Alinichukua kichawi, aliporopoka nikasitisha ndoa

Alinichukua kichawi, aliporopoka nikasitisha ndoa

chakufia nini

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2015
Posts
692
Reaction score
456
Ilikuwa miaka ya 90 mwanzoni nikiwa std 7, nilikuwa na girlfriend ambaye tulikuwa tukisoma darasa moja. (tulikuwa kwa wakati huo hatujawahi kusex japokuwa tulikuwa tukiandikiana barua na mapenzi flani hivi ya utoto).

Siku moja usiku nilipanda kitandani kulala mida ya saa nne hivi usiku, ghafla nilihisi kuishiwa nguvu, sikuweza kusogeza kiungo chochote japokuwa macho yalikuwa yakiona kila kitu kinachoendelea. niliona wanamme 3 na mwanamke mmoja waliokuwa wamefunga kanga tu.

waliniangalia huku wakitabasamu, wakaninyanyua kimo cha mbuzi nikawa naelea hewani wakawa wananisukuma kama vile manesi wasukumavyo kitanda cha mgonjwa,waliondoka na mimi mpaka nyumbani kwao yule girlfriend wangu.

yeye binafsi sikumuona ila mazingira ya kwao niliyatambua fika na hata mama yake (alikuwa mzee kidogo) niliweza kumuona na kumtambua.

niliwaona wakiongea na kuniangalia huku wakitabasamu japokuwa sikuweza kutambua walichokuwa wakiongea. baada ya muda mfupi tu wakaanza kunisukuma na kunirudisha nyumbani, walinifikisha kitandani kwangu, ghafla nilihisi maumivu makali kwenye paja na upande wa kushoto wa mishipa iliyo karibu na jicho, kama nimeumwa na nge vile kwani maumivu ya nge nilikuwa nayajua.

nilikurupuka huku nikipiga yowe la maana, wazazi na ndugu wengine waliamka na kuja chumbani kwangu, tulihangaika sana kutafuta mdudu aliyening'ata kwa takribani masaa 2 bila mafanikio. nikapewa huduma ya kwanza na kuwekewa dawa za kufyonza sumu ya nge.

kesho yake asubuhi sikuweza kwenda shule, niliwambia wanafunzi wezangu (majirani) wakaniombee ruhusa kwani naumwa. lakini walipotoka shule saa 8 walikuja na stori mpya.

kuwa hata yule demu wangu nae kang'atwa na nge mkononi. (japokuwa yeye aliweza kwenda shule siku hiyo). kwa hiyo kila mtu aka conclude kuwa pengine tulikuwa tumelala vichakani tukifanya mapenzi na nge walituumia huku.

maisha yakaendelea tukamaliza shule, kila mtu akashika 50 zake kuendelea na sekondari. nilihama sengerema. uhusiano ukawa umekufa baada ya std 7.

baada ya kama miaka 3, nikakutana tena na huyo demu wangu (safari hii nikiwa mtu mzima kidogo, nikamuomba mchezo kwani hatukuwa kuduu wakati wa primary),

For sure, i was her first cut, mi ndiyo nilimbikiri, na sijui kwanini hiyo ndiyo siku pekee niliyoduu nae. cjawahi tena mpaka leo hii. maisha yalisonga, tukamaliza vyuo tukapata kazi. nikafikiria kuoa.

nilimkumbuka nikahisi atafaa kuwa mama wa watoto, nikaamua kumtafuta ili nione kama naweza kupanga nae maisha. tukaanzaisha mawasiliano.

kabla sijamtamkia nia yangu nikawa bado napima kuona hali yake kwa wakati huo ikoje(katika maongezi),nione kama anaelekea katika dhamira yangu kabla sijamtamkia kuwa nataka kumchukua moja kwa moja.

siku moja nilimtembelea kwao mida ya jioni. akawa ananisindikiza wakati naondoka. tulipofika njiani akaniambia kwanini nisilale tu kwani siku hiyo alikuwapo peke yake nyumbani kwani mama yake hakuwepo.

nilimkatalia na kumwambia itakuwa siyo heshima kwake kulaza mwanamme nyumbani, akanijibu akiwa amekasirika kidogo na kunikazia macho "kwani unaogopa nini?unadhani itakuwa mara yako ya kwanza kulala kwetu? hivi unadhani yule nge alikuumia wapi?"

