Aliyeeiba simu yangu ameonekana CCTV

kagosha

Member
Aug 3, 2010
98
125
Jamani naomba msaada nini nifanye, nimemwona aliyeniibia simu yangu kwenye kamera live. Sasa ofisi inaendelea kufuatilia information kupitia huyo dada aliyekuja naye.

Je, sasa hatua gani nichukue kwa kuwa tayari tumepata namba ya simu ya huyo aliyekuja naye. Tukio zima limeonekana kwenye kamera tangu wanaingia reception mpaka wakati huyo jamaa anaichukua na kuitia mfukoni baada ya kuizima.
 
Loi Mollel

Member
Apr 11, 2014
6
0
Kama una namba ya simu ya jamaa nadhani tayari unaweza kumkamata kupigia service provider, nenda polisi wanipa kubali cha uchunguzi.
 
Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,482
2,000
Utasumbuka Bure,utapoteza muda wako mwingi huko, Zichange kannunue ingine
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,699
2,000
Sasa kama cctv imemuona anaiba unataka ni cha zaidi? Peleka ushaidi polisi wafanye kazi yao au kama una namba ya simu mwambie kiroho safi arudishe tu kabla mambo hayajafika mbali halafu unamtumia clip hyo aliyokuwa anaiba thru whatsup!! Halafu usikute simu aliyoiba sio gallaxy wala nini.
 
Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,318
2,000
Wewe tafuta taarifa zake halafu mfuatilie kitaeleweka kama CCTV zinamwonyesha vizuri usikate tamaa
 
kagosha

Member
Aug 3, 2010
98
125
Wewe tafuta taarifa zake halafu mfuatilie kitaeleweka kama CCTV zinamwonyesha vizuri usikate tamaa

Nyati na wadau wengine wote mliochangia thread hii, nawashukuru sana. Nimeipata simu yangu ingawa kulifanyika jaribio la kuiharibu (futa kumbukumbu zote) kwa hivyo imepoteza ubora wake na data pia, lakini nitaenda samsung service center wa in reinstall bila shaka itakuwa sawa,
Inauma sana lakini japo nimeokoa laki sita lakini nimepoteza data na contacts nyingi sana. katika yote namshukuru tu Mungu na kumsamehe aliyetenda hilo.
 
Hongera sana kwa kupata simu yako. Je jamaa kachukuliwa hatua ama ameachwa akaibe kwingine?
 
kagosha

Member
Aug 3, 2010
98
125
mimi nimesamehe na kila kitu kimeishia hapo. Mungu atamsamehe pia. najaribu sasa kugather data na information zangu kitu kinachoniuma zaidi lakini sina la kufanya
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom