PostGE2025 Aliyekosoa mchakato wa uteuzi wa Samia ndani ya CCM, Mzee Godfrey Malisa ashtakiwa kwa UHAINI

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Na mtu na akili timamu kabisa, unajitokeza hapa na fikra za namna hii na unajitambua wewe kuwa bado ni binaadam anayeishi?

Kwanza huyo Polepole alitoa siri zipi hasa! Anatofauti gani na mtu kama wewe kiuhalisia; mbali ya kumhusu Samia na pengine kuhatarisha ulaji mnaoutegemea kwa kuwakandamiza waTanzania?

Polepole alichangia lipi la muhimu sana katika ukombozi wa taifa hili kutoka mikononi mwa watu waovu nyinyi?
Kwani wewe Humphrey Polepole ni nani wako hasa?? Maana povu kama lote
 
Kwenye huu utawala kila mzaliwa wa Tanganyika ni mhaini
 
Huyu mzee Malissa naonaga anaongea ongea tu kupinga uhalali wa Rais nk nk

Ila maneno tu hayatoshi kumtia hatiani kama maneno yale hayako kwenye njama au mipango ya kutaka kumtoa raisi madarakan kwa nguvu.

Hii ndio mfano halisi wa
"Kumkomoa nyani Kundule".
Wanaoupinga urais wa Samuya ni wengi ni mamilioni, utekaji na mauwaji hayajafanikiwa kuzima sauti au kutisha watu ndio wengi zaidi wanazidi kujitokeza kupinga, nyie mna miaka mitano ya kutishia watu, kutesa na kufungulia makesi ya uhaini
 
Kwani wewe umewahi kumsikia au kumfahamu Godfrey Malisa kabla ya issue ya uchaguzi wa CCM?
Namjua muda mrefu ila hiyo sio fact. Kila anayetoa mawazo tofauti bila kujali unamjua au humjui anatuhimiwa kuwa anatumika.

Je ni kosa watu kuwa na maoni tofauti au kinzani?
 
Mchungaji Godfrey Malisa, aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro akikabiliwa na kosa la uhaini. Kesi hiyo (Namba 000028333 ya 2025) inatarajiwa kutajwa kesho, Ijumaa, Januari 2, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ally Mkama.

Mchungaji Malisa anashitakiwa chini ya Kifungu 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16) kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023. Anatuhumiwa kutenda kosa hilo mnamo Novemba 16, 2025, katika eneo la Miembeni, Wilaya ya Moshi.

Hati ya mashitaka inadai kuwa mshitakiwa alinuia kuhamasisha umma kushiriki katika mikusanyiko isiyo halali kwa lengo la kumtishia mtendaji mkuu wa Serikali. Inadaiwa kuwa alitoa matamko ya kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kujiuzulu kabla ya Desemba 9, 2025, na kutishia kuanzisha maandamano makubwa nchini iwapo matakwa yake hayatatekelezwa.

Zingatia: Kosa la uhaini chini ya kifungu hicho haliruhusu mshitakiwa kujibu chochote katika mahakama ya chini, na adhabu yake kisheria ni kifo iwapo mshitakiwa atapatikana na hatia.

Kesi hii inakuja wakati kukiwa na mfululizo wa mashitaka dhidi ya watu mbalimbali kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025, ambayo Serikali iliyatangaza kuwa ni haramu.
  • Msamaha wa Rais: Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwafutia mashitaka vijana walioingia kwenye maandamano hayo kwa mkumbo, akibainisha kuwa wengi hawakujua madhara ya vitendo vyao.
  • Kifungu cha 91(1): Baadhi ya washitakiwa tayari wamenufaika na kifungu hiki cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na kuachiwa huru.
Kabla ya kufikishwa mahakamani, Malisa alikuwa akionyesha misimamo mikali dhidi ya uongozi uliopo, ikiwemo:
  1. Kufungua kesi mahakamani kupinga uteuzi wa mgombea urais ndani ya CCM.
  2. Tishio la kufungua kesi ICC: Alitangaza nia ya kuwafungulia mashitaka Rais Samia na IGP Camillus Wambura katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Hadi kufikia kesho, Mchungaji Malisa atakuwa ametimiza siku 30 tangu alipowekwa kizuizini kufuatia kukamatwa kwake nyumbani kwake mwezi Novemba 2025.

