DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mchungaji Godfrey Malisa, aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro akikabiliwa na kosa la uhaini. Kesi hiyo (Namba 000028333 ya 2025) inatarajiwa kutajwa kesho, Ijumaa, Januari 2, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ally Mkama.
Mchungaji Malisa anashitakiwa chini ya Kifungu 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16) kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023. Anatuhumiwa kutenda kosa hilo mnamo Novemba 16, 2025, katika eneo la Miembeni, Wilaya ya Moshi.
Hati ya mashitaka inadai kuwa mshitakiwa alinuia kuhamasisha umma kushiriki katika mikusanyiko isiyo halali kwa lengo la kumtishia mtendaji mkuu wa Serikali. Inadaiwa kuwa alitoa matamko ya kumtaka Rais Samia kujiuzulu kabla ya Desemba 9, 2025, na kutishia kuanzisha maandamano makubwa nchini iwapo matakwa yake hayatatekelezwa.
Katika taarifa iliyosambaa Novemba 21, 2025, ilidaiwa kuwa Mzee Malisa alitekwa majira ya usiku nyumbani kwake maeneo ya Msamaria Majengo au Malenga, siku chache baada ya kutoa maazimio ya Kamati ya Kitaifa ya Kurejesha Haki na Amani katika Tanzania.
Unaweza kusoma zaidi hapa: Tetesi: - Inadaiwa Dkt. Godfrey Malisa ametekwa jana usiku akiwa nyumbani kwake
Zingatia: Kosa la uhaini chini ya kifungu hicho haliruhusu mshitakiwa kujibu chochote katika mahakama ya chini, na adhabu yake kisheria ni kifo iwapo mshitakiwa atapatikana na hatia.
Kesi hii inakuja wakati kukiwa na mfululizo wa mashitaka dhidi ya watu mbalimbali kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025, ambayo Serikali iliyatangaza kuwa ni haramu.
Dkt. Malisa awafungulia Kesi Rais Samia na IGP Wambura Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) The Hague
Katika taarifa iliyosambaa Novemba 21, 2025, ilidaiwa kuwepo kwa taarifa mzee huyo (Mchungaji Malisa) alitekwa majira ya usiku nyumbani kwake maeneo ya Msamaria Majengo au Malenga, siku chache baada ya kutoa maazimio ya Kamati ya Kitaifa ya Kurejesha Haki na Amani katika Tanzania.

- Msamaha wa Rais: Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwafutia mashitaka vijana walioingia kwenye maandamano hayo kwa mkumbo, akibainisha kuwa wengi hawakujua madhara ya vitendo vyao.
- Kifungu cha 91(1): Baadhi ya washitakiwa tayari wamenufaika na kifungu hiki cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na kuachiwa huru.
- Kufungua kesi mahakamani kupinga uteuzi wa mgombea urais ndani ya CCM.
- Tishio la kufungua kesi ICC: Alitangaza nia ya kuwafungulia mashitaka Rais Samia na IGP Camillus Wambura katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Wasifu wa Mchungaji Godfrey Malisa
Mchungaji Malisa (PhD) ana historia ndefu ya ushiriki katika siasa za upinzani na CCM:- 2010: Aligombea Ubunge Moshi Mjini (TLP).
- 2015: Aligombea Urais (CCK) na baadaye Uspika.
- 2018-2020: Aligombea Ubunge kupitia TLP na NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia CCM.
- 2025: Alifukuzwa uanachama wa CCM mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kupinga maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa kuteua mgombea urais, jambo lililotajwa na chama kama utovu wa nidhamu na kudhoofisha umoja.