Aliyekuwa kocha mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike, amefutwa kazi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Wanampangia mwalimu kikosai cha timu halafu wanajisafisha kwa kumfukuza. Tunarudi pale pale (Zero Sum) . Bora wajitazame wenyewe kwanza
 
timu ya taifa inachukua wachezaji walio fiti kutoka vilabuni, ligi yetu sio ya ushindani, tff inaamua tu mwaka huu ubingwa wende wapi, watu wananunua mechi mchana kweupee kwenye ligi, wenzetu wanapeleka watoto wao kwenye academy bora kabisa duniani huko, sisi tff wanaendesha michuano ya mikoa ya u15 na u17 wakati huo kuna umisetta na umitashumta inafanyika, kila kitu hakipangiliwi vizuri
 
Ingekuwa vyema kama uongozi wa TFF nao ungejiuzulu kwa kuwajibika kutokana na timu ya taifa ilivyoboronga kama walivyofanya wenzao wa Egypt. Lakini kutokana na ulevi wa madaraka hawawezi kufanya hivyo na ndiyo maana mpira wa miguu utabaki ngonjera tuu.
Cha ajabu ni kuwa tunawafahamu wachawi wetu lakini tunasita kupaza sauti kuwa wang'atuke.
 
Mtafukuza sana makocha, Bongo sisi kila kitu bado sana.
Makonda alisema Stars wanatekeleza Sera za CCM sasa Amunike amezijulia wapi? Ili timu ifanye vizuri zaidi katika kutekeleza Sera za CCM apewe timu mzee Polepole kwani ameiva hasa.
TFF walijua kabisa kuwa timu inatekeleza Sera kulikuwa na sababu gani kumleta Amunike kama sio upotevu wa fedha bure!
KIGYUMU CHAMA CHA MAPUNDUZI!!
 
Aiseeee !!!
 
Daah. Comments kama hizi hata kama pressure iko juu itakuwa "normalized" tuu
 
si kila anaejua kucheza mpira ukajua basi hata kuufundisha anaweza pia, mana kama ingeelikuwa hivyo basi Pele angekuwa kocha na mourinho angekuwa muokota mipira
 
Kamati mfu ya "kuhamasisha ushindi" nadhani nayo ilishajifia zamani. Yule mwenyekeit wake na yeye apigwe ban na TFF kujihusisha na mambo ya Taifa Sars
 
Katika asilimia 100 tumetoa 0.001 percent ya shida ya soka la Tz
 
Hapa wamefanya kosa kubwa sana kumuondoa Amunike kwa maana sisi hata kushiriki kwenyewe tulitegemea best looser yaaan Lethoto atoe draw ndo tupite,
Wamefanya vyema sana kumtupia virago. Tactically the guy is inept. Tulishindwa kucontrol game yetu na Kenya kwa kuwa Coach hana experience wala plan Bs. Mechi na ALGERIA tuligongwa kindezi sana. As much as Algeria wapo vizuri, hatukupaswa kutaka kwenda nao toe-to-toe. A new coach is needed.
 
Ni muda mwafaka sasa kwa TFF kumrudisha Kim Paulsen na kumkabidhiwa majukumu yote na vitendea kazi vinavyotakiwa.

Tuweke maslahi ya UTAIFA mbele, tusichanganye mahaba ya vilabu vyetu vya ndani kwenye timu ya TAIFA.

Tuache udalali kwenye mshahara wa kocha, apewe pesa yake"FULL"

Tuache siasa kwenye mpira, tusimwingilie mwalimu tumwache afanye kazi yake.

Tumpatie mwalimu malengo yetu, ya muda mfupi na ya muda mrefu.

Naamini tutafika.... kwanini tushindwe wakati kila kitu tunacho, uwezo, ari na mazingira mazuri ya kucheza mpira tunayo.
 
Hivi ni kocha gani aliwahi kuja Tanzania akaondoka tunamsifu akiwa na record nzuri? Kila kocha aliyewahi kufundisha Tanzania aliondoka kwa aibu.
Ukizungukwa na wababaishaji, ukaenda kuwafundisha ama kuwafundishia vijana wao na hata ukiweza kuwasogeza,ila matokeo 'makubwa ya ajabu ya kutaraji afya njema toka lishe mbovu ya miaka', yasipofanikiwa ndani ya kipindi kifupi,taraji kutolewa kafara,kufukuzwa na kupewa matusi ikiwezekana, wakati wazalisha maanguko halisi wakikomalia ofisi na viti vyao bila haya,aibu wala huruma au uzalendo!
 
Nakuunga mkono 100% + .Kukimbilia kumtimua kocha,nadhani nia hasa ilikuwa ni kuficha uozo halisi upo wapi, ili wababaishaji wabaki/wakae salama bila kuulizwa,na kutupa lawama kwa aliyetimuliwa na hayupo kujitetea hata kama angependa kufanya hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…