Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,879
Nkire Chacha, mmiliki wa ekari tatu za shamba la bangi amesema alikuwa akipata fedha zilizomwezesha kununua mifugo anayoitumia kwenye kilimo.
Mtuhumiwa huyo mwenyeji wa Kijiji cha Sogoti wilayani Serengeti alikamatwa jana.
Hata hivyo kutokana na mazingira ya eneo imebainika kuwa kilimo hicho kimefanyika kwa muda mrefu na watu mbalimbali lakini hata viongozi wa eneo hilo hawakutoa taarifa.
Mbele ya kamati ya ulinzi na usalama inayoongozwa na mkuu wa wilaya, Nurdin Babu alisema soko lake lilikuwa hapohapo kijijini na limemsaidia kupata fedha za kukidhi mahitaji mbalimbali.
“Kwa kweli mbegu za bangi hii zilikuwa ndani ya nyumba yangu nilizitoa na kuzimwaga shambani maana hata mimi mwenyewe ninatumia, mimi sijawahi kusafirisha kwenda popote kwa kuwa wateja wanakuja nyumbani wenyewe na nimenunua ng’ombe wa kulimia,” alisema.
Babu akimkabidhi mtuhumiwa huyo kwa polisi baada ya kukamilisha ukaguzi ulioongozwa na hakimu mkazi, Felix Ginene.
“Kila siku tunahamasisha kilimo cha mazao kama pamba, mahindi na mengine lakini wananchi kwa kushirikiana na viongozi mnakwenda kinyume, lazima tuwafikishe mahakamani,” alisema Babu.
Alisema maeneo hatari kwa kilimo cha zao hilo haramu ni kata za Kebanchabancha na Machochwe lakini wataendelea kuwakamata.
“Huyu amehusika kuwavuruga wananchi kwa kuwauzia dawa za kulevya, atakuwa fundisho maana tulishawataka walime mazao yanayokubali,” alisema.
Mkuu wa polisi wilaya, Methew Mgema alisema watu watatu akiwemo mwenyekiti wa kitongoji wanashikiliwa.
“Huyu alikuwa anajua maana ndiyo wanaogawa mashamba na anaishi hapahapa. Tutawakamata viongozi kila tutakapokuta bangi kwenye maeneo yao na wao hawatoi taarifa,” alisema.
Mwenyekiti wa kitongoji, Magabe Chacha alisema hakuwa na taarifa ya kilimo hicho.