Alinisaliti, nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alinisaliti, nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sipo, May 22, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukisalitiwa ufanyeje?
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  M'mwage..life is too short to live miserably
   
  Last edited by a moderator: May 22, 2009
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kaka una uhakika gani kama walikutana tu kwa maongezi au kuna kitu walifanya?
  Halafu nimuda mrefu umepita tangu amefanya hilo tukio ina maana humpenzi ndo maana mpaka leo kinakuuma wewe una kinyonho, mapenzi yanasamehe na kusahau, ameshajaribu kukuambia hana mawasiliano naye tena kwa nini huamini?
  Kummwaga siyo tatizo haya ni mambo yanayoweza kuzungumzwa kwa mapana zaidi maana mnataka kuelekea hatua muhimu na kuyatatua.
  Yaani umenishangaza sana najua mapenzi yanauma lakini siyo kukaa na kinyongo muda wote huo utakufa kwa kihoro.
  Halafu tangu muda huo alivyokwa mbia kwa nini usimmwage tangu hapo kama kweli ulikuwa na principles zako umesubiri mmmekaa mnakaribua kuoana leo ndo roho imezidi kukuuma sana? huoni kama ukimuacha utakuwa na yeye umemuumiza na umempotezea muda.
  Mwanaume unatakiwa uwe na msimamo siyo unakufa na tai shingoni.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mambo ya u -girlfriend na u Boyfriend shuleni na vyuoni sio guarantee ya kuja kuoana baadae.

  ...hakujua ipo siku ataishi nawe vile vile.

  ...hakuwa na uhakika wa msimamo wako mpaka ulipomuonyesha ile reaction.

  ...'mavi ya kale hayanuki!' ...kwani wewe na yule ex -Girlfriend wako mmeyafanya mangapi bana?
   
 5. stanluva

  stanluva Senior Member

  #5
  May 22, 2009
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nashndwa kukuelewa ndugu yangu, kwani kulikuwa kuna kitu gani hadi mkafikia kuulizana hivyo? Inaonyesha mlikuwa watoto kiasi kwamba unamuuliza mpenzi wako ni muda wa mwisho kukutana X-BF wake! Na inaonyesha kweli anakupenda maana alikuueleza ukweli na ndo ukakuleta machungu, sasa vip ulitaka akudanganye kuwa ilikuwa miaka 5 iliyopita? Ushauri wangu kama ulianzisha wewe mwenyewe ulilikologa inakupasa ulinywe bint hana kosa alikueleza ukweli!
  Jikaze baba kumbuka wanaume tumeumbwa mate....... kuhangaika!
   
 6. A

  AbbyBonge Member

  #6
  May 22, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdogo wangu! sifa ya mwanamume ni kufanya maamuzi yake mwenyewe.

  Wewe inaonyesha sio mvumilivu maana bado unakumbuka kitu ambacho mlisha sameheana hapo nyuma, inaonyesha hata mkiingia ndoani siku mkitofautiana kidogo utamkumbusha hilo. Naamini litamuuma sana akijua huwa unasamehe kinafiki.

  Kumbuka wewe pekee ndo unajua umeumia kiasi gani na mkasa huo. Sasa jiulize unaweza kusahau na uanze maisha mapya? maana wanawake hubadilika sana, kumbuka hizo ni foolish age.

  Nakushauri umuoe huyo binti maana kila mtu hapa duniani amewahi kufanya ujinga na kama hukumbuki basi ujue ndio unafanya ujinga sasa ...ACHAAA

  Kumbuka hii leo ni ngumu sana kuanza kutafuta mtu mpya na muanze mahusiano ya pekupeku maana watu wapima kwa macho siku hizi.

  Chukua mzigo wako jikaze, vumilia huo ulikua ni utoto tu na ndio maana alisema ukweli otherwise angekuficha na angeendeleza libeneke mpaka kesho.
   
