Hapo nilivyoelewa mimi
Huyo mama inaonesha kabla ya hapo alikua amemshika mtoto mikononi sasa mtoto akaanza kusinzia. Mama akambeba kumpeleka kwenye chumba cha huyo mtoto ili alale.
Kinachofanyika sasa hapo mama anajaribu kuweka mkono wake mwilini mwa huyo mtoto kwa staili ya kumbeneleza ili mtoto aendelee kufeel kua yupo na maa yake kwasababu bado usingizi haujachanganya
Kama ilivyokawaida ya watoto wengi pindi akiwekwa kitandani huwezi ukakurupuka kuondoka ukidhani kua amelala,
Kwaiyo picha ya kwanza inanesha huyo mama akijaribu kumbembeleza
Picha ya pili inaonesha huyo mama anamchungulia mtoto kuhakikisha kua mtoto amelala fofofo ( na ndio maana ametoa macho)
Picha ya tatu inaonesha huyo mama akijiandaa kusepa kwa staili ya kunyata baada ya kuona huyo mtoto amelala
Picha ya nne na tano inaonesha huyo mama ameshuka kitandani ila mkono wake mmoja bado umemgusa huyo mtoto ili kumpa tumaini kua mama yake bado yupo endapo kama ajalala fofofo
Picha ya sita inaonesha huyo mama ameutoa mkono uliobakia mwilini mwa huyo mtoto kwa umakini mkubwa ili asije kumuamsha
Picha ya saba huyo mama anamsikilizia huyo mtoto kama kalala kweli au atahisi upweke baada ya mkono wa mama yake kuondolewa mwilini mwake
Picha ya tisa inaoneha huyo mama amebaini kua mtoto amelala hivyo anaanza kufanya jitihada za kusepa kimya kimya asije kumuamsha mtoto kwa kelele endapo ataondoka kwa vurugu
Picha ya mwisho inaonesha mtoto kastukia mchezo ameamka baada ya kutohisi kumbatio kutoka kwa mama yake.......soon ataanza kulia na mama yake atarudi tena kumbembeleza