Alinusurika kifo kwa kudra ya Mwenyezi Mungu

fisitembo

Senior Member
Jun 19, 2020
123
273
Hili ni tukio la kweli kabisa lililotekea mwaka 1988, kuna Jamaa mmoja alitokea Tanzania kwenda Msumbiji kwa kupitia border mmoja inaitwa Congress au mkenda.kipindi hicho haikuwa njia rasmi sababu kulikuwa hakuna ofisi za uhamiaji kwa pande zote mbili yaani TZ na MOZ.

Jamaa alikuwa anaenda kuuza viatu Vya mitumba, utaratibu ilikuwa unatafuta mwenyeji atakayekusafirisha kilomita 120 kwa baskeli unalala kwake ili alfajili muuanze safari kabla jua halijapambazuka.

Huyu Jamaa anasema walipolala usiku na mwenyeji wake akawa anamsimulia habari zake za huko anakokwenda kwenye mji mmoja wa Lichinga na akamuonyesho Dora 20 za mojamoja pamoja na Mzigo wake wa viatu.

Kulipopambazuka asubuhi wakaanza safari, hii njia imepita katikati ya mbuga.Nazani waliosafiri na baskeli wanajua sio njia nzima utapanda, kwenye mchanga, mlima lazami utasukuma.

Jamaa anasema muhanga ilipofika zamu yake ya kusukuma, mwenyeji wake akawa anamfuta kwa nyuma,gafla akamchoma na kisu kwenye mbavu, Jamaa akamuuliza ndugu yangu unataka kuniuwa? Akamwambie tena unipe na zile Dora ulizonionyesha Jana,basi jamaa akampa hera.

Baada ya kupewa hera mwenyeji wake akamwambia akimbilie ndani ya msitu akafie ndani asipofanya hivyo atammalizia,Basi huyu Jamaa akachukua baskeli yake na Mizigo ya huyu Mtanzania na kuanza kuludi walikotoka akimuacha mwenzake bila msaada.Jamaa anasema kuangalia lile jeraha akaona utumbo unaanza kutoka na huku damu zinavuja, akavua shati na kujifunga kuzuia utumbo usitoke

Akaona kuliko kufia msituni heri aludi barabarani labda anaweza kupata msaada,baada ya mda wakaja fisi nazani kutokana na halufu ya damu wakawa kama wanataka kumkamata, anasema alikata tawi la mti akawa anafanya kuwafukuza,akawa anajisemea moyoni si mda mrefu atakuwa chakula cha hawa fisi, huku nguvu zikimwishia.

Baada ya mda wakatokeza mwanamke na mwanaume wamepakizana kwenye baskeli,ikabidi Jamaa awaombe msaada na kuwasimulia kisa kizima, ikabidi mgonjwa apandishwe kwenye baskeli wawe wanamsukuma maana kupanda wote hawawezi wako watatu wamsaidie wakafike vijiji Vya kalibu,maana kutoka walipo kuipata hospitali pana kilomita 70.

Baada ya Kama nusu saa wakasikia Muungurumo was gali,kumbe alikuwa padiri anaenda kusoma Missa,ikabidi wamsimamishe wamuombe msaada,alichowajibu aliwaambia waendelee kwenda taratibu wamsubilie akamilize misa,anapoludi atawakuta njiani.Kumbuka anakokwenda padiri ni kama kilomita 50 na njia ni kama zile za porini wanakokwenda watu kuchukua mkaa au mbao yaaani ni msitu.

Wakakubali kwa shingo upande wakaendelea na safari ya baskeli huku wanasikuma,anasema baada ya nusu saa wakaona padiri analudi tena,anasema anakokwenda haoni njia,na ni njia anayopita kila jmapili kwenda kusoma misa. Basi ikabidi Jamaa apakiwe kwenye gari kuletwa hospitali ya mkoa.

Huyu Jamaa anatusimuli kipindi hicho yuko wodini kama watanzania wenzake alikuwa mwenyeji wa Dar es Salam, Mungu alimsaidia akapona na aliyemchoma kisu alikamatwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom