Aliyeoa amefanya uamuzi mgumu kweli, anahitaji pongezi

Aliyeoa amefanya uamuzi mgumu kweli, anahitaji pongezi

Linamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
9,974
Reaction score
24,504
Habari MMU,

Nimekaa nikaziangalia baadhi ya ndoa na nikatafakari kwa muda sana swala la ndoa nikaona mwanaume aliyenyanyua mkuu wake na kwenda kwao mwanamke akamtolea mahari mwanamke akaoa nikajiridhisha kwa kusema huyo ni mwanaume. Nasema haya kwa sababu moja tu. Wote tunajua asilimia kubwa sana wengi yetu kuna kipato cha chini tunaweza kuacha kiasi cha kawaida sana kwa hao wake.

Cha ajabu unaporudi unakuta chakula tofauti na matarajio yako ukilinganisha na kiasi chako ulichoacha ukizingatia hana kazi wala biashara yoyote anayoifanya zaidi ya mama wa nyumbani ila wengi huwa hawaulizi na maisha yanaendelea.
Wakati huo huo mke wako atavaa kanga mpya na wigi jipya wala huulizi vimetoka wapi bila shaka wewe ni mwanaume.

Wakati wewe unaambiwa baba naniii mtoto anaumwa naomba hela nimpeleke hospital unajibu mama naniii mpe tu panadol msikilizie hadi baadae ngoja niende kwenye mizunguko yangu nikipata utampeleka hospital wakati wewe unaambiwa hayo kuna kidume anapigiwa simu tena kwa kuitwa baby, sweet, honey na majina mengine mengi mazuri kuwa kuna dera jipya limetoka linauzwa elfu 30 anataka na yeye atingishe mtaa kidume kinajibu nakutumia sasa Hivi tigo pesa tena kwa kujitutumua kabisa na kukutukana juu huyu mjinga wako kaondoka? Maana anataka apetipeti. Aliyeoa kweli ni mwanaume.

Mbaya zaidi unakuta ameoa mwanamke asiyeendana naye. Anachukua taa ya barazani anaenda kuweka chumbani au anachukua solar anaenda kuifunga msongora huko hamna hata umeme unaenda kuwamulikia wenzako hapo jirani atanza kuomba kuja kuchomeka charger yake achaji simu kesho ataomba mwingine kesho kutwa mwingine tena kutaamaki unatafuta panga ukate nyaya tena ushachelewa Kweli kweli. Kuna wanawake wameumbwa kwa lengo la kuwafurahisha tu wanaume na kuna wanawake wameumbwa kwa ajali ya kuolewa.
 
Somethings are realy difficulty to understand in a normal life, even a wisest person in a world of menkind can not explain it, sometimes I ask myself what is the reality! how does it look like?????
 
Kwaiyo unashauri nini? Nimeona assumptions zako kuna hekaya za kilevi tu. Tatzo ni kwamba watanzania wengi hawajapata elimu ya mahusiamo tangu wakiwa wadogo kuanzia nyumbani na mashuleni (sexuality education) na hii ndio imepelekea vijana wetu kuwaza mambo kama haya. Hakuna respect, love, care and responsibility kwenye mahusiano yao.
 
Akili zako zimejaa uoga halafu unatafuta followers katika grup lako la waoga, sijaona kitu hapo zaidi ya uoga tu na kutojiamini..kuna wanawake wanaojiheshimu na wenye maadili wanaoweza kuishi maisha yoyote,, usifananishe walevi na masista duu wa mitaani na wanawake wenye sifa za kuolewa. UMEFELI
 
Mimi pia nina sita sita kuoa lakini lakini sio kwa hoja mufilisi kama zako. Sasa ww endelea kujidanganya eti ukimwachia hela nyingi mkeo ndio utakukuwa huchapiwi. kalagabao
 
Sio kila mtu anaoa mke, wengine wanaoa mkeka! Ni heri ukosee kujenga Nyumba kuliko kukosea Kuoa!
 
Somethings are realy difficulty to understand in a normal life, even a wisest person in a world of menkind can not explain it, sometimes I ask myself what is the reality! how does it look like?????


Haujui Kiingereza!

​
 
Back
Top Bottom