Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,942
- 3,606
Mwanaume mmoja Raia wa Nigeria
ambaye anaishi Afrika Kusini,
amenunua gari ya kifahari aina ya
Mercedes-Benz G-class, na kumpa
mwanaume mwenzake, ili kumuomba
msamaha kwa kumpa ujauzito mke
wake walipokuwa wakichepuka.
Gari aina ya Mercedes-Benz G-
class.
Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina
la John, amenukuliwa na moja ya
mtandao wa habari wa Afrika Kusini
unaoitwa Daily Live, akisema kwamba
mume wa mchepuko wake huyo
alimsamehe mara tu baada ya
kumkabidhi gari hiyo.
“Najua nilichokifanya sio kizuri, lakini
najisikia vizuri amepokea zawadi
yangu. Amekubali kuwa mke wake
ambaye ni 'girl friend' wangu ni
mjamzito na hivi karibuni atajifungua
mtoto wa kiume ambaye ni wa kwangu.
Mwanzoni alikuwa na hasira lakini
nilipompa gari hasira zake zilimuisha”,
alinukuliwa John.
Mtandao huo ulipofanya mazungumzo
na mwanaume mwenye mke wake
alinukuliwa akisema kuwa..... “Itakuwa
ni kosa kuniambia mi ni mpumbavu,
suala limeshatokea na hatuwezi
kulifuta, tulikaa chini tukayamaliza
kama wanaume, biblia imesema
tusamhe na kusahau. Siku zote
nilikuwa na ndoto ya kuendesha G-
Wagon, Krismas imekuja mapema
kwangu na familia yangu”.
Mwanaume huyo aliendelea kusema
kwamba ...”mtoto atazaliwa siku si
nyingi nami nitamjali kama mwanangu,
baba yake akitaka kumchukua
kumpeleka kwao Nigeria sitajali,
nitampa ushirikiano wote mke wangu,
hiyo ndio ndoa. Nampenda mke wangu
na sitamuacha kwa sababu ya ujauzito
wake wa bahati mbaya”.
Imetafsiriwa kutoka African Spotlight
ambaye anaishi Afrika Kusini,
amenunua gari ya kifahari aina ya
Mercedes-Benz G-class, na kumpa
mwanaume mwenzake, ili kumuomba
msamaha kwa kumpa ujauzito mke
wake walipokuwa wakichepuka.
Gari aina ya Mercedes-Benz G-
class.
Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina
la John, amenukuliwa na moja ya
mtandao wa habari wa Afrika Kusini
unaoitwa Daily Live, akisema kwamba
mume wa mchepuko wake huyo
alimsamehe mara tu baada ya
kumkabidhi gari hiyo.
“Najua nilichokifanya sio kizuri, lakini
najisikia vizuri amepokea zawadi
yangu. Amekubali kuwa mke wake
ambaye ni 'girl friend' wangu ni
mjamzito na hivi karibuni atajifungua
mtoto wa kiume ambaye ni wa kwangu.
Mwanzoni alikuwa na hasira lakini
nilipompa gari hasira zake zilimuisha”,
alinukuliwa John.
Mtandao huo ulipofanya mazungumzo
na mwanaume mwenye mke wake
alinukuliwa akisema kuwa..... “Itakuwa
ni kosa kuniambia mi ni mpumbavu,
suala limeshatokea na hatuwezi
kulifuta, tulikaa chini tukayamaliza
kama wanaume, biblia imesema
tusamhe na kusahau. Siku zote
nilikuwa na ndoto ya kuendesha G-
Wagon, Krismas imekuja mapema
kwangu na familia yangu”.
Mwanaume huyo aliendelea kusema
kwamba ...”mtoto atazaliwa siku si
nyingi nami nitamjali kama mwanangu,
baba yake akitaka kumchukua
kumpeleka kwao Nigeria sitajali,
nitampa ushirikiano wote mke wangu,
hiyo ndio ndoa. Nampenda mke wangu
na sitamuacha kwa sababu ya ujauzito
wake wa bahati mbaya”.
Imetafsiriwa kutoka African Spotlight