Maserati
JF-Expert Member
- Jun 15, 2014
- 11,602
- 20,101
Niende moja kwa moja katika mada iliyonifanya nishike simu yangu na kuyaandika haya baada ya kusikia habari hizi kutoka kwa rafiki yangu ambapo imenilazimu kuandika haya.
Huyu ni mshikaji wangu kitambo tumuite Masumbuko ila ila sio jina lake sahihi.Huwa namuona anapouza na kununu bidhaa kama simu kwa lengo la kuuza na kujipatia kipato.Siku moja Masu kapigiwa simu kama kuna mtu ana simu yake SAMSUNG s3, 4 na huawei Y300. Basi Masu akatazama list ya watu waliompigia simu wakiulizia simu kama ambazo ameambiwa. Akachukua simu zile na kwenda kuziuza, jioni akarudisha ela kwa mwenye mzigo na cha juu akakichukua yeye.
Lakini kuna simu haikununulika S3. Hivyo Masu akanunua kwa ela yake. Lakini baada ya siku 2 akatokea mtu na kuomba auziwe simu ile na masu akampa, dili lkaisha. Masu Kapigiwa simu na mshikaji mwingine ambae akataka simu na baada ya muda masu akaenda na simu ambayo alikuwa nayo kwa wakati huo ambayo ilkuwa Iphone 4s. Alipofika akaambiwa ingia ndani tucheki simu na kukupa ela yako, masu akaingia.
Wakaicheki basi wakamwambia haya twende nimeridhika nayo, twende sehemu tukachukue hela. Masu akakubali, likawashwa gari safari ikaanza, mpaka Msimbazi polisi akashushwa na kupelekwa ndani, akavuliwa mkanda, viatu, saa, simu na vitu vingine. Baada ya hapo akaambiwa "kumbe kweli wewe ndo mwizi mwizi unaeuza simu za uhalifu eeeh" basi akapigwa makofi kadhaa kisha akapelekwa sero na kuambiwa asubiri achukuliwe maelezo, huko akamkuta mteja wake wa simu ya S3. Saa tisa akaitwa na kuchukuliwa maelezo.
Baada ya maelezo na kusema alikoitoa simu ile ambayo ni S3 akatoa namba za mtu aliyeinunua simu ile. Akapigiwa simu kwa kumtumia Masumbuko lakini hakupatikana na masumbuko alikaa ndani siku mbili, bahati nzuri siku ya tatu alipatikana na kupatikana kwa yule mtu aliyemuuzia simu Masu ndio pona yake. Hapo tukapokea simu kutoka kwa mchizi Masu akitaka tumsaidie kuwaambia ndugu zake wakamtoe." Tulienda Msimbazi polisi centre na kufatilia taratibu za kumtoa.
Tulipofanikiwa ndio akatuambia kumbe ile simu imeporwa katika tukio la uhalifu ambapo aliyeibiwa alikuwa na wenzake na mtu mmoja alichomwa kisu cha bega mara 2 na mkononi mara 1. Na pia kuliibiwa pesa na vitu vingine ikiwemo laptop.
Mpaka sasa jamaa aliyemuuzia Masu simu hapatikani kwa simu na jamaa hajatoka mpaka sasa yupo kituoni.
Onyo:usipende kununua simu au laptop kwa mtu yaani mkononi better uende dukani au uwe na taarifa za kujiridhisha maana hatuwezi zuia kabisa kununua simu mkononi mwa mtu (used ).
Mwenye kuelewa aelewe na apate fundisho. Na asiyetaka kusikia asubiri.