Hadhi ya mwanaume na Dunia ya kisasa

Jack Daniel

JF-Expert Member
Sep 23, 2021
2,149
10,390
Mambo yanaenda kasi, mambo yanaenda mbio na Miaka nayo Inakatika, nakumbuka juzi Kati tu nilikuwa mtoto ninayechapwa nikikosea.

Lakini leo nina familia yangu, namuona mwanangu Binti wa kike alivyomkubwa, ni kama juzi tu yaani, watu waliponipa hongera ya kuitwa baba, lakini maisha yanavyokimbia, Leo hii nashindwa kushinda na singilent hapa home,

Unajua kwanini?

Ni Mila na desturi za kabila langu na Africa kiujumla, si vyema kuchangamana na Binti aliyevunja ungo, Naam nimekuwa mtu mzima Sasa.

Namwangalia mke wangu nagundua naye umri umeenda, namna anavyoongea na kupangilia maneno, namna anavyovaa natambua anajua Nini avae mbele ya watoto wake wa kiume.naam mke wangu kipenzi amekuwa mkubwa Sasa.

Nawasha PC yangu najaribu kuingia kunako social network ili nipoteze muda nakutana na posts zenye vitimbi, Mikasa na uchafu kibao, kwa hasira naizima kabisa, halafu baada ya muda kidogo najikuta nacheka kwanini nizime na sijawahi kuzima, Sasa watu wangu wa Telegram na Whatsapp business watanipataje naamua kuacha tu.

Natoka nje kidogo, ili nijichanganye na wahuni wa mtaa nagundua naamkiwa sana, yaani shikamoo zimekuwa nyingi tofauti na zamani, hapa nanoti kitu tena.natakiwa kubadilisha style ya uvaaji na unyoaji kwani ni mtu mzima tayari na nauendea uzee.

Lakini pamoja na kwamba najiona jamaa fulani wa mjini, nagundua nimepitwa na vingi, hususani misemo ya mjini, unajua kwanini?

Ni kwasababu Kuna baadhi ya maneno nikiongea nakosolewa mara Moja na napakaziwa mambo makubwa kiasi cha kutaka kupigana, lakini napigana na nani?
Maana zaidi ya watu kumi wote wapo upande mmoja.

1.leo hii mwanaume huwezi kumsifia mwanaume mwenzio kirahisi, utaambiwa ni shoga au una elementi hizo, lahaulaaaa.

2.leo hii hata midomo yako ikiwa mikavu huwezi kuilamba mbele za watu utakuja kuonekana ni wale wale kumbe masikini siyo.

3.leo hii mtu akinyooshewa kidole kuwa anapumuliwa, usimtetee eti hata kama una uhakika wanamzushia maana utazushiwa jambo kama vile unaamulia mwizi mbele ya wenye hasira Kali.

4.leo hii unaweza kulipenda shati au fulana, yaani mwenyewe unajua litakukaa, Sasa ole liwe na rangi na tafsiri wanayoijua wananzengo, utasikia tu tayari yule.

5.tuna washikaji, tuna Wana tunawakubali kinoma, Sasa ole wako uoneshe unamkubali sana huyo mchizi, basi utaambiwa aidha unamtaka umfanye au unataka ufanywe. Lahaulaaaa.... Dunia hebu nishushe kwanza.

6.leo hii huwezi kukumbatiana na mwanaume mwenzio, awe Boss wako, Mfanyakazi mwenzako n.k.
Utaambiwa tayari.

7.leo hii hata Role models wetu hatuwasemi hadharani, siku ukikwea pipa kwenda zako Sri Lanka kuuza Ruby utaambiwa , kamfuata bwana wake. lahaulaaaa Mimi niwe na bwana! Dunia tusamehe kama tumekosea.


Tuzidi kumuomba MUNGU na tukemee ushoga all Men tunadhalilika sana yaani.
 
Meipenda hiyoo, Leo kuna nyimbo ukiplay kwa wahuni , utaambiwa unapigo za , Dunia kwishaa
 
Back
Top Bottom