Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Christopher-Bageni-696x654.jpg

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni, aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kuwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro, amepinga adhabu hiyo katika Mahakama Rufaa jijini Dar es Salaam.

SP Bageni amewasilisha maombi ya mapitio Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo yamepangwa kusikikizwa Juni 16, mwaka huu mbele ya jopo la majaji watatu, Stellah Mugasha, Ferdinand Wambali na Rehema Kerefu.

Katika maombi yake ya mapitio, Bageni amewasilisha sababu mbalimbali za kupinga adhabu hiyo ikiwamo kwamba jopo la majaji lilifanya makosa ya dhahiri katika muonekano na hivyo kusababisha haki kutozingatiwa katika kutoa hukumu hiyo.

SP Bageni alihukumiwa adhabu hiyo Septemba 16 mwaka 2016 na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mbele ya jopo la majaji watatu, Jaji Benard Luanda, Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage.

Mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) akipinga aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe na maofisa wenzake watatu akiwemo Bageni kuachiwa huru na Mahakama Kuu mwaka 2009.

Hukumu hiyo ilisomwa na aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa wakati huo, Jaji John Kahyoza. Aliwataja wajibu rufani kuwa ni Zombe, SP Bageni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Katika kesi hiyo, wafanyabiashara wa madini waliouwawa ni Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva taksi, mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Juma Ndugu.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika Msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Mtanzania
 
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
 
Kwa nini rufaa imekatwa awamu hii ya tano baada ya mda mrefu sana toka hukumu?
Huenda tangazo la polisi kutoshtakiwa kwa awamu hii likamuokoa mhalifu na muuji kisa ni polisi. Kwa sasa hivi inaonekana sheria haiwahusu polisi
 
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
Hii adhabu haitekelezwi ili kurudisha waliouawa au kuboresha maisha ya ndugu walioachwa au watakaoachwa, inatekelezwa ili mimi na wewe tuogope kufanya uhalifu wa aina hiyo, kama hakuna adhabu ya kifo, mimi naweza kuja nyumbani kwako, nikakulawiti wewe, mke wako na binti yako, kisha nikawaua kwa kuwachinja mkeo na binti yako, Je, wewe uliyebaki, utajisikia vizuri kuniona mimi niko hai ili mradi tu niko gerezani? Gerezani ni maisha tu kama maisha mengine, kuna watu kule wanakula vizuri tu na kuishi vizuri..

Je, ni haki kwa aliyekatisha maisha ya wengine kikatili, kuendelea kula bata tu huko gerezani?
 
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
Kumuua BAGENI hakutarudisha uhai wa kina Chigumbi ila itakua fundisho kwa polisi wengine wanao ua watu wasio na hatia na kuwaibia. Vile vile kutaonyeaha kwamba institutions za serikali hii ziko hai na serikali inasimamia haki sio serikali ya wacha wapigwe tu kama untouchable mmoja alivyosemaga. Binafsi najua Bageni alihusika kuwaua wale watu huku akijua ni kosa mbele ya binadamu na dhambi mbele za Mungu.
Otherwise atuambie walikufaje au nani aliwau?
 
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
We unapendekeza adhabu gani?
 
Back
Top Bottom