sikuamini masikio yangu, kwani ilikuwa imepita miaka na mimi nishasahau kuhusu ile stori ya nge. niliunganisha dots nika conclude kuwa yale niliyokuwa nikiyaona kabla ya kuumwa na yule mdudu ambaye hakupatikana yalikuwa ya kweli kabisa na siyo ndoto.

hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kuonana mimi na yeye, nilikata mguu, nikajiondokea zangu. kama asingenitamkia maneno yale basi leo hii ningekuwa nimeoa mchawi.
 
Huwa nakasirika nikiona bongo muv wanakopi kwa wahindi na wanaigeria visa vyao vya stori wakati kuna stori za kweli nyingi tu.hii nayo ikiwekwa kwenye muv nafikiri itauza hasa .
 
Saa nyingine hawa jamaa wanapojichukulia sheria mkononi kwa wachawi wanakuwa wako sahihi
 
Huku tukutafutie mwenza ama??wakuague??
 
Mshukuru sana Mungu!,huyo demu asingelitamka hivyo usingelijua km huyo demu ni mchawi na leo hii yangelikuwa mengine,km mkiwa wadogo mling'atwa na nge basi ipo siku mngeng'atwa na Koboko tena kwenye Kauboo na mwenzio kwenye........
 
Be strong and of a good courage, fear not, nor be afraid of them: for the Lord thy God, he it is that doth go with thee; he will not fail thee, nor forsake thee.
 
Unamaanisha hasemi ukweli? Hii ni true story kabisa,wanawake wa kanda ya ziwa ni noma,ni gusa unate.


Yawezekana ijawa imetokea, i had a man of that kind alikuwa player balaa kumbe kwa sababu ya hayo makitu anawafanyiaga wadada akafanya jambo flan hivi baya lakunibore nlipomwambia kanijibu " mimi ni mwanaume mi tunavyoagana leo hutakaa unione nakutafuta but nakuapia utanitafuta wew kwa udi na uvumba labda kama sio mimi, maisha yangu hamna mwanamke ananitisha nakuwa nayeyote nimtakaye na siachwi na mwanamke mimi, tafuta wenzio 3 nmewazalisha nakuwaacha lakini wananinyenywkea mbaya hapa umefika" sikuamini aisee nlipiga duaa moja matata sana nakuishi kwa imani ya allaah nlishangaa uchawi haujafanya chochote na aliiahia kunitafuta yeye misamaha kibao nkamwambia tafuta mchawi mwenzako alinyong'onyea sana nakuona aibu akasepa
 
yawezekana ijawa imetokea, i had a man of that kind alikuwa player balaa kumbe kwa sababu ya hayo makitu anawafanyiaga wadada akafanya jambo flan hivi baya lakunibore nlipomwambia kanijibu " mimi ni mwanaume mi tunavyoagana leo hutakaa unione nakutafuta but nakuapia utanitafuta wew kwa udi na uvumba labda kama sio mimi, maisha yangu hamna mwanamke ananitisha nakuwa nayeyote nimtakaye na siachwi na mwanamke mimi, tafuta wenzio 3 nmewazalisha nakuwaacha lakini wananinyenywkea mbaya hapa umefika" sikuamini aisee nlipiga duaa moja matata sana nakuishi kwa imani ya allaah nlishangaa uchawi haujafanya chochote na aliiahia kunitafuta yeye misamaha kibao nkamwambia tafuta mchawi mwenzako alinyong'onyea sana nakuona aibu akasepa

mkuu,hii kitu imetokea sana,kuna wakati hapo usukumani kuna vijana watatu walimchukua msichana mmoja na kulala nae kwa usiku mmoja sehemu tofauti.kila mmoja akadai alikuwa nae usiku huo.baadae ikawa ajabu.but stori ikaja baadae kuwa kuna wawili kati yao usiku ule walilala na fisi,na mmoja ndo alikuwa na yule dada
 
Kwa hiyo ulikuwa ushambikiri long siku hiyo ukizani umembikiri alikuwa kashindiria maji ya ndimu ya kutosha.
 
Back
Top Bottom