Aliyemfuata Rais Kikwete Ikulu apokewa kishujaa..................

Huo ni ujinga.Kama mtu anayeendesha pikipiki aina ya SANLG toka dar hadi Makambako anapofika tu anakimbizwa hospitali,huyo wa baiskeli toka Geita hadi Dar alikuwa salama kweli?Upuuuuzi mtupu.Huyo lazima tuchunguze akili yake.Isije ikawa aliugua sana utotoni.
 
great thinkers,msimlaumu kijana wa watu kama kweli hayo yoote ni kweli inaonekana kijana ni mtu makini sana wahusika wa michezo waanze mtafuta twaweza jipatia medali za gold za kumwaga ktk anga za uendeshaji bike wa mwendo mrefu atiiiii,mana kijana anaoneka ana mota ktk miguu yake.anaweza kutuletea japo tujisifa ili mkwere azidi julikana,sijui why jk didnt thought of ths idea.:target:
 
Wednesday, 08 December 2010

NA PETER KATULANDA, GEITA

MKAZI wa Kasamwa wilayani Geita, Mussa Dotto, ambaye alitembea kwa baiskeli hadi Dar es Salaam, kumpongeza Rais Jakaya Kikwete, amerejea kijijini kwake na kupokelewa kishujaa.

Dotto (35), aliendesha baiskeli kutoka kijiji cha Chabulungo hadi Singida akiwa njiani kwenda Dar es Salaam, kumpongeza Rais Kikwete kwa kuchaguliwa kuongoza tena, alipokewa juzi huku akiwasilisha salamu za rais kwa kuwataka vijana kufanya kazi kwa bidii.

Aliwaeleza vijana wenzake kijijini hapo kuwa, hawana budi kusoma kwa bidii kwani ndiyo silaha ya mafanikio katika maisha.

Mapokezi na sherehe za kumpongeza Dotto, zilifanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Bungíwangoko na kuhudhuriwa viongozi mbalimbali wa CCM, wazazi na mamia ya wananchi.

"Rais Kikwete anawasalimia sana wana Bungíwangoko na Geita, anatuomba tujitahidi kuchapa kazi, vinginevyo tutaendelea kulaumu viongozi na kuichukia serikali," alisema huku akishangiliwa.


Alisema kuwa Rais Kikwete alimuasa kuwa kila mwananchi wakiwemo wakulima, watimize wajibu wao kwa kuchapa kazi na wasichukulie elimu kama jambo la mchezo.

"Vijana wenzangu Rais anatutaka tuchape kazi, maisha bora hayaji kwa kukaa tu bila kufanya kazi kwa bidii, wanafunzi someni kwa bidii, acheni kudharau elimu, maisha mazuri na bora yanataka elimu," alieleza.

Awali, Mwakilishi wa Rais Kikwete katika sherehe hizo, Joseph Makirikiri, alisema uhodari na mapenzi ya Chama alioonyesha Dotto yanapaswa kuigwa na vijana wengine.

Makirikiri, ambaye alionyesha kushtushwa na mapokezi hayo makubwa kwa Dotto, alisema wananchi wana kila sababu ya kufanya jambo kubwa la maendeleo kama kumbukumbu ya Dotto.

Katibu wa UVCCM wa Mkoa Mwanza Josephat Ndolango, alisema Dotto amekitangaza kijiji hicho na kwamba, hana budi kuenziwa na kusema milango ya CCM iko wazi kwa vijana wengine wenye nia kama yake.

Pamoja na zawadi za baiskeli mbili alizozawadiwa Dar es Salaam, Dotto pia alizawadiwa baiskeli nyingine na diwani wa Kata ya Nzela, Joseph Kasheku.

Badala ya kurudi na angalau Power Tiller amerudi na baiskeli mbili zaidi??? Na anapokelewa kishujaa?
 
Mbona alichofanya na ujumbe alioleta havifanani. Amewaambia vijana wasome kwa bidii???? bila kuendesha biskeli alikuwa hajui hadi alipofika ikulu?? uwiii tanzania tunaenda kinyumenyume
 
Yaani mtu ananpanda baiskeli kwenda kumpongeza mchakachuaji kwa uwizi wake wa kura! What a waste! Zitakuwa ni propaganda za CCM kutaka kumfanya JK aonekane anapendwa. Machungu ya kuibiwa kura CHADEMA bado ndo kwanza yanaanza!
 
For what purpose? kama tukijua huko njiani alifanya nini, kama alihamaisha watu kuhusu jambo fulani la maana kwa jamii na kwa taifa naweza kukubaliana naye. Lakini kama ndio ule ujinga wa kutembea na kujitaftia sifa, atakuwa ni mjinga wa mwaka 2010.
tunaweza kuongezea hapo! ni mpenda sifa wa mwaka
 
Back
Top Bottom