Aliponiona si akanikumbuka

Aliponiona si akanikumbuka

Galadudu

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
2,304
Reaction score
780
Jaman yule dada ambaye nilimlipia nauli kwenye daladala jumapili iliyopita halafu akanipeleka kwa mume wake akaenda kunirudishia, jana tumeonana tena.

Kama inavyofahamika kwa sisi watanzania wengi ukiwa ofisini ikafika mida ya lunch utaenda kula lakini lazima ushushie vibia viwili, sasa nina ka chupa kangu mezani mara nikashangaa mhudumu naongezwa bia nyingine wakati hata sijaagiza.

Mhudumu akaniambia, umeagiziwa na yule mdada, nilipogeuka kuangalia, lahaula" nikakutana na tabasamu kali la yule mrembo, nikampungia tu mkono, huku moyoni nikiamini kwamba hapa sio bure, kukutanishwa nae tena huyu kiumbe.

Na yule jamaa yake aliyenipa ile sh elfu 5 alikuwepo, kwa kuonesha uungwana ili nizidi kumchanganya nikaamua kuinuka kwenda kumsalimia, nilipofika kwanza kabisa jamaa hakuonekana kutambua uwepo wangu pale (dharau hizo) baada ya salamu sasa kilichofuata.

Mdada akanitambulisha kwa yule mshamba, unamkumbuka huyu mkaka jamaa akaniangalia juu mpaka chini halafu akatikisa kichwa kwa dharau kuwa hanifahamu, mrembo akasema huyu si ndo alinilipia nauli siku ile kwenye daladala, nikaja nae ukampa sh elfu 5.

Jamaa likauliza kwa kashfa sana, kwa hiyo na leo kaja nimpe elfu 5 nyingine.

Sio siri nilikasirika vibaya sana hadi nikajiuliza sijui nimfumue ngumi kalikali za kushtukiza huku nikichombeza kwa vipepsi vya hapa na pale, lakini kabla sijatimiza azma yangu hiyo, jamaa akainuka kwenda toilet, shati lake likajivuta kidogo, nikaiona bastola imetulia kiunoni, nikajua kumbe ndo maana ana dharau sana, hapo nikawa mpole.

Jamaa lilipoondoka demu akaniambia, huyu nae huwa ana mawivu ya kijinga sana, akatoa simu yake fasta akanipa nikawa nishajua cha kufanya muda huo, nikaweka namba zangu, akasema tutawasiliana, nikamalizia bia yangu nikaondoka, lakini bado najiuliza sana kwa upuuzi wa yule mshamba hivi nikimpigia demu wake nitakuwa na makosa kweli, namba ndo tayari nimempa nasubiri tu kitakachotokea nitaleta mrejesho hapa.
 
Kama inavyofahamika kwa sisi watanzania wengi ukiwa oficn ikafika mida ya lunch utaenda kula lakin lazima ushushie vibia viwili, sasa nna ka chupa kangu mezani mara nikashangaa muhudumu naongezwa bia nyingine wakati hata cjaagiza.

mh mlioko maofisini ni kweli haya ndio yanayofanyika?
 
Nimefurahi sana kupata sehemu ya pili, usichelewe mkuu kuja na sehemu ya tatu ya huyu lijamaa
 
Jaman yule dada ambae nilimlipia nauli kwny daladala jumapili iliyopita halafu akanipeleka kwa mume wake akaenda kunirudishia....jana tumeonana tena.

Kama inavyofahamika kwa sisi watanzania wengi ukiwa oficn ikafika mida ya lunch utaenda kula lakin lazima ushushie vibia viwili, sasa nna ka chupa kangu mezani mara nikashangaa muhudumu naongezwa bia nyingine wakati hata cjaagiza.

Muhudumu akaniambia:- umeagiziwa na yule mdada....nilipogeuka kuangalia, lahaula" nikakutana na tabasamu kali la yule mrembo, nikampungia tu mkono, huku moyoni nikiamini kwamba hapa sio bure, kukutanishwa nae tena huyu kiumbe.

Na yule jamaa yake aliyenipa ile sh elfu 5 alikuwepo, kwa kuonesha uungwana ili nizidi kumchanganya nikaamua kuinuka kwenda kumsalimia, nilipofika...kwanza kabisa jamaa hakuonekana kutambua uwepo wangu pale (dharau hizo) baada ya salamu sasa kilichofuata.

Mdada akanitambulisha kwa yule mshamba....unamkumbuka huyu mkaka.....jamaa akaniangalia juu mpaka chini halafu akatikisa kichwa kwa dharau kuwa hanifahamu, mrembo akasema huyu si ndo alinilipia nauli cku ile kwny daladala, nikaja nae ukampa sh elfu 5..... jamaa likauliza kwa kashfa sana, kwa hiyo na leo kaja nimpe elfu 5 nyingine......!!!!

Sio siri nilikasirika vibaya sana hadi nikajiuliza cjui nimfumue ngumi kalikali za kushtukiza huku nikichombeza kwa vipepsi vya hapa na pale, lakin kabla cjatimiza azma yangu hiyo, jamaa akainuka kwenda toilet, shati lake likajivuta kidogo
..heeee...!!! nikaiona bastola imetulia kiunoni, nikajua kumbe ndo maana ana dharau sana, hapo nikawa mpole

Jamaa lilipoondoka demu akaniambia:- huyu nae huwa ana mawivu ya kijinga sn, akatoa simu yake fasta akanipa nikawa nishajua cha kufanya muda huo, nikaweka namba zangu, akasema tutawasiliana, nikamalizia bia yangu nikaondoka, lakin bado najiuliza sana kwa upuuzi wa yule mshamba hivi nikimpigia demu wake nitakuwa na makosa kweli, namba ndo tayar nimempa nasubir tu kitakachotokea nitaleta mrejesho hapa.

Uliza mwenzako wa juzi kati aliyepakuliwa umate mate kunako jicho chongo :mini kabang) atakupa feedback ya kilicho jili baada ya kuwa kwenye himaya ya dingi swayo. Na ndo mana waliwa ti.go hamtakaa kuisha kwani kila siku mnaongezeka. ziepukeni tamaa zisije waponza kwani buku 5 na bia moko itakufanya uishie kuchujiwa nafaka/ wazungu weupe kwa kuchaniwa marinda yako mazuri (mbaya zaidi wakiifanya shughuli hiyo "dunga dunga au mateja ".
N.B:Kwa hisani ya wazee wa kubambia mzigo kama huyu hapa chini kwenye picha.
 
hahahahahaaa, nasubiri part 3. Kahadithi katamu.
 
siku hizi limekuwa jukwaa la vichekesho
 
Mkuu mim Part 1 nilikosa, Part 2 ndio hii hapa, Part 3 nishaiona itakua mbaya usikubali kuigiza
 
Mkuu mim Part 1 nilikosa, Part 2 ndio hii hapa, Part 3 nishaiona itakua mbaya usikubali kuigiza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom