Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Katika Mila na desturi za Tanzania shikamoo ni salamu unayompa mtu aliyekuzidi umri. Nimekutana na watu wazima waliokwepa salamu hii. Mfano mtu mzima uliyemuajiri, anaitikia vizuri shikamoo za wengine lakini shikamoo kutoka kwa boss inamsumbua.
Pamoja na kuwa kijana au binti unaeweza kumzaa akawa boss wako lakini haibadili ukweli kuwa uliiona dunia kabla yake na hii ni heshima unayostahili. Hizi ni Mila na desturi zetu.
Maoni yenu tafadhali mtu mzima asiyetaka salamu ya shikamoo nimpe salamu gani?