Aliyechoma Qur'an afungwa jela miezi 24

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Aliyechoma Qur'an afungwa jela miezi 24 Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 21:21

Salma Said, Zanzibar

RAMADHANI Handa Tuma (28) Mkazi wa Mombasa wilaya ya Magharibi Unguja, aliyekuwa akituhumiwa kwa kosa la kuchoma moto msahafu wa dini ya kiislamu amehukumiwa kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miezi 24.

Lakini pia mshtakiwa huyo ametakiwa kulipa faini ya Sh 200,000.

Adhabu hizo zilitolewa na hakimu Khamis Ali Simai wa Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, baada ya kumtia hatiani.

Akifafanua adhabu hizo hakimu Khamis alisema shitaka la kwanza la kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani atalipa faini ya Sh200,000 na endapo atashindwa atatumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miezi sita.

Kuhusu shitaka la kukashifu dini, mahakama hiyo imempa adhabu ya kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miezi 18, na kufahamisha kuwa adhabu zote hizo zitakwenda sambamba, hivyo atalazimika kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda huo wa miezi 18.

Alisema pamoja na hilo pia mtuhumiwa huyo ambaye alipatikana na makosa hayo alipewa adhabu mbili hizo ili iwe fundisho kwa wengine kutofanya makosa kama hayo ambapo alisema haki ya kukata rufaa mahakama ya mkoa ipo wazi, iwapo kuna upande ambao haukuridhika na hukumu hiyo.

Kwa upande wake, upande wa mashtaka unaosimamia kesi hiyo uliongozwa na Raya Issa Mselem, ulitoa taarifa ya kwa mahakama hiyo ya kukata rufaa kwa kutoridhika na adhabu iliyotolewa dhidi ya shitaka la pili kukashifu dini.

Taarifa hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 358 (1) cha sheria za mwenendo wa jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar .

Katika hukumu yake iliyodumu kwa takriban saa moja,hakimu Khamis alisema kuwa upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha makosa hayo dhidi ya mtuhumiwa huyo pasi na kuacha chembe ya shaka ya maana. Na kumuona ni mkosaji kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, mshtakiwa huyo aliomba apunguziwe adhabu kwa madai kwamba ana familia inayomtegemea akiwemo mke na mtoto pamoja kusumbuliwa na maradhi ya tumbo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu sasa.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, Ramadhan Handa Tuma alifanya kitendo Novemba 16, mwaka jana hadharani kwa makusudi na bila ya halali alichoma moto kitabu kitakatifu yaani msahafu pamoja na juzuu za dini ya kiislamu kitendo ambacho kingeweza kuleta uvunjifu wa amani kwa jamii ya kiislamu.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments




0 #3 2pak.hitem all 2011-03-02 07:52 Wangemwa mwacha !!!!, maana nilimfuatilia tangu mwanzo alikuwa na njaa,halafu hayupo kwenye uislam wala ukristo achilia mbali upagani kwa ufupi ni jahli. pia ushauri wangu huko chuo cha mafunzo awekwa karibu na wanazuoni huenda akapata hidaya.
Quote









0 #2 mbuyi 2011-03-02 07:17 Habari haiku-ballance, imeelezwa zaidi kwa kupendelea kuegemea muelekeo na mapenzi ya mtoataarifa, haikuelezwa sababu za huyo mliyemfunga kwa nini alifanya hivyo na wala alikuwa anajitetea vipi. habari imeaacha maswali mengi badala ya mjibu.
Quote









0 #1 DESRE 2011-03-02 02:44 utaumwa kweli m[NENO BAYA] weee,,ningekuwa karibu wakti unafanya hivyo na mie ningefungwa maana lazma ningekupa mafaulu,,heshim u imani za watu nahis ni [NENO BAYA] anepimwa akili
 
Back
Top Bottom