Alitaka kujiua baada ya kutoswa..

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,513
11,276
MSEMO wa mapenzi yaua nusura utimie kwa mrembo Sophia Amir, baada ya kuamua kubwia sumu, kisa kulikosa penzi la mtoto wa mkuu wa mkoa (jina kapuni), chanzo kinaarifu. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Sophia ambaye ni mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam, alidaiwa kumeza idadi kubwa ya vidonge aina ya Flagyl kwa lengo la kujiua.

Chanzo cha habari kinaeleza kwamba, msichana huyo alipatwa na wazimu wa mahaba baada ya mtoto huyo wa mkuu wa mkoa kwa jina moja anaitwa Thomas kumtamkia wazi kuwa hamtaki tena kimapenzi.“Walikuwa wapenzi wa siku nyingi, lakini yule kaka akamwambia Sophia kuwa amemwacha, kwa uchungu ndiyo akaamua kunywa hivyo vidonge, watu wakamuwahi, kalazwa Mwananyamala hospitali,” chanzo kilifunguka.

Baada ya taarifa hiyo, mwandishi wetu alikwenda hospitalini ambako alimkuta mrembo huyo akipatiwa matibabu na bila ajizi alikiri kutaka kujitoa roho.“Nampenda sana, aliniahidi mambo mengi, leo nikimpigia simu hapokei wakati mwingine ananitukana, nikaona ni bora nijiue,” alisema Sophia huku akibubujikwa machozi.Kama ilivyo ada habari lazima itende haki, mwandishi wetu alimpompigia simu Thomas alijibu kwa kifupi: “Usinifuatefuate,” kisha akakata.

My take: Duh..!
 
Pamoja na maumivu ya kucheleweshewa muda na kutotimiziwa ahadi, bado alitakiwa kujitambua na kujua kuwa uhai alionao una thamani kuliko chochote. Lazima ajue kuwa yeye ni yeye na ataishi kama yeye, hakuna anayeishi kwa ajili ya mwingine.

Kutojitambua hupelekea mtu aone hana lolote analoweza kufanya bila uwepo wa mwingine, kitu ambacho si kweli. Mapenzi yapo na yataendelea kuwepo, asipokupenda huyu atakupenda yule, huna sababu ya kujiua kwa ajili ya kukataliwa. Umia siku moja, songa mbele miaka elfu moja!
 
... na iwe hivyo Ndugu Furaha ushindi (happiness win)
 
Alikua anatishia tu ili jamaa arudishe majeshi aisee!
km aliamua kweli angekunywa sumu ya panya,hizo flagil alijua hawezi kufa haraka na watamuwahi na kupona!!

Tatizo ni mapnz ya kitoto alitakiwa kujua sababu za kuachwa je jamaa aliamua tu kumtema au yy ndio amesababisha au laa!
Alafu kujiua sio solution ya yy kupendwa tena bali atamuacha mwenzie alika raha dunian,angekubali matokeo na kuvumilia badae angepata mwingine!!
 
Kwenye Bold naona umeamua kumpatia njia rahisi na yenye uhakika, lol...
 
Pamoja na maumivu ya kucheleweshewa muda na kutotimiziwa ahadi, bado alitakiwa kujitambua na kujua kuwa uhai alionao una thamani kuliko chochote. Lazima ajue kuwa yeye ni yeye na ataishi kama yeye, hakuna anayeishi kwa ajili ya mwingine.

Kutojitambua hupelekea mtu aone hana lolote analoweza kufanya bila uwepo wa mwingine, kitu ambacho si kweli. Mapenzi yapo na yataendelea kuwepo, asipokupenda huyu atakupenda yule, huna sababu ya kujiua kwa ajili ya kukataliwa. Umia siku moja, songa mbele miaka elfu moja!

Nitaufanyia kazi huu ushauri dadaaa.
 
LOOSER !!!!!!!!!!!!!!

Sidhani alikuwa anampenda huyo Katoma. Ametaka kujiuwa kwa sababu Katoma kamvunjia ndoto zake ambazo alipanga kutokana na ahadi alizo pewa.

Kama kweli angekuwa anampenda, angejitahidi kumfanyia yale ambayo yame muuzi Katoma. Rudi kwa mungu wako. Fanya toba. Anza upya kulitafuta penzi. Safari hii sio kwa manufaa yako bali kwa wote. GOOD LUCK.:shock:
 
Kupenda hadi kutaka kutoa uhai wake?

Namuomba Mungu isije ikanitokea, Maisha matamu sana i see.
 
Back
Top Bottom