Aliyekuwa kocha mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike, amefutwa kazi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Kama hatuna uzoefu kwa kiwango cha kushindana kimataifa hata akija Morinyo sidhani kama atabadilisha mambo. Kwani ni kocha gani aliyeivusha hii timu kwenda kwenye hizo fainali
Kati ya makosa Mahali Viongozi Wa Tff Wanakoseaga ndiyo hapo. Kubadili waalimu kila tunapofungwa.

Inatakiwa TFF wawe na Kocha Mkuu anayedumu walau miaka kadhaa, tuseme kama miaka 5 nakuendelea. Akiwa na uwezo wa kufundisha ni vema wakati timu haiko mazoezi kwa mashindano serious akawa anapewa nafasi kufundisha makocha Mikoani.
 
Naamini wamejipanga kumlipa fidia kwa kuvunja mkataba bila kusumbuana. Ni wakati gani viongozi wa TTF watawajibika kwa matokeo mabaya?

Tunataka kuvuna tusipopanda.

Tuwekeze katika soka la vijana, viwanja, na uamuzi. Tujiulize ni lini waamuzi kutoka Tanzania walitumika katika mashindano makubwa?

Waamuzi wanajua na kufuata sheria za mpira?

Yote haya yaangaliwe na si swala la kocha pekee.
 
Ile timu ya Vijana iliyoingia fainali gabon vp mbona tff waliitelekeza hawakuiendeleza
Tuanze hapo

Ova
 
Ile timu ya Vijana iliyoingia fainali gabon vp mbona tff waliitelekeza hawakuiendeleza
Tuanze hapo

Ova
Kazi ya kulea vijana sio ya tff ni ya club, kwani hujui wachezaji wa timu za taifa wanapatikana vipi? Au ulitaka wawalee hadi lini?
 
mawazo yako ndio uhalisia hasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…