 7. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  sio utoto ndio ulipelekea kuulizana maswali hayo ila ni mapenzi, unajua unapompenda mtu unatamani kumjua zaidi ili ujiridhishe kuwa upo sehemu ya umakini. Kama hangenidanganya ingekuwa heri kwani nani hasiyejua mapenzi kwa kiasi kikubwa ni uongo. Ila nashukuru kwa ushauri wako maridhawa
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nadhani nimekuwa mvumilivu kuliko unavyofikiri, na pia usema age ya 25 to 26 ni foolish age kwangu sio kweli. Halafu kumbuka huyu binti wakati tunakutana kimapenzi tulikuwa tunatumia condoms. Lakini kuna siku alikuja akaniambia anahisi ana mimba kwakuwa haoni siku zake. Mimi nikamuuliza uko serious au unatania, akaniambia niko serious mpaka alienda hospitali kupima. Ebu pima hapo na baada ya kama wiki mbili ndio akaja kunieleza kama nilivyoandika kwenye post ya kwanza. Jamani hivi hii kweli ni sahihi? Ila nashukuru kwa ushauri wako
   
 9. A

  AbbyBonge Member

  #9
  May 22, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati niko mdogo nilishudia masela/mateja wakienda kum-baka mdada mgonjwa wa akili, lakini kabla ya kuanza kum-baka walimuogesha kwa sabuni nyingi tu then wakamuanlika juani kiasi ili akauke maji na baadaye wakajisevia.

  Na wewe mchukue mchumba wako makilshe chini muongee vizuri mkumbushe hiyo mikasa yote na uone kama ataahidi kubadilika umuoe.

  Nimegundua unampenda huyo dada, sasa tumia muda wako kumjenga ili umpende zaidi.

  Hao wanawake wote wenye tabia nzuri wameandaliwa, japo wapo waliozaliwa na vipaji vyao/tabia zao nzuri
   
 10. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ndugu Sipo,
  Kama hili linapokusumbua moyoni sasa, huko uendako litakuwa chungu zaidi, hasa utakapokuja kubaini kuwa anaendelea nae au atakapojipatia mwingine. Kumbuka mlamba asali halambi mara moja. Mimi nadhani hapo ulipofikia kuja kuomba ushauri katika uwanja huu, basi upo mbali. Chukua hatua zitakazokufanya ufurahie mapenzi kwa muda ulionao. Ila yakupasa pia kujua kuwa kumwacha huyo haikufanyi kumpata ambae atakuwa mzuri au mwaminifu kuliko huyo! Viumbe hawa (wanaume na wanawake) hawaaminiki.
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  HIVO HIVO BABAAKE!
  tudem dem twa chuo hutu ni tumalaya sana
   
 12. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nafahamu fika kuwa kumwacha huyu na kumtafuta mwingine ndio solution. Na ndio maana nimekuja hapa ukumbini mwetu. Ila ninachotaka nikufikia uamuzi ulio sahihi na husiokuwa na mazonge na hii ni pamoja na kupata ushauri wenu wadau. Nashukuru sana kwa ushauri Nono. Ila ingekuwa ni wewe hungefanyaje?
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni kweli nampenda lakini naogopa kumpenda mtu ambaye amenisaliti na kuniumiza kwa sababu anaweza kuwa kikwazo maishani mwangu. Unajua mapenzi ni furaha na sio karaha. Sasa kama mtu alishindwa kuniheshimu hapo hata kama tunapendana vipi si itkuwa kudanganyana. Halafu mimi nafikiri watu wengi wanatembea na MA-EX wao lakini sio mpaka the present one ajue kuwa umetoka nje. IT PAINS JAMANI! ACHA! nashukuru kwa ushauri once again
   
 14. M

  MAO Senior Member

  #14
  May 22, 2009
  Joined: Dec 23, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  utoto ulikuwa unakusumbua, na kama huna uhakika na hiyo mimba kama ni ya kwako, muache!!! Kumbuka kwa sasa hujafungwa na kitu chochote.
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  halua haina kipolo!!
  kwa nini upashe kipolo wakati vya kupikwa vipo?

  PIGA CHINI!
   
 16. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani sijui kwanini hapa utoto unawekwa mbele, mimi namini mtu wa age ya 25 na 26 yuko very matured enough katika kufanya maamuzi sahihi. Na mimi nakiju nilichokuwa nakifanya kwa asilimia nyingi tu. By the way thanks for your advise
   
 17. idea

  idea Senior Member

  #17
  May 22, 2009
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 120
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  poleeeeeeee weeeeeeee
  "penzi kiti cha basi ukishashuka anapanda mwingine" by mr paul.
  Itakuuma zaidi ukimbwaga halafu siku nyingine ukaona ana mtu mwingine.
  By the way yeye anakupenda kihivyo kama wewe? If yes then zifanyie kazi tofauti zenu halafu endeleeni na hatua nyingine. It takes a lot of time and energy to invest in a relationship so kaka fikria mara mbili mbili kuanzisha mahusiano mapya.

  Ni hayo tu-wishing you the best of luck
   
 18. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dar, pole sana. Uwe na msimamo wewe, wa kiume. Mtu anaye ku cheat kirahisi hivyo bado wa mlilia? Afanye vyote asamehewe sio tabia hizo. Anaonekana ni bingwa wa kudanganya huyo. Una hakika ilikuwa kwa huyo tu? SMS nzuri huku anakutenda? Tabia haina dawa. Uzuri wa mtu tabia bwana. Kwani hamna walio wazuru zaidi yake kwa tabia na urembo? Mnacommitment gani?

  Hebu pata uhakika zaidi wa tabia zake ktk mahusiano. Chunguza kwa kina uaminifu wake. Lakini ana dalili mbovu.

  Mademu wengi wa vyuo huwa na mabuzi kama ifuatavyo: Nadhani unajua

  1. Kipanga wake -Huyu ni anayempa mapenzi kwa sababu ya uwezo wa shule/akili za kidume.
  2. Handsome - Huyu ni anayempenda kwa dhati kimapenzi kwa sababu ya maumbile yake, shughuli ktk game, unadhifu na sura nzuri n.k. Anaweza kuolewa na mtu huyu. Yuko tayari kutoka naye na kuonyesha wenziwe/ndugu zake.
  3. BUZI/ATM- Hawa wanaweza kuwa zaidi ya mmoja. Mara nyingi ni waajiriwa. Hata waume za watu. Ndio wafadhili kipesa na vitu; TV, friji, simu, gari, bajaji n.k.
  4. Mwalimu mnoko- mambo ya maksi na uhakika wa kufaulu.
  5. Wa zamani kabla hajajoin chuo au wa mtaani kwao/alikotoka- Huyu ni kwa sababu ya historia tu. Anaweza kuachwa any time.

  Au nimekosea jamani? Haya kazi kwako. Ila cha muhimu devise ways and mechanism kumpata ambaye japo afadhali ukicheche wake.
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  unasex nae na condom cku zote. leo anakuja kukwambia ana mimba na alishakutana na huyo ex wake hapo kati ukiwa haupo, kuna cku condom ilipasuka?....kuna walakini hapo bro!
   
 20. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Mnh!! Mara ya kwanza alikuambia kwamba alikutana nae ingawaje mlishakuwa tayari ni wapenzi!!! Kwa jinsi ilivyo, si ajabu ni yeye ambae alianzisha hayo maongezi kuhusu ex-friends!!! For sure, lipo jambo ambalo lilimdatisha ambalo alitamani sana ulijue, otherwise asingekuambia kwamba alikutana nae wakati tayari mlishakuwa wapenzi!! Vuta kumbukumbu unapoenda kuangalia matokeo (especially when u are just a kid, may be o-level or primary) halafu ukakuta umefaulu!! baada ya kuona matokeo hayo, utatamani upae angani ili ukamwambie kwamba umefaulu!! Umedata na matokeo mazuri!!!Hofu yangu ni kwamba, shemeji yetu alidatishwa ile mbaya kiasi kwamba ilikuwa ngumu kuhifadhi siri hii!!! Mhemuko ukiwa mkubwa, akili ya kibinadamu hugoma kufanya kazi!! Pole sana, am afraid ataendelea kukusaliti kwa sasa atakuwa makini na kauli zake kv ulikuwa aggressive alipokupa info!!
   
Loading...