Alinishauri mwenyewe ila sasa ananitangaza vibaya kwa watu

Fanya kazi yako kisomi zaidi.Fuata sheria na uwe tofauti na boda wote.Jitahidi wekeza upate boda yako mwenyewe halafu itumie hiyo kuandikia proposal upate mkopo benki ili upate boda nyingine.Ajiri kijana kadiri siku zinavyoenda fungua kampuni ya boda boda ajiri vijana wengi zaidi.Hakikisha unaaminika na watu wenye maduka makubwa au watoa huduma uwe unatoa deliveries.Weka matangazo ya kampuni yako na namba za simu watu wakupigie popote wanapohitaji usafiri na utoe huduma kwa uaminifu.
Baadaye huyo bwana atakuheshimu.
 
Utofauti uliopo kati ya bodaboda msomi na asiye msomi ni kwamba msomi yuko kwenye foleni ya bomba linalotoa maji while bodaboda asiyesoma kapanga foleni na madumu huku bomba lishakatwa na vibaka kwa mbele
 
Ushauri nzuri ila maisha yangekuwa simple like that basi maskini wangekoma Tanzania.
 
Piga kazi Mkuu huyo jamaa anateseka ndani kwa ndani baada ya kuona hauwezi kumuomba tena hela ndogo ndogo.
 
Akikutangaza kinapungua nini kwenye maisha yako??
 
Endelea kukomaa tu .Hakuna mtu atakuletea sembe la Bure ukiwa umekaa tu .
 
Mpakize kwenye boda yako mpeleke umbali wa km 20 ambako usafiri hakuna, kisha mpeane makavu live...

Halafu sepa mwache huko atajijua
 
Wewe mtoa mada ni kilaza sana, elimu yako haijakusaidia maana unashindwa ku-handle kesi ndogo kama hiyo. Sasa tukikuajiri na kukuambia utoe ushauri ili kampuni iingize faida si utatuharishia kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…