Wasifu wa Mchungaji Godfrey Malisa

Mchungaji Malisa (PhD) ana historia ndefu ya ushiriki katika siasa za upinzani na CCM:
  • 2010: Aligombea Ubunge Moshi Mjini (TLP).
  • 2015: Aligombea Urais (CCK) na baadaye Uspika.
  • 2018-2020: Aligombea Ubunge kupitia TLP na NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia CCM.
  • 2025: Alifukuzwa uanachama wa CCM mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kupinga maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa kuteua mgombea urais, jambo lililotajwa na chama kama utovu wa nidhamu na kudhoofisha umoja.
Pia Soma:
Dkt. Malisa awafungulia Kesi Rais Samia na IGP Wambura Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) The Hague

Katika taarifa iliyosambaa Novemba 21, 2025, ilidaiwa kuwepo kwa taarifa mzee huyo (Mchungaji Malisa) alitekwa majira ya usiku nyumbani kwake maeneo ya Msamaria Majengo au Malenga, siku chache baada ya kutoa maazimio ya Kamati ya Kitaifa ya Kurejesha Haki na Amani katika Tanzania.

Unaweza kusoma zaidi hapa: Tetesi: - Inadaiwa Dkt. Godfrey Malisa ametekwa jana usiku akiwa nyumbani kwake
Hamna kesi ya uhaini hapo, ni mambo yale yale judiciary ku side na serikali kuwatosha wakosoaji wake kwa kuwapa kesi za uhaini

That is their only way

System is so corrupted to the core
 
CCM wote matako yenu.kazi kubambika watu kesi za kihuni.Sisi kama GenZ,mnazidi kutuchochea zaidi ili tukiwashe Tena kama ilivyokuwa MO29
 
Kwa kweli kama ndugu angekuwa ni Polepole ningesema apotee tu na asirudi. Ni upumbavu w kuacha kazi inayokupa mshahara kisha unarudi unaanza kutoa siri zake za ndani.

Wangemuacha hai ingekuwa ni kosa kubwa Ki-intelligensia
Si kila anaekosoa ni masikini. Kama unaogopa kukosoa sababu ya mshahara badi huna moral aothority, ww ni fukara mwenye nafasi tu
 
Mchungaji Godfrey Malisa, aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro akikabiliwa na kosa la uhaini. Kesi hiyo (Namba 000028333 ya 2025) inatarajiwa kutajwa kesho, Ijumaa, Januari 2, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ally Mkama.

Mchungaji Malisa anashitakiwa chini ya Kifungu 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16) kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023. Anatuhumiwa kutenda kosa hilo mnamo Novemba 16, 2025, katika eneo la Miembeni, Wilaya ya Moshi.

Hati ya mashitaka inadai kuwa mshitakiwa alinuia kuhamasisha umma kushiriki katika mikusanyiko isiyo halali kwa lengo la kumtishia mtendaji mkuu wa Serikali. Inadaiwa kuwa alitoa matamko ya kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kujiuzulu kabla ya Desemba 9, 2025, na kutishia kuanzisha maandamano makubwa nchini iwapo matakwa yake hayatatekelezwa.

Zingatia: Kosa la uhaini chini ya kifungu hicho haliruhusu mshitakiwa kujibu chochote katika mahakama ya chini, na adhabu yake kisheria ni kifo iwapo mshitakiwa atapatikana na hatia.

