna taarifa kamili za mazingira ya ajali yenyewe. Inawezekana kulikuwa na matatizo katika steering ya fusso, etc.Kama wanataka ku-ondoa roho ya zitto sio lazima wamsubiri barabarani. Nadhani sasa tunakwenda mbali sana.
 
Mungu ni mkuu na mwema sana!!! naamini ataendelea kumlinda mh. Zitto na kila aina ya hila na ubaya unaolengwa kwake!!

It looks as if he was the target!!

C'mon man, are you serious? Nashindwa kuamini ulicho andika, mwacheni huyu mama marehemu angalau azikwe kwanza!!. Ulichoandika hapo juu sound like a suicide mission, kitu ambacho kwa mswahili hakipo and therefore your theory is not only wrong but untimely,corrupt and far fetched.....GADEMU.
 
Mwafrika huwezi kusema hii ni assasination attempt. Hilo nakupinga kwa sababu hatuna taarifa kamili za mazingira ya ajali yenyewe. Inawezekana kulikuwa na matatizo katika steering ya fusso, etc.Kama wanataka ku-ondoa roho ya zitto sio lazima wamsubiri barabarani. Nadhani sasa tunakwenda mbali sana.

Asante mwanamalundi,

No wonder watu wengine wameniita mpuuzi na mjinga huku wengine wakishauri nikapimwe akili. Unachosema ni kweli na ninashawishika kukubaliana nawewe.

Tatizo ni kuwa nimeishi America long enough na kusoma vitabu vya kutosha kuonesha kuwa mambo mengi duniani hayatokei kwa bahati mbaya.

Kuna watu walisema hapa kuwa waendeshaji wa mabwawa ya maji mtera na kidatu walifungulia maji makusudi ili kuwe na energy crisis in Tanzania na baadae mikataba bomu isainiwe kwa haraka na mimi nikabisha sana.

Baada ya kusoma hii mikataba ya Kiwira, IPTL, Richmonduli, Songas, etc na kisha kucompare kilichotokea America na middle east miaka ya 79-80, Sina sababu kabisa ya kutosikiliza theories zote zinazosemwa kuhusu matukio.

I might be wrong ( na sitaumia nikitukanwa kwa hili) lakini hii ajali iko so suspicious to me!
 
Sijui ni kwanini watu wanapenda sana kukuza na kuandika mambo ambayo hayapo.

Labda wangetaka tuamini kuwa Zito ndio alikuwa target basi wangetuambia how they think the whole plan was executed and what went wrong.

From my simple understanding and from what the madia has reported hii inaonekana ni ajali ya kawaida tu ambayo ingeweza kumpata mtu yoyote.

Kama Zito alikuwa target basi dereva wa lori lazima alijua Zito anatumia gari gani. Unless gari lake na la Marehemu yalikuwa sawa then jiulize kwanini alikosea na kuligonga gari la Marehemu?

Pili mwandishi anataka tuamini kuwa Marehemu, Zito, Sumaye na Mathayo walikuwa wanaongozana barabarani kiasi kwamba kama dereva wa lori angeikosa gari ya Marehemu basi angeligonga gari la Zito. Zito mwenyewe kasema kuwa alifika sehemu ya tukio baada ya dakika tano hivi. Kwa wale wenye uzoefu wa kusafiri safari ndefu, dakika tano kwa gari linaloenda Km 80 kwa saa ni sawasawa na umbali wa Km 6 hivi. Sasa kwa umbali huo utaona kuwa hata kama angeikosa gari ya Marehemu basi angeweza kuanguka mwenyewe tu unless mwandishi anataka tuamini kuwa hiyo error kama isingetokea kwa Marehemu basi ingetokea kwa Zito.

Pia mwandishi anakuwa na mashaka juu ya maelezo ya polisi kuwa dereve wa lori alitoroka au "kutoroshwa" baada ya ajali. Kwa kumbukumbu zangu mara nyingi madereva wasababishapo ajali hukimbia kuhofia maisha yao na wengine wakiogopa kushitakiwa.

Mimi naona hii ilikuwa ni ajali ya kawaida tu kama ajali nyingine.
 
ha ha ha shakazulu,

usijekosa usingizi bure mwenzangu. Hizi ndizo huitwa conspiracy theories (take emphasis on conspiracy). Bado haijathibitisha na labda haitakuja kuthibitishwa.

mwandishi anadhani dereva alitoroshwa na amesema hivyo, ni vizuri pia nawe umedhani kuwa dereva alitoroka and thats fine.

Mimi naona kuna kitu fishy hapa na nimekubaliana na mwandishi huyu at least for now. Nimekubali kuitwa mjinga kwenye hili
 
Kwa mazingira ya ajali hii, ni vigumu kusema moja kwa moja kuwa kuna mtu alilengwa kutolewa uhai, tuache polisi wafanye kazi yao na watupatie matokeo ya uchunguzi.
 
error ya dakika tano ni kubwa sana kwa kusema alitaka kudhuriwa mtu mwengine .........

au labda huyo alotumwa alikuwa si mtaalamu basi! lol .....kazi hakuiweza (jk)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom