Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,778
Heri ya sikukuu wapenzi,
Huyu jirani yangu na mume wake wana watoto wawili, wakiume na wakike, bidada alitafuta sana nafasi ya kwenda kuongeza elimu, amepata chuo Mwanza, mume kwa furaha alimpeleka mke wake mpaka Mwanza, walitafuta nyumba nzima na baba alilipa pango la mwaka mzima, kwasabu watoto na house girl walikwenda Mwanza kukaa na mama.
Kama zawadi ya kuanza shule shost alinunuliwa Mercedes new model ya kuendea shule, kifupi mume wake mpunga umetulia. Akiwa shule, mashost zake Dar, wakina sie tena, tukimuona shemeji na vidada si tunapeleka ujumbe kwa mkewe. Mashallah shost kaumbika, toto la pwani lililotulia, si akapata kijana wa Kisukuma wa kumtoa stress za yale aliyokuwa anayasikia yakiendelea Dar.
Bwana shemeji alikuwa anakwenda Mwanza kila baada ya miezi miwili na akifika hukaa wiki mbili. Kuna wakati akiwa mwanza akapata kidudu mtu wa kumpa story za mkewe, shemeji hasira, alimpiga sana shost, shost alikataa kabisa. Baada ya hapo bwana shemeji aliamua kuwa rafiki, akamwambia shost mimi ni mume wako wa kanisani, tuliahidiana kwa shida na raha, sasa kama kweli mke wangu ulinicheat niambie, shost alilainika kama butter si amwage ukweli wake. Shemeji yangu aliumia sana.
Shost alimaliza shule, akarudi Dar, sasa sikuhizi shemeji ni anaishi yale maisha ya 'I don't care' yaani anarudi saa anayotaka, anaweza kukaa siku tatu hajarudi nyumbani, shost akiuliza anajibiwa wewe si una mambwana zako.
Je ilikuwa sahihi kwa shost kukubali kuwa alikuwa na buzz?