PreGE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Shinyanga, Emmanuel Ntobi na Glory Tausi wajiunga na ACT Wazalendo

PreGE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Shinyanga, Emmanuel Ntobi na Glory Tausi wajiunga na ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi amehamia chama cha ACT Wazalendo na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu.

Akizungumza leo Juni 03, Ado amesema "wapiganaji ambao wamegonga mlangp hapa ACT tumekuwa tukiwapokea leo ninayo furaha ya kuwaleta mbele yenu wapigananaji wakubwa wawili katika siasa za Tanzania ambao wamepata heshima ya kupokelewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo"

"Tunao wapiganaji wawili hapa tunaye ndugu yetu Emmanuel Ntobi yeye mpaka hivi sasa ni kada mwandamizi wa CHADEMA ameniandikia barua rasmi jana na kusema anayo nia ya kujiunga na ACT Wazalendo wa pili ni ndugu Glory Tausi na yeye ni kada mwandamizi"

1748948603026.png
Ado ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha watu wengine ambao wanataka kujiunga na chama hicho kuwa nafasi zipo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Baada ya kuwapokea wanachama hao wapya Ado amewakabidhi Kadi ya mwanachama ya Maalim Seif pamoja na Katiba ya chama hicho.

1748948636082.png

"Tulikaa na baadhi ya wenzangu tuliokuwa G55 tukapitia baadhi ya katiba, tukapitia baadhi ya vyama, lakini kiukweli kwa sasa hivi anayeweza kuiangusha CCM ni ACT Wazalendo." - Emmanuel Ntobi, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

 
Back
Top Bottom