Aliniacha akafuata ndoa, sasa anataka turudiane kwa kuibia

Aliniacha akafuata ndoa, sasa anataka turudiane kwa kuibia

Ninamfahamu binti ambae aliishi kwenye ndoa miaka saba bila mtoto, alianza kumtafuta kwa hali na mali, kwakweli dada alikigawa, from right to the left. Ilikuwa miaka ya 90 wakati ule UKIMWI ilikuwa ticket ya kifo. Alipata vyote viwili kwa mpigo, UKIMWI na mimba na aliaga dunia mara baada ya kujifungua.
 
Hana lolote pengine mumewe hampi show za kibabe,amekumbuka show zako!,songa mbele mkuu atakunyagisha miwaya ujutie maisha yako yote.
 
Braza achana nae mpotezee,watu ambao wanakuja kwa design hio hua wanaleta matatizo makubwa sana katika maisha yako.ww songa mbele na maisha yako.
 
Usidhubutu kufanya anachotaka yy alikumiza vya kutosha hivyo huna haja yakurud nyuma, songa mbele, mkataa pema pa baya panamwita acha ale dhambi aliyokutendea, mabint kuweni na msimamo ukipendwa upendeke wanaume ndio wale wale ona yanawasibu huyu Dada sasa
 
Ni binti niliyempenda kwa dhati, nae alionyesha kunipenda kwa takribani miaka miwili na tulishatambulishana kwenye familia zetu na nilikuwa nasubiria amalize chuo tufunge ndoa. Binafsi nilimtangulia kumaliza chuo na nilikuwa nipo kazini tayari.

Mabadiliko ya tabia zake kama kutojibu SMS, kutopokea simu, kunizuia nisifike hostel kwao, kutokuja kwangu, siku akipokea simu anajibu nyodo, nikajua kuna shida. Kwa msaada wa rafiki zake nikabaini amepata mshkaji flani ambaye kwa wakati ule nikiri alinizidi kipato sana.

Nakumbuka jmosi niliyotumiwa SMS na rafiki yake akinieleza kuwa shemeji yao mpya amewaambia wajiandae anakuja kuwachukua hosteli kuwapeleka club flani town maarufu sana, nikasema acha nibadili namba nimpigie mpenzi wangu kuwa nataka kuonana nae, alipokea kwa shangwe ila alipojua ni mimi akajibu yupo busy na studies akakata simu.

Night ilipofika nikazama club niliyoambiwa watakuwepo, nikapanda kwa juu kuona wanaoingia baada ya kujihakikishia ndani hakuwemo. Kama SAA sita flani hivi nikaona washikaji wawili wakiingia huku wameongozana na mabinti watano, yap walikuwa wenyewe, mpenzi wangu kashikwa mkono na huyo ambaye nilibaini ndo mchizi mpya, na yule mchizi mwingine alikuwa yupo yupo tu akikagua kati ya wale wengine akomae na yupi.

Mida ikaenda, nimechill tu nacheki picha linavyokwenda, Mara apigwe romance, Mara ashikwe tako, kenyewe kanachekacheka tu. Washikaji wakawa wanapiga sana kilevi, mabinti waliagiza grand, reds na MAJI.

Punde, mabinti wote wakanyanyuka wakaenda toilet, wakiwa wanatoka nikawablock, nikamwambia nimeona kila kitu alichokuwa anafanya na yule jamaa pale chini. Akanijibu, bora umejionea mwenyewe, ukome kufuatilia usivyovimudu. Akaondoka huku wenzake wakimfuata kwa nyuma akiwemo yule alieniambia kuwa watakuwa pale.

Niliondoka club, na kuamua kuendelea na maisha yangu, ndugu na jamaa walipohoji kuhusu ndoa yangu, niliwajibu wavute tu subira. Miaka mitatu baadae, nakutana na yule binti kwenye mgahawa mmoja wakati wa lunch, kumbe aliolewa na yule jamaa, aliniomba msamaha kwa Yale aliyonitendea, nami nikamjibu sina kinyongo nae.

Aliponishangaza ni pale aliposema anajutia maamuzi yake ya kukubali kuolewa na yule jamaa, alinieleza mengi ambayo siwezi kuyamwaga hapa, lakini kiukweli nilimuhurumia sana. Nikamuuliza vipi kuhusu watoto, akaanza kulia, nilimbembeleza, akasema, naomba nizae na wewe, mume wangu anashida ya uzazi, tumeshahangika sana bila mafanikio. Naomba tufanye kwa siri hadi nipate mimba please.

Kauli ile ilinikumbusha nyakati za furaha na zile za karaha nilizopitia na yeye.
Nilimuonea huruma mwanaume mwenzangu kwasababu nilijua nyakati za kuonja shubiri ya huyu mwanamke zimefika.

Nilimjibu acha nikafikirie ombi lako ili kumuondoa njiani. Sijamjibu kitu wiki sasa, ingawaje hachoki kunitafuta.

Malaika wako alikuepusha na mabalaa...keep going don't look back[emoji120]
 
Wala jamaa hana shida ya uzazi ni mbinu tu ya kutaka umbinue, wenye shida hawasimuliagi hivyo haraka wewe, huo ni mtego anauweka na pengine ukute ana watoto

Huo uwezekano ni mkubwa mno.
 
Huenda huyu binti mume wake kicheche. Anaweza kuwa anataka kukutumia kama njia ya kulipiza kwa mumewe.
 
kampa, kampa tena! Kaumiza, anataka kuumiza tena! Changanya na zako!
 
Back
Top Bottom