Ndugu, Si tu kuwa hukuelewa maudhui ya Uzi huu, Kiswahili pia inaonekana ni tatizo kubwa kwako kukiandika, Pole.
Chukuwa somo la bure.
KIUANDISHI na KIMANTIKI;
Maneno yako:"Kwenye maelezo yako unahisi umeongelea ulivyotendwa ama unatafuta cheap sympathy tu!!!"
Sentesi yako hii haieleweki kama unaniuliza ama unanieleza.
-Mapangilio wako wa maneno ni dhaifu katika kujenga hoja.
-Uchaguzi wa maneno si-sahihi, pamoja na matumizi ya alama za kiuandishi ndio hoooovyo kabisa.
*Matumizi ya alama za mshangao (!!) katika hali yoyote hapo juu hazikustahili kuwepo.
Kukusaidia tu;
Kwa kuwa hujaelewa maudhui kusudiwa yaliyobebwa na uzi huu (Hoja kuu) hali inayopelekea nilazimike kukupa darasa la ziada tena lisilohusiana kabisa na uzi mkuu,
Siku nyingine unaweza kupunguza usumbufu usiokuwa wa lazima kwa kufanya yafuatayoi;
MOJA:Kaa pembeni ili kutoa nafasi kwa wenye hoja (Walioelewa mada) wajadili kwa nafasi bila kero kama ufanyavyo sasa.
MBILI:Jifunze namna ya kujenga hoja na kuandika kwa usahihi kutoka kwa wengine.
**Kumbuka si kila uzi unaoupitia au kuuona unalazimika kuchangia mawazo, Mengine hasa yaliyokupita uelewa ni busara kuyaacha yajadiliwe na wenye kuelewa.