Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Wednesday, 08 December 2010
NA PETER KATULANDA, GEITA
MKAZI wa Kasamwa wilayani Geita, Mussa Dotto, ambaye alitembea kwa baiskeli hadi Dar es Salaam, kumpongeza Rais Jakaya Kikwete, amerejea kijijini kwake na kupokelewa kishujaa.
Dotto (35), aliendesha baiskeli kutoka kijiji cha Chabulungo hadi Singida akiwa njiani kwenda Dar es Salaam, kumpongeza Rais Kikwete kwa kuchaguliwa kuongoza tena, alipokewa juzi huku akiwasilisha salamu za rais kwa kuwataka vijana kufanya kazi kwa bidii.
Aliwaeleza vijana wenzake kijijini hapo kuwa, hawana budi kusoma kwa bidii kwani ndiyo silaha ya mafanikio katika maisha.
Mapokezi na sherehe za kumpongeza Dotto, zilifanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Bungíwangoko na kuhudhuriwa viongozi mbalimbali wa CCM, wazazi na mamia ya wananchi.
"Rais Kikwete anawasalimia sana wana Bungíwangoko na Geita, anatuomba tujitahidi kuchapa kazi, vinginevyo tutaendelea kulaumu viongozi na kuichukia serikali," alisema huku akishangiliwa.
Alisema kuwa Rais Kikwete alimuasa kuwa kila mwananchi wakiwemo wakulima, watimize wajibu wao kwa kuchapa kazi na wasichukulie elimu kama jambo la mchezo.
"Vijana wenzangu Rais anatutaka tuchape kazi, maisha bora hayaji kwa kukaa tu bila kufanya kazi kwa bidii, wanafunzi someni kwa bidii, acheni kudharau elimu, maisha mazuri na bora yanataka elimu," alieleza.
Awali, Mwakilishi wa Rais Kikwete katika sherehe hizo, Joseph Makirikiri, alisema uhodari na mapenzi ya Chama alioonyesha Dotto yanapaswa kuigwa na vijana wengine.
Makirikiri, ambaye alionyesha kushtushwa na mapokezi hayo makubwa kwa Dotto, alisema wananchi wana kila sababu ya kufanya jambo kubwa la maendeleo kama kumbukumbu ya Dotto.
Katibu wa UVCCM wa Mkoa Mwanza Josephat Ndolango, alisema Dotto amekitangaza kijiji hicho na kwamba, hana budi kuenziwa na kusema milango ya CCM iko wazi kwa vijana wengine wenye nia kama yake.
Pamoja na zawadi za baiskeli mbili alizozawadiwa Dar es Salaam, Dotto pia alizawadiwa baiskeli nyingine na diwani wa Kata ya Nzela, Joseph Kasheku.