TANZIA Aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Mifugo awamu ya kwanza, Mzee Herman Kirigini afariki dunia

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Mifugo na Mjumbe wa Baraza la mwisho la Mawaziri la mwl. Julius k. Nyerere mhe. Herman Kirigini afariki dunia nyumbani kwake Musoma.

----

ALIYEKUWA mbunge wa zamani wa jimbo la Musoma vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Herman Kirigini amefariki dunia.

Akizungumza na Mzawa kwa njia ya simu mtoto wa marehemu na kada wa Chama cha Mapinduzi Paul Kirigini amesema mzee Kirigini amefariki mei 23 kwenye hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara.

Paul amesema amepokea kifo cha mzee Kirigini kwa masikitiko makubwa kwa kuwa bado walikuwa wakihitaji ushauri wake.

Amesema hayo ni mapenzi ya Mungu na kilichobaki ni kumuombea na kuhusu taratibu za mazishi zitatolewa na familia.

Paul amesema msiba wa mzee Kirigini upo nyumbani kwake Kata ya Kamnyonge manispaa ya Musoma na taratibu nyingine za mazishi zikiendelea.

Marehemu Herman Kirigini,alikuws mbunge wa jimbo la Musoma vijijini toka mwaka 1980 hadi mwaka 1985 na licha ya Waziri wa Kilimo na Mifugo amewahi pia kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM na serikali.

Kirigini.jpg

Mzee Herman Kirigini​
 
Huyu Mzee Mungu kamweka sana ,kumbe alikua hai,? familia Impe Mungu shukrani kwa maisha marefu hayo .
Tulikuwa na Mwalim Kirigini , mwalimu wetu wa English, Obay Primary school , ninakumbuka enzi hizo za "Good Afternoon Mrs Herman" ,alikua mrembo sana , natumai yupo na afya bora .
Hivi yule Mbunge Rosemerry ndio ShaKa? alikua demu mrembo kinoma enzi hizo, alikua darasa la juu yangu kaa mawilia au matatu , ila nilikua namzimikia kinoma , nakumbka alikua na dada yake sikumbuki jina ,hivyo nina wachanganya ,ila niliye mzimia ni nadhani ni Shaka ambaye alikua mdogo wa huyo dadake .
Mungu aendelee kumweka mahali pema Mr Kirigini.Amen
 
Rose aka Shaka alikuja kuwa mbunge wa ccm viti maalum.
 
Back
Top Bottom