Aliyejifanya sekretari wa Kova | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyejifanya sekretari wa Kova

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]

  Kulwa Mwaibale na Musa Mateja
  Askari Polisi mmoja wa kike Faraja Jabir, anayedaiwa kujifanya ni Sekretari wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kwa kushirikiana na wenzake watatu wanatuhumiwa kumshushia kipigo ‘hevi’ kijana mmoja muuza samaki aitwaye Sunday John mkazi wa Tabata Kisiwani, jijini Dar es Salaam na kumjeruhi...
  Akiongea na Amani juzi, Sunday alidai kuwa tukio hilo lililomfanya achungulie kaburi lilitokea Machi 14, mwaka huu majira ya saa 1.00 usiku eneo la Tabata relini alipokuwa akielekea Ubungo kununua samaki wa biashara.

  [​IMG]
  Alidai kwamba, siku ya tukio akiwa nyumbani kwake mishale ya mchana alipigiwa simu kwa namba ambayo hakuifahamu lakini baadaye aliyempigia alijitambulisha kwa jina la Mama Angel.

  “Namfahamu vizuri mama huyo lakini sikuwa na uhusiano wowote naye. Nilipomuuliza alikuwa anasemaje akanijibu kuwa, ametokea kunipenda hivyo akaomba kama sitojali nimfuate kwenye saluni yake iliyopo karibu na eneo ninaloishi, mimi nikakataa.

  “Saa 8:00 mchana akanipigia tena kunisistiza tena ombi lake na kunieleza kuwa, niende kwenye Gesti moja iitwayo Out alikochukua chumba ili tukapeane raha lakini nikamkwepa kwa kumueleza kuwa, muda huo niko Mabibo.

  “Nilipomdanganya hivyo akaniambia nimsubiri huko huko kwani alikuwa akinihitaji sana, mimi nikakataa na kuendelea na kazi zangu. Ilipofika saa 10 akanipigia tena kuniuliza niliko huku akiniambia kuwa, muda huo alikuwa Muleba Bar Mabibo,”alizidi kudai kijana huyo.

  Akaendelea kuanika kuwa, ilipofika saa 12 jioni ndipo alipokwenda maeneo ya Tabata Relini kuchukua teksi ili aende Ubungo kununua samaki lakini akapigiwa tena simu na Mama Angel akimuuliza yuko wapi ambapo alimtaarifu kuwa, muda huo alikuwa akielekea Ubungo.

  “Kumbe wakati ananipigia simu alikuwa ng’ambo ya barabara akiwa na Askari Faraja, Ally ambaye ni mume wa mama Angel na mgambo aitwaye Betto, nilipowaona nikaingia haraka kwenye gari, ile nataka kufunga mlango, Ally alikuja na kunivuta nje kisha kuanza kunipiga akidai kwamba nimekuwa nakimtongoza mkewe (mama Angel),” alizidi kulalama kijana huyo.

  [​IMG]
  Akaongeza kuwa, wakati akiwa ameduwaa walitokea Faraji ambaye anadaiwa kujifanya ni Sekretari wa Kova, mama Angel na Betto kisha nao kuungana na mwenzao kumpiga kabla ya kumchukua kwa gari na kumpeleka Kituo Kidogo cha Polisi cha Tabata Kisiwani.

  “Walipiga sana na hata waliponifikisha Polisi waliendelea kunipiga kisha nikatupwa rumande bila kuandikisha maelezo yoyote. Wakati huo nilikuwa nimeshapoteza simu mbili zenye thamani ya shilingi 315,000, raba za shilingi 50,000 na pesa taslimu shilingi 400,000.

  “Nilikaa kituoni hapo damu ikinichuruzika, baadaye wakapigiwa simu Polisi wa Kituo cha Buguruni ambao walifika na Defenda kisha kunichukua. Nilipofika huko walichukua maelezo yangu, wakanipa PF3 kisha nikafungua jalada la kesi lenye namba BUG/RB/3310/2010 KUJERUHI. Nikaenda kutibiwa na kesho yake nilifungua kesi katika Kituo cha Tabata Kisiwani yenye jalada namba TBKS/RB/139/2010,”alisema Sunday.

  Amani juzi lilimpigia simu Ally anayedaiwa kuwa ni mume wa mama Angel na kusomewa tuhuma zake ambapo alikana kumpiga Sunday na kueleza kuwa, waliompiga ni raia wenye hasira kali baada ya kudhani ni kibaka.
  Mama Angel alipopigiwa simu naye alikana kuhusiana na tukio hilo huku Askari Faraja Jabir akikacha kuongea na Mwandishi Wetu kwa kudai kuwa, aliyempigia alipiga ‘wrong number’.

  Juzi (Jumanne) Mwandishi Wetu alimpigia simu Kamanda Kova na kumuuliza juu ya askari huyo aliyejipachika kuwa ni sekretari wake ambapo alisema kuwa Afande faraji si sekretari wake bali ni mtu wa masijala. Hata hivyo Kova alimuagiza msaidizi wake, ACP Chilongo kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu.
   
 2. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Haya ndiyo mateso wanayotoa polisi jamii wetu achilia mbali kazi za Kamanda Zombe!!!
   
 3. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ila kuna kitu huyu kijana hajasema
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hii ni hatari sana hasa pale Police wanampoamua kuchukua sheria mkononi
  Kwanini wampige mtu kiasi hicho wana uhakika gani kama mama Angel alikuwa anatongozwa na si yeye kutongoza ???
   
 5. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mwisho wa Dunia umekaribia.. Ndio maana matukio kama haya yanazidi.. Tumrudie MUNGU jamani..
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Yah kweli nadhani kijana kajaribu kueleza story kupata sympathy fulani.ukiona huo mtiririko sa simu ulivyokuwa unakwenda mhhh.
  lakini nadhani hatua walizochukua hawa jama sio sahihi.
   
 7. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sometimez polise huwa wanafanya mambo ya ajabu sana
   
 8. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Hapo umenena...huwezi kula kichapo cha kiasi hicho bila sababu.......!!
   
Loading...