Mgirik
JF-Expert Member
- Apr 27, 2013
- 13,281
- 13,451
hapo nmekumbuka kipind nilivyokuwa mdogo tulienda kuwinda nyan, ila ktk kukimbizana na huyo nyan akawa amepanda kwenye mchikichi.
Kuna wale wakubwa waliokuwa wametuzidi umri wakatuamlisha tupande kwenye miti iliyokaribu na huo mchikichi ili kumzuia nyan asirukie kwenye mti mwingne.
Mm nikapanda mti mmoja hvi baadae wakawasha moto kwenye ule mchikichi na nyan akakurupuka akarukia kwenye mti niliyokuwa nmeupanda sasa kumbe ule mti una nyuki wana mzinga wao nyan akawakurupua wale nyuki nikashambuliwa baada ya hapo skujua kilichoelelea mpaka nilipojikuta nipo hospitali nmefungwa hogo mkono wa kushoto na bibi akiwa pemben yangu.