Aliyejifungua chumba cha mtihani "afunguka"

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
  • ASEMA ALIPONZWA NA UGUMU WA MAISHA,
  • AJUTIA NDOTO YAKE YA UDAKTARI KUYEYUKA

NDOTO za Happiness Mzalendo (18) kuwa daktari zimeingia dosari, baada ya kushindwa kumaliza kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba, baada ya kujifungua akiwa katika chumba cha kufanyia mtihani.

Happiness aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kabirizi na mkazi wa Kitogoji cha Nyakaziba Kijiji cha Kabirizi, Wilayani Muleba
anasema kuwa alianza kusikia dalili za kuumwa uchungu wakati akifanya mtihani wa pili uliokuwa somo la Hisabati.

Katika mahojiano na mwandishi wa makala haya, anasema kuwa baada ya kusikia uchungu alimweleza msimamizi wa mtihani ambaye hakujua jina lake, kwamba anaomba amtoe nje ya darasa kutokana na hali yake kuwa mbaya.

"Msimamizi alinikubalia, akanisaidia kunitoa nje, lakini, alishagundua nina tatizo gani. Nilipotoka nje tu, nguvu zikaisha, nikalala chini ya mgomba. Msimamizi akamwita mwalimu mkuu na kuweleza matatizo yaliyonikumba," anasimulia Happiness.

Anasema kuwa baada ya Mwalimu mkuu wa shule hiyo David Buberwa kufika, alionekana mama aliyekuwa na jembe akiwa ametoka shambani.

"Ikabidi wamwombe mama huyo, ili atoe msaada kwa sababu wao hawana ujuzi wa namna ya kumsaidia mama mjamzito kujifungua," anasimulia.

Anasema kuwa mama huyo ambaye pia hakumfahamu, alikubali kumsaidia na kumzalisha akiwa chini ya mgomba, ulio katika shamba la shule hiyo.
Happiness anasimulia kuwa baada ya kuzalishwa aliitwa bibi afya wa eneo hilo, anayejulikana kwa jina la Leokadia Francis kwa msaada zaidi.

Anasimulia: "Bibi afya alipofika, alinisaidia kutoa kondo la nyuma, baada ya hapo walinipeleka katika ofisi ya mwalimu, nikapewa chai na chakula na baadaye nikaambiwa nilale."

Anaeleza kuwa baada ya kupumzika, walituma ujumbe nyumbani kwao ili watume pesa kwa ajili ya kukodisha pikipiki ya kumpeleka hadi nyumbani, ambapo alisindikizwa na bibi afya huyo.

"Zililetwa pikipiki mbili; moja nikapanda mimi na nyingine akapanda bibi afya akiwa na mtoto tukaenda hadi nyumbani. Tulikaa kidogo tu na mwalimu mkuu akaja, kuna fomu za mtihani niliokuwa nikiendelea kuufanya nilikuwa sijazisaini. Nikasaini akarudi nazo," anasema.

Anasema kuwa kabla ya kupelekwa nyumbani bibi afya alimpima uzito mtoto wake huyo wa kiume ambaye hadi sasa hajapewa jina na alionekana kuwa na kilo 2.7.

Hapinnes anasema kuwa kwa sasa anaishi na bibi yake, Felista Nestory (82), kutokana na kufiwa na mama yake mzazi alipokuwa na umri wa miaka 12.

Anasema kwamba bibi yake alijua hali aliyokuwa nayo, kabla hajaanza kufanya mitihani na hata lilipotokea tukio hilo, hakushangaa wala kumgombeza, kwa sababu alijua kuwa ni mja mzito.

"Nilipogundua kuwa nimepata mimba. Sikumficha bibi yangu, nilimwambia akanizuia kuitoa. Lakini shuleni walikuwa hawajui kama nina mimba hadi nilipojifungua nikifanya mtihani," anabainisha.

Akizungumzia sababu zilizomfanya kujihusisha katika mahusiano ya kimapenzi akiwa mwanafunzi, Happiness anasema kuwa hali hiyo ilitokana na ugumu wa maisha uliopo nyumbani kwao, ambapo hata bibi yake anamtegemea yeye, ingawa bado ni mwanafunzi.

"Nilimpata huyo kijana (hakutaka kumtaja jina) nikawa na mahusiano naye ili awe akinisaidia kupata mahitaji ya nyumbani maana baba yangu hakuwahi kunisaidia chochote tangu nizaliwe, hata mahitaji ya shule alikuwa hanipi," anasema.

Anasema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri, ingawa alipojifungua nguvu zilimwishia kwa siku kadhaa na ndiyo sababu alishindwa kufanya mitihani iliyobaki.

Anasema kuwa alifanya mtihani yote ya kumaliza darasa la saba, isipokuwa ya sayansi na hisabati ambao aliuanza na kupata uchungu wakati akifanya mtihani huo.

"Kesho yake nilipata nguvu kidogo, nilikwishamwomba mwalimu aniruhusu niendelee na mtihani na akakubali, lakini nilikosa mtu wa kubaki na mtoto wangu, hivyo sikuweza kuendelea na mtihani," anasema Happiness.

Kuhusu mvulana aliyempa mimba, anasema kuwa mvulana huyo bado hajaoa, lakini kwa sasa yupo katika harakati za kazi na kwamba ana imani kuwa atarudi kuoana yake.