Kesi hii inakuja wakati kukiwa na mfululizo wa mashitaka dhidi ya watu mbalimbali kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025, ambayo Serikali iliyatangaza kuwa ni haramu.
  • Msamaha wa Rais: Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwafutia mashitaka vijana walioingia kwenye maandamano hayo kwa mkumbo, akibainisha kuwa wengi hawakujua madhara ya vitendo vyao.
  • Kifungu cha 91(1): Baadhi ya washitakiwa tayari wamenufaika na kifungu hiki cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na kuachiwa huru.
Kabla ya kufikishwa mahakamani, Malisa alikuwa akionyesha misimamo mikali dhidi ya uongozi uliopo, ikiwemo:
  1. Kufungua kesi mahakamani kupinga uteuzi wa mgombea urais ndani ya CCM.
  2. Tishio la kufungua kesi ICC: Alitangaza nia ya kuwafungulia mashitaka Rais Samia na IGP Camillus Wambura katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Hadi kufikia kesho, Mchungaji Malisa atakuwa ametimiza siku 30 tangu alipowekwa kizuizini kufuatia kukamatwa kwake nyumbani kwake mwezi Novemba 2025.

Wasifu wa Mchungaji Godfrey Malisa

Mchungaji Malisa (PhD) ana historia ndefu ya ushiriki katika siasa za upinzani na CCM:
  • 2010: Aligombea Ubunge Moshi Mjini (TLP).
  • 2015: Aligombea Urais (CCK) na baadaye Uspika.
  • 2018-2020: Aligombea Ubunge kupitia TLP na NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia CCM.
  • 2025: Alifukuzwa uanachama wa CCM mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kupinga maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa kuteua mgombea urais, jambo lililotajwa na chama kama utovu wa nidhamu na kudhoofisha umoja.
Pia Soma:
Dkt. Malisa awafungulia Kesi Rais Samia na IGP Wambura Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) The Hague

Katika taarifa iliyosambaa Novemba 21, 2025, ilidaiwa kuwepo kwa taarifa mzee huyo (Mchungaji Malisa) alitekwa majira ya usiku nyumbani kwake maeneo ya Msamaria Majengo au Malenga, siku chache baada ya kutoa maazimio ya Kamati ya Kitaifa ya Kurejesha Haki na Amani katika Tanzania.

Unaweza kusoma zaidi hapa: Tetesi: - Inadaiwa Dkt. Godfrey Malisa ametekwa jana usiku akiwa nyumbani kwake
Kwenda kinyume na matakwa ya MamaSamia2025 ni uhaini. Huyu mama Ana uchu n uroho wa hali ya juu wa madaraka.
 
Lini tutaukaribia ubinadamu kwa kupata akili kidogo na kupunguza uhayawani toka kwnye unyamapori tulionao? Sio ajabu watu wanakuja kutalii kuona wanyamamjini na wanyamapori.

Hata kama unamtetea huyu mama mbona mengine ni makosa ya kitoto kabisa? Hilo kubwa la mauaji hata hajajua mwelekeo, na kakaririshwa na kina mchengelwa kaseme unaanzisha maridhiano na kenge watasahau tu, kaibua lingine!

Yani bado wanaona watanzania wa leo ni kama wa miaka ya sabini, umeshika shoka eti unataka maridhiano, my asshole! Watashaa zamu hii
 
Mchungaji Godfrey Malisa, aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro akikabiliwa na kosa la uhaini. Kesi hiyo (Namba 000028333 ya 2025) inatarajiwa kutajwa kesho, Ijumaa, Januari 2, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ally Mkama.

Mchungaji Malisa anashitakiwa chini ya Kifungu 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16) kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023. Anatuhumiwa kutenda kosa hilo mnamo Novemba 16, 2025, katika eneo la Miembeni, Wilaya ya Moshi.

Hati ya mashitaka inadai kuwa mshitakiwa alinuia kuhamasisha umma kushiriki katika mikusanyiko isiyo halali kwa lengo la kumtishia mtendaji mkuu wa Serikali. Inadaiwa kuwa alitoa matamko ya kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kujiuzulu kabla ya Desemba 9, 2025, na kutishia kuanzisha maandamano makubwa nchini iwapo matakwa yake hayatatekelezwa.

Zingatia: Kosa la uhaini chini ya kifungu hicho haliruhusu mshitakiwa kujibu chochote katika mahakama ya chini, na adhabu yake kisheria ni kifo iwapo mshitakiwa atapatikana na hatia.

