WomanOfSubstance
Platinum Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 975
Kwa kweli Gaijin sijakutana na legislation hii ila huenda ipo Ila as a rule of practice mahakamani kuna miiko yake ikiwemo huu utaratibu wa kuvua kofia, kusimama pale hakimu au jaji anapoingia au kutoka na pia kukaa kimya bila kupiga kelele ya aina yoyote ile karibu na eneo la mahakama. Kuna hakimu aliwahi kumfunga mtu kwa masaa machache kwa kupiga honi eneo la mahakama, kuna mtu aliwahi kuhukumiwa faini kwa kosa la kuonyesha dharau mahakamani ( contempt of court)..na hata hili la baraghashia utaona ni along same lines - contempt of court ila adhabu was manifestly excessive.yuko huru kwa sababu mahakama kuu iliona kuwa ulikuwa si uamuzi sahihi lakini wengine ndio wanaona mahakama kuu imeamua tu vile kwa sababu ya shinikizo la waaislam
labda wos anaweza kutusaidia ..............jee kuna sheria ya maandishi inayokataza kofia mahakamani?
Kwani Acid, tunapaswa kuwaogopa watu tuonapo kuna upotoshaji?WOS, umejitakia mwenyewe... mwenzio huyo ana agenda yake na wala si haki ya huyo aliyefungwa, yeye kaja hapa na politikal agenda lile jukwaa lao limedoda siku hizi
Tatizo linakuja katika usahihi wa hakimu kumtaka ndugu Sururu avue baraghashia
Mkuu hivi unaakili wewe ama? Nimesema nitaka rufaa wa baragashia arudi jela hiyo orodha umeitoa Madrasa
Bernard James
Jaji Kiongozi Fakihi Jundu jana aliliambia Mananchi Jumapili mahakama iliamuru kuchiliwa kwa mzee Sururu baada ya kuridhika hapakuwa na sababu za kutosha kisheria kutoa hukumu hiyo.
Muda mfupi baada ya kusomwa hukumu hiyo maofisa wangu walinipa taarifa na kuchukua hatua ya kuitisha faili la kesi. Jana majira ya saa kumi jioni ofisa wa mahakama alikuwepo gerezani kuhakikisha Bwana Sururu anaachiwa huru na kuungana na familia yake, alisema jaji kiongozi.
Aliongeza: Wakati Bakwata (Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania) wanahoji uhalali wa hukumu hiyo tayari tulikwishachukua hatuai. Hatukusubiri kusukumwa na mtu yeyote. Sisi tulihisi tatizo katika hukumu hiyo na kuchukua hatua mara moja.
Chanzo: Wavuti ya Mwananchi