Aliyefariki dunia akiuliza swali Bandari azikwa

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Aliyefariki dunia akiuliza swali Bandari azikwa


na Hellen Ngoromera


amka2.gif

ALIYEKUWA Mfanyakazi wa Idara ya Uhandisi Ujenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ofisi ya Bandari Dar es Salaam, Shaaban Mlawa, ambaye alifariki dunia ghafla juzi muda mfupi baada ya kumuuliza swali Mkurugenzi wa TPA, Ephraim Mgawe, wakati wa mkutano wake na wafanyakazi hao, amezikwa jana kijijini kwake Kisarawe, mkoani Pwani.
Mazishi hayo ambayo yalionekana kugubikwa na simanzi kutokana na mazingira ya kifo hicho, yalihudhuriwa na wafanyakazi mbalimbali wa bandari wakiwamo viongozi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari Tanzania (DOWUTA), Abdallah Kibunda, aliiambia Tanzania Daima kuwa kabla ya shughuli za mazishi kufanyika wilayani Kisarawe, shughuli nyingi za msiba huo zilifanyika nyumbani kwa marehemu eneo Vingunguti, Dar es Salaam.
Habari za kufariki dunia kwa Mlawa zilitangazwa juzi na Mwenyekiti wa Dowuta Tawi la Bandari, Athumani Mkangara, hali iliyowashangaza wengi hasa waliokuwa naye katika mkutano wa wafanyakazi wa TPA na Mkurugenzi wao, Mgawe, ambapo kabla ya kufikwa na mauti Mlawa alianguka na kuzirai, kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Regency.
Katika swali lake kwa mkurugenzi wa PTA, marehemu Mlawa alihoji wafanyakazi kupatiwa mapumziko wakati wa siku za Jumamozi na Jumapili na sababu ya Mgawe kutoishirikisha Dowuta kuhusu ubinafsishwaji wa vitengo vya bandari ambavyo ni maegesho ya magari, nafaka na kitengo kipya cha magari kinachomilikiwa na Bandari.
Tukio la marehemu Mlawa kuanguka na kuzirai lilitokea majira ya saa 11 jioni wakati mkutano huo ukiendelea chini ya ulinzi mkali wa askari wa bandari waliotapakaa kila kona.
“Kwanza nafurahi sana kukuona ndugu mkurugenzi, kwani tangu uingie madarakani sijawahi kukuona, hivyo hii ni fursa pekee kwangu, pili tunaomba Jumamosi na Jumapili tupumzike au kulipwa posho za ziada,” alipomaliza kuzungumza mambo hayo Mlawa alianguka na kuzirai, kisha kubebwa kwa msaada wa watu, ndipo baadaye ilitangazwa na mwenyekiti wa Dowuta tawi la bandari kuwa amefariki dunia.”

Source:Tanzania Daima

Jamani hii mimi haijanikaa vizuri kichwani mwenye data zaidi azimwage hapa kwani hii habari sijaielewa vizuri.
 
Siku yake ilifika.
Its just a natural Death, japo kibongo mazingira hayo ya kifo yataacha utata wa mwaka!
 
Siku yake ilifika.
Its just a natural Death, japo kibongo mazingira hayo ya kifo yataacha utata wa mwaka!

...utata huanzia hapo. Bora uchunguzi wa kidaktari uwe wazi kuwa alikufa kwa shinikizo la damu, au katika hayo...
 
Labda aliuliza swali kwa jazba sana (jazba na shinikizo la damu ni mtu na binamu yake)
 
Aliomba kupumzika siku 2 kwa juma, kumbe bila kujua alikuwa anaomba kupumzika milele. Na amepumzika kweli! RIP Mlawa, umemaliza kazi yako hapa duniani.

Vifo vya namna hii pengine ni matokeo ya watu kutofanya check-up za mara kwa mara juu ya afya zao. Wanasubiri mpaka mwili uanze kuwa-bip kwamba una matatizo ndipo wanapogutuka na kwenda kwa daktari. Kumbe usikute mtu alikuwa anaumwa siku nyingi bila kujua kwamba anaumwa mpaka anaanguka na kufariki. Hadharani inaonekana amefariki ghafla lakini kumbe alikuwa na matatizo siku nyingi na pengine hata yeye hakujua. Poleni wanafamilia.
 
Back
Top Bottom