Anasema kuwa wakati wote alikuwa akimpa faraja, huku akimhimiza pia asome kwa bidii na kumwahidi kuwa baada ya kumaliza masomo wataoana.

Kuhusu maendeleo yake darasani, anasema kuwa hayakuwa mabaya kwani kati ya watoto 45 alikuwa hajawahi kushuka chini ya nafasi ya 18.

Kuhusu ndoto ya maisha yake ya baadaye, Happiness anasema kuwa wakati wote alikuwa akitamani kuwa daktari.
Anasema kuwa baada ya kupata mimba na kujifungua mtoto hana tena uhakika wa kutimiza lengo hilo na hafikirii tena kuendelea na masomo.

"Kusoma sasa nimekata tama, labda nikipata msaada wa fedha za mtaji kutoka kwa wasamaria wema ili niweza kufanya biashara," anasema.

Akizungumzia tukio hilo, bibi yake Happeness anasema kuwa alipokea taarifa hizo na kwamba kama zilivyomfikia, hana la kufanya na yote anamwachia Mungu.

Anasema kuwa alimlea mtoto huyo tangu alipofariki mama yake hadi sasa, bila kipato chochote, ambapo amekuwa akitegemea misaada midogo midogo kutoka kwa ndugu na jamaa.

Baba mzazi wa Happiness ambaye pia anaishi katika kitongoji hicho, anasema kuwa amesikitishwa mno na taarifa hizo za binti yake na kuwa tangu ajifungue hajafika kumwona.

Baba huyo, Justuce Mzalendo (48), alisema kuwa Happiness ndiye mtoto wake wa kwanza na kuwa alimzaa na mwanamke mwingine, tofauti na aliye naye kwa sasa.

Anasema kuwa amekuwa akimpa mahitaji yote ya nyumbani na shuleni binti huyo, lakini kauli hiyo ilipingwa na Happiness aliyesema kuwa hakuwahi kununuliwa hata sare za shule na baba yake.

"Sikujua kama ana mimba. Nilishangaa sana kuletewa taarifa kuwa amejifungua. Nilichanganyikiwa, hadi sasa akili yangu haijakaa sawa. Naogopa hata kwenda alipo nisije nikaua," anasema Mzalendo akiashiria kukasirishwa na Happiness.

Anasema kuwa kwa sasa ana mke mwingine na watoto watano na kwamba kutokana na tukio hilo, amekata tamaa ya kusomesha watoto, hasa wa kike.

source:mwananchi
 
JK: ukikubali kula sharti ukubali kuliwa pia, ugum wa maisha unaharibu watoto wetu afu ndo Rais anajibu hivyo what do you expect. Shida tupu.
 
Huo umri miaka 18 nao umechangia kuingia mambo ya ukubwani. Alitakiwa awe amemaliza form four.
 
Kwanza JK alishasema kupata mimba ni kiherehere!
Ila huyo mtoto anadanganya, alishindwa kufanya hata vibarua jamani hadi atumie mwili wake? Haya sasa, shida ndo zitakuwa mara dufu. Sasa hivi ndo amekumbuka wasamaria wema wanaweza kumpa mtaji? Akicheza anapewa mtaji wa mimba nyingine.
 
Hako kabinti kamalaya tu hamna cha kumumunya maneno napita mimi atakaye nifuata athubutu aone
 
Kweli kuna watu wana viwanda vya kuzalisha uongo!!
Kuna redio ilitangaza kwamba mwanafunzi huyu wa Muleba Bukoba(Umri miaka 14),alianza kusikia uchungu darasani,na alipomuomba msimamizi atoke nje akanyimwa.
Baada ya muda uchungu ukazidi ndio ikabidi apelekwe darasa la pembeni,mkunga akaitwa kumzalisha! 'Binti akapewa muda kidogo kupumzika,akarudi kufanya mitihani mingine iliyobaki.
Mtoto pia alipewa jina la OMR -Omri(Mfumo mpya wa majibu ya mtihani kama sijakosea).
 
:dizzy::dizzy::dizzy::dizzy::dizzy::dizzy::dizzy:

AAaaaaaiseeeeeeee....!!
 
Huyo baba mtu ni chiziiiiiiii huko alipozaa watoto watano amelishwa katerero ndio akamsahau hy mtoto wake m1
 
Huo umri miaka 18 nao umechangia kuingia mambo ya ukubwani. Alitakiwa awe amemaliza form four.

Kwa historia mkuu inaonekana kabisa mtot alilelewa na bibi bila mama (MAREHEMU) na baba ambaye ni wale ambao hawajali watoto. Lawana zote zimwendee huyo baba aliyemtelekeza hadi kusababisha mimba za utotoni na kukatisha maendeleo ya huyu binti. Poverty and adolescence pregnancies!!!
 
mmmh! miaka 18 std 7??? kwahiyo mshikaji alimtoa kwenye hilo dimbwi la umaskini na ugumu wa maisha?? au ndo alikuwa anapewa buku then anaishia kupigwa mzigo daily tena pekupeku vichakani??? tatizo cyo umaskini, tatizo ni upeo wa huyo binti na elimu ya kujitambua ndiyo aliyokosa.au mshakj alikuwa anampa practicals za biology za live c amesema alitaka kuwa daktari???
 
Back
Top Bottom