Kesi hii inakuja wakati kukiwa na mfululizo wa mashitaka dhidi ya watu mbalimbali kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025, ambayo Serikali iliyatangaza kuwa ni haramu.
  • Msamaha wa Rais: Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwafutia mashitaka vijana walioingia kwenye maandamano hayo kwa mkumbo, akibainisha kuwa wengi hawakujua madhara ya vitendo vyao.
  • Kifungu cha 91(1): Baadhi ya washitakiwa tayari wamenufaika na kifungu hiki cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na kuachiwa huru.
Kabla ya kufikishwa mahakamani, Malisa alikuwa akionyesha misimamo mikali dhidi ya uongozi uliopo, ikiwemo:
  1. Kufungua kesi mahakamani kupinga uteuzi wa mgombea urais ndani ya CCM.
  2. Tishio la kufungua kesi ICC: Alitangaza nia ya kuwafungulia mashitaka Rais Samia na IGP Camillus Wambura katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Hadi kufikia kesho, Mchungaji Malisa atakuwa ametimiza siku 30 tangu alipowekwa kizuizini kufuatia kukamatwa kwake nyumbani kwake mwezi Novemba 2025.

Wasifu wa Mchungaji Godfrey Malisa

Mchungaji Malisa (PhD) ana historia ndefu ya ushiriki katika siasa za upinzani na CCM:
  • 2010: Aligombea Ubunge Moshi Mjini (TLP).
  • 2015: Aligombea Urais (CCK) na baadaye Uspika.
  • 2018-2020: Aligombea Ubunge kupitia TLP na NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia CCM.
  • 2025: Alifukuzwa uanachama wa CCM mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kupinga maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa kuteua mgombea urais, jambo lililotajwa na chama kama utovu wa nidhamu na kudhoofisha umoja.
Pia Soma:
Dkt. Malisa awafungulia Kesi Rais Samia na IGP Wambura Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) The Hague

Katika taarifa iliyosambaa Novemba 21, 2025, ilidaiwa kuwepo kwa taarifa mzee huyo (Mchungaji Malisa) alitekwa majira ya usiku nyumbani kwake maeneo ya Msamaria Majengo au Malenga, siku chache baada ya kutoa maazimio ya Kamati ya Kitaifa ya Kurejesha Haki na Amani katika Tanzania.

Unaweza kusoma zaidi hapa: Tetesi: - Inadaiwa Dkt. Godfrey Malisa ametekwa jana usiku akiwa nyumbani kwake
Inaelekea wenzetu hawa akina Malisa walikuwa na ajenga ambayo ni zaidi ya demokrasia nchini. Tanzania ni taifa maskini sana linaloandamwa na madeni lukuki. Haiwezekani watanzania wenzetu waone ni sawa kuchoma miundombinu muhimu kwasababu ya demokrasia. Tanzania sisi tuna demokrasia kubwa kuliko nchi zote za Afrika chini ya Jangwa. Tanzania ndiyo nchi ambayo makabila yanakwenda kuishi sehemu yoyote nchini na kumiliki chochote huko ugenini. Wachaga, wasukuma, wapemba wako nchi nzima bila kuulizwa maswali. Tz kila mtu ana uhakika wa kuiona kesho yake na kuwaona wajukuu wake. Tz kabila yote yanasoma na kuajiliwa na kufanyakazi pamoja.

Hawa jamaa walimkataa Samia hata kabla ya kuapishwa kuwa Rais, walikuwa wana Rais wao ambaye alikuwa nje ya Katiba.

Wacha mahakama ikachambue, kama hana hatia ataachiwa na kurudi nyumbani kwake.
 
Mchungaji Godfrey Malisa, aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro akikabiliwa na kosa la uhaini. Kesi hiyo (Namba 000028333 ya 2025) inatarajiwa kutajwa kesho, Ijumaa, Januari 2, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ally Mkama.

