Alimaanisha Nini?

Signora D

Member
Aug 2, 2012
19
5
kama binti niliejitoa katika himaya ya mapenzi baada ya kuumizwa vibaya na first love kisha kuoa imeaditely baada ya breaking up with me, niliapa kuwa sitopenda tena!! nilibainisha msimamo wangu kwa muda wa miaka miwili kukaa bila mtu, ingawa nilikumbana na vikwazo vingi, vishawishi na tamaa but nilimuomba Mungu na niliweza kuikimu nafsi na moyo wangu kwa mda huo!!

kwa bahati nilimaliza chuo vyema na nikabahatika kupata nafasi ya masomo ya juu nje ya nchi!! wakati nashughulikia swala langu hilo nilikutana na kijana mmoja, mpole na mkarimu sana na kwa kuwa yeye alikuwa mzoefu wa safari hizo aliweza kunijuza mengi na kunisaidia hatua kwa hatua hadi safari yangu ilipokamilika, nikiwa airport kuagana na baba na mama na mdogo wangu, aliweza kunisaidia each step mpaka kuniaga nikiwa on board( he had access on the flight) wakati namuaga i felt so emotional na nilijua i felt kitu cha tofauti kwa mda ule! nikiwa nje tulianza mawasiliano ya ukaribu zaidi! skype,online chats, zote zilituwezesha kutufanya kama tuko pamoja mda wote!! kiukweli nilimpenda sana na ilinibidi nivunje msimamo wangu nakuanzisha the distance love!!!

Nisiwachoshe wana jf nina miezi miwili tangu nimerudi toka safari yangu ya masomo, kwa bahati nikapata kazi karibu na ofisi ya huyu kaka,,CHAKUSHANGAZA ni kwamba huyu kijana HATAKI MAWASILIANO NA MIMI SINCE NIMERUDI NIKIULIZA KWANINI ANASEMA YEYE ANA MTU WAKE AND THAT WAS ONLY A DISTANCE LOVE!!! NOW THAT AM HERE HE NO LONGER NEED ME PHYSICAL!! NILISTAAJABIKA KWA SABABU NASHINDWA KUJUA ALIMAANISHA NINI KUANZISHA UHUSINANO ULE?:disapointed:
 
Pole hii ndo dunia na haya ndo maisha so just take it usilazimishe kitu wala kulalamika. Binafsi naona kama huyo mtu anakupenda ndio maana amekuambia kuwa ana mtu wake kuliko kama angekudanganya
 
Kipi cha ajabu hapo..jamaaa alipenda distance love na wewe na kamwe si hili la karibu,...acha kumlazimisha usije vunja upendo wa wapendanao...ahahaaaaaaaaaaaa_this is bongo bhana
 
That was just a distance love for him...! alikuchukulia kama mpenzi aliyembali and i am sure kama ingetokea angekuja huko ulopokua angeweza kua mpenzi wako vizuri tu. shida ni kwamba huyu mtu alikuwa na mpenzi wake tokea mnaanza mahusiano and of course as a man haikua lazima kukwambia mapema na ukumbuke mambo kama haya hutokea sana katika mahusiano, kwa sababu mbalimbali kama mtu unajikuta mara nyingi haushindi sana na mpenzi wako so unapata muda mwingi wa kuongea na mtu fulani na hata kuanza urafiki wa aina hiyo (long distance relationship)

kwa hiyo imekua ngumu sana kwake kuwa na muda na wewe coz ana mtu wake, na akicheza foul hapo itagundulika. Kubali matokeo tu, siku moja mambo yatakua poa
 
Aseee its better amekujuza mapema kuwa kwenye moyo wake haupo.
Usijaribu kulazimisha penzi kwa huyo jamaa coz utaishia kuvunjika moyo.
Chukua tym yako,utampata wa kwako,subiri mida ufike.
 
Labda uliapa kwa Mungu wako kwamba hutopenda tena, na hayo ni matokeo ya kiapo chako, ukiweka ahadi na Mungu inatimizika tu.
 
duuu kazi ipo,but jibu amekupa kuwa ilikuwa distance love so take your time and look for other things
 
pole sana, inaelekea wewe ulimaanisha wkt jamaa alikua anazuga tu.
Ulipokuwa nje Hukuwahi kumuuliza kama ana mtu?
Hamkuwa na plan yoyote nae au mlikua mnapeana kampany tu?
Huyo kashakutema na usijaribu kulazmisha, utaumia.
Jitulize na uombe sana umpate wa kweli wa kukufaa.
 
hommie si umeambiawa hapo mambo ya skype na maninii sijui
Hhahahaha........... hommie, nlitaka aseme mwenyewe bana. Kwa hiyo jamaa limeshachungulia Ikulu ndogo na miti iizungukayo?

Amaa kweli:

I may be walking slowly, But I never walk backwards! and Whenever I walk backwards, Its for a long jump!!
 
pole mwaya yanapita tu hayo, ila wakati mnaanzisha uhusiano wenu wa skype na nk alikwambia hana mtu? Alikwamnia malengo yake ya baadae juu yako?
 
Hhahahaha........... hommie, nlitaka aseme mwenyewe bana. Kwa hiyo jamaa limeshachungulia Ikulu ndogo na miti iizungukayo?

Amaa kweli:

I may be walking slowly, But I never walk backwards! and Whenever I walk backwards, Its for a long jump!!
hahahaha Chezea skype weyeeee!!
 
Labda hakuwa na mapenzi ya kweli, may be t was just a crush!!Ndo mapito ya mapenzi,mimi nlikua naskiaga story ila yalivonikuta nkajua kumbe kuumizwa is a must???sizani kama kuna mtu ambaye hajawahi kuumizwa kwenye maswala ya mapenzi.So uanhitaji mda tu utapata wako wa ukweli
 
Usilazimishe mapenzi pasipo na penzi! Njoo huku machungu yatapoa!
 
Back
Top Bottom