Aliyekuwa mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la zima moto na uokozi, Wenzake wahukumiwa

Hizi mahakama ni za kipuuzi kama walivyo majaji nao wapuuzi tu, juzi mtu kahukumiwa kwenda jera maisha kwa kukamatwa na mirungi leo hawa wanahujumu uchumu unawatoza faini ya laki tatu?
Nakuelewa mrungi ambao jirani zetu kenya sio kosa ......!
 
Hela zote hizo eti faini laki 3 au jela miezi sita . Pumbafu sana nilitegemea atapigwa japo miaka kumi na faini milioni mia sta
Hapo nakumbuka kuna mjumbe wa bunge la katiba alipendekeza kuwepo na utaratibu wa kufuatilia mahakama zetu, unawezo ona kabisa hata wewe usiejua sheria kuwa hapa kuna walakini, na wao hawajali eti kwa kuwa hawaingiliwi na wako huru na hamna wa kuwahoji, hawa mahakimu ni binadamu na wengi ni majibu tu, wapo kimya kama malaika kipindi hiki!
 
Eti kesi ya kugushi nyaraka na kuhujumu uchumi..

Amehukumiwa kulipa 300,000/= kila kosa au jela miezi 6!!!

Hizi sheria zilitungwa kwa ajili ya maskini na wanyonge maana wao hukumu zao ni miaka mingi jela na faini kubwa kubwa.
Mkuu unashangaa haya, hii ndiyo TZ. Umesahau ya mramba na mwenzake?.
 
Aliyekuwa Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani katika jeshi la kuzima moto na uokozi na Bw. Naamini Hendry Sangiwa pamoja na Mkandarasi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd Bw. Webu Manoth Masawe wamehukumiwa leo tarehe 24/3/2016 kwa kesi ya kuhujumu uchumi katika Mahakama ya wilaya ya Ilala. Hukumu hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Hassan.

Washtakiwa tajwa hapo juu walishtakiwa kwa makosa 7 yakiwemo Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kutumia Nyaraka Kumdanganya Mwajiri kinyume na kifungu cha 22 na 31 mtawalia vya Sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007, Kughushi Nyaraka kinyume na Kifungu cha 333, 335 (d) (1) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, na kuisababishia Serikali hasara kinyume na Aya ya 10(1) ya Jedwali la Kwanza, Kifungu cha 57(1) na 60(1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200.

Mnamo mwaka 2009 Serikali ilitoa zabuni ya Ujenzi wa uzio wa Chuo cha Zimamoto na Uokozi kilichopo Mbopo Bunju katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Kiareni Investment Ltd (Mzabuni), ilipatiwa zabuni hiyo na kulipwa Kiasi cha Shilingi 81, 963, 360/=.

Hata hivyo taratibu za utoaji zabuni hazikufuatwa, na Mzabuni ambaye ni Kampuni ya Kiareni Investment Ltd, alifanya kazi yenye thamani ya kiasi cha Shilingi 13, 784, 652/= tu kati ya fedha yote aliyolipwa.

Ili kuwezesha malipo ya Shilingi 81, 963, 360/= kulipwa pasipo kazi kukamilika, Washtakiwa walitoa zabuni kwa Mkandarasi pasipo Mkataba (LPO), na Kughushi Hati ya kuonesha kazi imekamilika (Certificate of Works Completion).

Washitakiwa wote watatu walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mwanzoni mwa mwaka 2014 na kusomewa mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mkazi Hassan, ambapo washitakiwa walifunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi No. 06/2014.

Upande wa Jamhuri katika Kesi hii uliwakilishwa na Wakili STANLEY HILMAR LUOGA akisaidiana na Wakili EMMANUEL JACOB, wote waendesha Mashitaka wa TAKUKURU Makao Makuu.

Upande wa washtakiwa wote waliwakilishwa na Wakili wa Kujitegemea MDUMA.

Upande wa Jamhuri uliita Mashahidi 7 na kupeleka vielelezo 21 ili kuthibitisha kesi dhidi ya washtakiwa. Upande wa washtakiwa hawakuita shahidi hata mmoja walijitetea wenyewe.

Mshitakiwa wa kwanza Dotto Salehe Mgogo, ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Mafunzo wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika idara ya Jeshi la Zimamoto na Uokozi alifariki dunia mwaka 2014 baada ya kusomewa mashitaka na hivyo Mashitaka dhidi yake yalifutwa kwa mujibu wa sheria.

Kufuatia kifo cha Mshitakiwa wa kwanza, Mshitakiwa wa Pili Bw. Naamini Hendry Sangiwa ambaye alikuwa Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Katika Jeshi la Zimamoto na Uokozi alikuwa anakabiliwa na makosa manne (4) ambapo makosa mawili ni ya Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kughushi na Kuisababishia Serikali Hasara, ametiwa hatiani katika makosa yote mawili ya Matumizi ya Madaraka na kupewa adhabu ya kulipa faini ya Tshs.300, 000 kwa kila kosa la Matumizi Mabaya ya Madaraka kama atashindwa kulipa faini, kwenda jela miezi 6 kwa kila kosa.

Katika Kosa la Kughushi Nyaraka, Mshtakiwa ametiwa Hatiani na Kuamriwa kutotenda kosa lolote la jinai kwa muda wa miezi 12.

Mshitakiwa wa tatu ambaye ni Bw. Webu Manoth Masawe, ambaye ni Mkandarasi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd, anakabiliwa na Kosa moja la Kuisababishia Serikali Hasara.

Mahakama imemtia hatiani na kumpa adhabu ya kwenda Jela miaka mitatu (3) pamoja na Kuirudishia Serikali kiasi cha Shilingi 67, 913, 748/= ikiwa ni hasara aliyoisababishia Serikali.

IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
24 MACHI, 2016
Ukiisha mwaka huu bila kusikia TAKUKURU kupitia wizara husika mnapeleka sheria za kurekebisha adhabu. Haiwezekani adhabu ikawa laki 3. Hii ni aibu
 
Let me conclude kwamba hii nchi mtu ukiiba ma billions jela utaisikia tu ila ukiiba vi mill 4 ujue jela inakuhusu
 
Sioni hata maana ya hii hukumu milioni 67 jela wakati wanaosemwa wamekwiba mamilioni wapo nje wanaponda raha tu...

Hakuna la maana hapoo mpaka tuone wa mabilioni wakiwa ndani...otherwise kufanya watanzania kuwa hawana akili.
 
Milioni 81 wanahukumiwa
Mabilioni wapo kitaa
Nakupenda Tanzania

Mkuu achana hill la mirungi, this week kuna muhasibu kahukumiwa miaka 23 jela kwa kosa la kuisababishia serikali hasara ya mil 4, Lakini huyu aliyesababisha hasara ya mil 81 anahukumiwa kwa kupewa option ya adhabu either laki 3 au jela miezi sita. Huu ni upuuzi at the highest level kulikotukuka.


labda sheria zina macho, na kutoa hukumu tofauti kulingana na hadhi au wasifu wa watuhumiwa...

na wasiwasi na maamuzi ya kimahakama ktk kutoa hukumu.
 
Mauza uza ya mahakama zetu nchini. Mwizi wa kuku anakwenda jela miezi 3-6, mbeba mirungi jela maisha, muhujumu uchumi wa thamani ya tsh 67m faini laki tatu au jela miezi sita wakati muhasibu mwingine alihukumiwa jela miaka 20 kwa uhujumu wa tsh 4m.
 
Huwa najiuliza kwa nini katika taarifa au habari za wizi na kuhujumu uchumi majina ni yale yale majitu ya kutoka kule!?
 
Back
Top Bottom