Mchungaji Malisa anashitakiwa chini ya Kifungu 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16) kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023. Anatuhumiwa kutenda kosa hilo mnamo Novemba 16, 2025, katika eneo la Miembeni, Wilaya ya Moshi.

Hati ya mashitaka inadai kuwa mshitakiwa alinuia kuhamasisha umma kushiriki katika mikusanyiko isiyo halali kwa lengo la kumtishia mtendaji mkuu wa Serikali. Inadaiwa kuwa alitoa matamko ya kumtaka Rais Samia kujiuzulu kabla ya Desemba 9, 2025, na kutishia kuanzisha maandamano makubwa nchini iwapo matakwa yake hayatatekelezwa.

Katika taarifa iliyosambaa Novemba 21, 2025, ilidaiwa kuwa Mzee Malisa alitekwa majira ya usiku nyumbani kwake maeneo ya Msamaria Majengo au Malenga, siku chache baada ya kutoa maazimio ya Kamati ya Kitaifa ya Kurejesha Haki na Amani katika Tanzania.

Unaweza kusoma zaidi hapa: Tetesi: - Inadaiwa Dkt. Godfrey Malisa ametekwa jana usiku akiwa nyumbani kwake

Zingatia: Kosa la uhaini chini ya kifungu hicho haliruhusu mshitakiwa kujibu chochote katika mahakama ya chini, na adhabu yake kisheria ni kifo iwapo mshitakiwa atapatikana na hatia.

Kesi hii inakuja wakati kukiwa na mfululizo wa mashitaka dhidi ya watu mbalimbali kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025, ambayo Serikali iliyatangaza kuwa ni haramu.
  • Msamaha wa Rais: Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwafutia mashitaka vijana walioingia kwenye maandamano hayo kwa mkumbo, akibainisha kuwa wengi hawakujua madhara ya vitendo vyao.
  • Kifungu cha 91(1): Baadhi ya washitakiwa tayari wamenufaika na kifungu hiki cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na kuachiwa huru.
Kabla ya kufikishwa mahakamani, Malisa alikuwa akionyesha misimamo mikali dhidi ya uongozi uliopo, ikiwemo:
  1. Kufungua kesi mahakamani kupinga uteuzi wa mgombea urais ndani ya CCM.
  2. Tishio la kufungua kesi ICC: Alitangaza nia ya kuwafungulia mashitaka Rais Samia na IGP Camillus Wambura katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Hadi kufikia kesho, Mchungaji Malisa atakuwa ametimiza siku 30 tangu alipowekwa kizuizini kufuatia kukamatwa kwake nyumbani kwake mwezi Novemba 2025.

Wasifu wa Mchungaji Godfrey Malisa

Mchungaji Malisa (PhD) ana historia ndefu ya ushiriki katika siasa za upinzani na CCM:
  • 2010: Aligombea Ubunge Moshi Mjini (TLP).
  • 2015: Aligombea Urais (CCK) na baadaye Uspika.
  • 2018-2020: Aligombea Ubunge kupitia TLP na NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia CCM.
  • 2025: Alifukuzwa uanachama wa CCM mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kupinga maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa kuteua mgombea urais, jambo lililotajwa na chama kama utovu wa nidhamu na kudhoofisha umoja.
Pia Soma:
Dkt. Malisa awafungulia Kesi Rais Samia na IGP Wambura Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) The Hague

Katika taarifa iliyosambaa Novemba 21, 2025, ilidaiwa kuwepo kwa taarifa mzee huyo (Mchungaji Malisa) alitekwa majira ya usiku nyumbani kwake maeneo ya Msamaria Majengo au Malenga, siku chache baada ya kutoa maazimio ya Kamati ya Kitaifa ya Kurejesha Haki na Amani katika Tanzania.

Unaweza kusoma zaidi hapa: Tetesi: - Inadaiwa Dkt. Godfrey Malisa ametekwa jana usiku akiwa nyumbani kwake
Yaa, anastahili. Hashitakiwi kwa kukosoa kwake kule, bali kwa mengine, usipotoshe kaka. Waliokosoa walikuwa wengi mbona tunao humu?
 
Back
Top Bottom