kitu ambacho wachawi huwa wananifurahisha ni kwamba wakiongea huwa wanakaza sana macho. kwenye uchawi wao huwa wanaamini kuwa ukimkazia macho mtu unamchukua nguvu anakubaliana na kila utakachosema, ni kama kumchukua mateka. nilishakutana sana na wanadamu wa kukazia macho mahali ambapo hata si pa kukazia macho, lakini naona kwangu wanadunda.
nilishawahi kuwa na demu ambaye ukilala naye chumba hiki, kinachoendelea chumba cha tano anakijua na anakusimulia aina ya mtu huyo alivyo. siku moja nimelala naye kwenye hotel moja mbali kabisa sisi wote wageni mji ule, tukasikia mayowe ya watu chumba kama cha tatu hotelini, yowe la mwanamke, yeye akaniambia hapo kwenye kelele kuna mwanaume anafanya kitu kibaya sana (ilikuwa shinyanga mjini) akaeleza everything kinachoendelea kati ya mwanaume na mwanamke pale chumbani, tukatoka nje tukaona watu wamekusanyika, kusikia story ni kwamba kuna mwanaume mmoja alikuwa amechukua malaya, na alikuwa anataka kumchinja pale chumbani kama kafara fulani sijui achukue kichwa na alikuwa ametoa kisu kumbe madawa aliyomnywesha mwanamke hayajamlevya vya kutosha mwanamke akapata nguvu akapiga kelele na kupambana jamaa akalala mbele. mwanzoni nilikuwa namuogopa, nikajua hatutakuja kuachana, akanitishia kuwa nikimuacha sitakaa salama.
kilichotokea nilimpiga chini, akatishia uchawi hadi akachoka, na hakuna hata baya moja limenipata. alikuja kukiri baadaye akawa anasema mimi silogeki...nikasema poa.