Aliyebuni mfumo wa namba za Magari alikosea

Aliyebuni mfumo wa namba za Magari alikosea

Namba D imekaa sana kiasi kwamba imemeza namba A,B na C..

Namba DA ilianza August 2014 na leo march 2017ndio tupo DK..

Kwa spidi hii namba D inaweza fika 2030..

L M N P Q R S T U V W X Y Z.... Hapo parefu kuliko A had K
Haitafika 2030 labda wangetenganisha na Trailer ziwe na namba zake kama motorcycle
 
T AAA ilitoja 2004 ka sihakosea miaka 13 imepita ndio kwanza D... So had zisogee herufi nne ifike namba K itakua 2040 huko
Umeona mkuu? Na hapo hata nusu ya alphabet utakuwa bado hujafika. Sasa hiyo Z tunaikuta lini? Tutakuwa nado tupo tu? Hizo ni namba za wajukuu zetu!! Kwa hiyo mfumo huu uko sawa kabisa na hongera zake aliyebuni mfumo huo?
 
miaka 20 ijayo haifiki tutakua tumesha maliza.
Haiwezekani. Toka mfumo huu uanze 2002 hadi leo ni miaka 15 na bado tupo herufi ya 4 ambayo ni D. Sasa hadi tufike herufi ya 26, Z siyo leo wala kesho. Bado sana.
 
Unapo Fanya uchambuzi wa mfumo gani utumike (Identification Code) lazima uhakikishe vitu hivi unavizingati.

1. Mfumo wako unataka uwe na muda gani bila namba kujirudia.

2. Mfumo wako lazima ubebe taarifa , mfano nikisoma namba ya gari nipate taarifa Fulani za gari, sisi hapa utakuta rangi ndio zinatumika.

na mengine mengi.

nikianza na hill kwanza , nimeshtuka sana kuona hadi sasa tumesha anza kutumia namba za DKX XXX INA maana miaka michache ijayo itabidi tunaanze upya maana namba zitakua zote zimesha tumika.

Je aliyependekeza mfumo wa namba za magari alikua anafikiria jambo hili?
Umeongea jambo jema sana kiongozi, ijapo utapingwa na wengi ila ilikuwa muhimu sana kujua hiyo gari imesajiliwa wapi sio gari zote zianze na T
Mfano ingekuwa T(DA 360 BBE)au T (MO 360 BBE) au T (KI 360 BBE)
Hapo ingekuwa inatambulika kuwa gari hii ya Dar, moro au Kilimanjaro
 
Mfano rahisi sana fanya hivi T xxx AAA =999
T xxx AAB = 999 .Ukimaliza herufi zote utakua na magari mangapi ndio uje tena kukosoa.
 
Haziwezi kwisha karne hii, kama kusajiri wanaanzia moja inaamaa kila herufi inatumika kwa magari 999
Kwa mfana T......AA(A-Z) magari 999 mara 26=25,974 hiyo ni kwa T..AAA peke yake. So ukichanganua kwa herufi zote T..ABA mpaka TZZZ sijui itakuwa mwaka gani
 
daima hazitAisha mkuu. ikitoka iyo DKX itakuja XKD so zitakua zinageuka haziwezi jirudia ama kuisha
 
Ukifanya calculations kwa zile tarakimu tatu ukichanyanya na herufi 3 unapata maelfu ya namba tofauti.
MFANO: T 123
ABC
Hizi ukizkcomand kwenye sytem ziwe random utapata namba nyingi mno ndugu
Ni kama vocha, tarakimu ziko kumi na kitu tu ila kila siku tunatumia milions za vocha na still hamna tatizo.
mkuu, usiangalie wingi wa namba, angalia wingi wa magari. kila mwaka tunamaliza herufi moja. Mwakani tutakua HZZ XXX
 
Umeongea jambo jema sana kiongozi, ijapo utapingwa na wengi ila ilikuwa muhimu sana kujua hiyo gari imesajiliwa wapi sio gari zote zianze na T
Mfano ingekuwa T(DA 360 BBE)au T (MO 360 BBE) au T (KI 360 BBE)
Hapo ingekuwa inatambulika kuwa gari hii ya Dar, moro au Kilimanjaro
Hilo la region ID lingekuwa la muhimu sana. Japo kusema kweli hizi namba zitachukua karibia karne moja kuisha, lakini registration ingehusisha region codes. Sishauri kuweka majina kama MO-Morogoro, DA-Dar es salaam etc, mimi nadhani wangeweka codes kwa regions, mf. xxT101xxx. Tuna mikoa haifiki 40, hivyo hizo x mbili za mwanzo zinakuwa regional codes, then zingine kama kawaida. 11 T 101 DKA. Hiyo 11 iwe regional code kama Dar.

Hata hivyo, hii system yaweza kufika 2080's huko ambapo wengi tutakuwa tumekata umeme, itakuwa kizazi kingine kabisa.
 
mkuu, usiangalie wingi wa namba, angalia wingi wa magari. kila mwaka tunamaliza herufi moja. Mwakani tutakua HZZ XXX
Kiongozi, jiulize huu mfumo umeanza kutumika mwaka gani, hadi sasa tupo herufi ya nne tu. Kama tangu 2002 zimetumika A-D tu na hiyo D ipo DK..., jaribu kufanya hesabu ndogo tu..
 
mkuu ivi unajua kwa mwaka magari mangapi yanaingia? karne unaijua. kabla hujazeeka utashuhudia namba TZZ XXX.
 
mkuu, usiangalie wingi wa namba, angalia wingi wa magari. kila mwaka tunamaliza herufi moja. Mwakani tutakua HZZ XXX
Mkuu, Ndio kwanza tuko DK saiv...

Na hii n tokea 2014.. ndio kwanza ilianza tumika, mpk ifike mwisho n leo? Mpk siku inasoma ZZZ... n miaka hata 200 na zaid ijayo.. na ikifika mwsho wanauwezo wa kuanza na

T 1111 AAA.. au T 111 AAAA.. Hazitofika mwsho kamwe
 
Kiongozi, jiulize huu mfumo umeanza kutumika mwaka gani, hadi sasa tupo herufi ya nne tu. Kama tangu 2002 zimetumika A-D tu na hiyo D ipo DK..., jaribu kufanya hesabu ndogo tu..
Hizi namba zilitakiwa hata tuishi miaka mil 2 zisiishe kwa sababu utunzaji wa kumbukumbu utasumbua sana. nashangaa watu wanaona mbali 2100. Mtazamo kama huo ndio unaturudisha nyuma.

Mambo mengi tumeyafanya tukadhani ni makubwa kumbe baada ya miaka 20 yameonekana hayafai kwa sababu ya mtazamo mbaya.

Mkapa aliipanua Moro road ikaonekana bomba , kabla hata hajamaliza ikaonekqna haifai tena.

IPO njia ya kutengeneza mfumo huu usiwe na mwisho, pengine kwa kuongeza herufi au namba moja tuu.
 
Hakuna mfumo uliokamilika asilimia 100 na huu mfumo ukiisha si utakuja mfumo mwingine! Kubadilisha kunaongeza mapato wa Serikali. Umekosoa ndiyo lakini angalau ungependekeza mfumo ungekuwaje!
 
Back
Top Bottom