Buzi Maarufu
JF-Expert Member
- Oct 30, 2019
- 422
- 330
Nilianza mahusiano naye akiwa na mtoto mmoja ambaye kwa wakati huo baba yake alikuwa hajulikani,Mwaka mmoja baadaye baba wa mtoto akajulikana na kujitambulisha rasmi.
Baada ya utambulisho nikawa na wasiwasi kuhusu hatima ya mapenzi yetu,nikamuuliza mwenzangu,Je ikitokea jamaa akataka kukuoa nawewe uko na mimi itakuwaje? akaniambia ikishakuwa hivyo basi mahusiano ya mimi na yeye yatakuwa yamefika tamati.
Nikamuuliza Kwanini ? Akajibu kwasababu hataki kuzaa watoto wa baba tofauti tofauti,kwakuwa nampenda Sana nikaendelea kusubiri maamuzi ya mkwezi mwenzangu,miezi ikaenda ghafla mawasiliano ya wazazi wenza yakawa yamedhoofu hatimaye kufa kabisa, hakuna cha pesa kwa ajili ya mtoto wao wala chochote.
Kwangu mimi ikawa ni shangwe nikaitumia hiyo nafasi vizuri sana, nikatia mimba mtoto akazaliwa jana katimiza miaka minne na tukamfanyia kasherehe uchwara kwa ajili ya kutimiza 4yrs.
Tukiwa kwenye sherehe kuna mtu kanitonya mzazi mwenza wa yf ameanza kutoa huduma kwa mwanaye kuanzia mwaka jana mwezi wa pili,usiku wa jana tumekesha tukizozana,nilimuuliza Kwanini wanawasiliana kimyakimya hanishirikishi? Yf anadai kwamba nisiwe na shaka yoyote mawasiliano yao ni kwa ajili ya mtoto tu hakuna kingine zaidi,"si ulishaniapisha nikaapa nikifanya usaliti nife hapohapo kwenye tukio! Bado uniamini?unataka nifanye nini kingine zaidi ya kiapo?
Nipo tayari kwa lolote kwa ajili ya uhai wa ndoa yetu.Nikamwambia,Unatakiwa usitishe mawasiliano na huyo mtu kwakuwa mtoto yupo kwa bibi yake na ndugu zako wapo basi mpe namba zao, atakuwa anawatumia wao hizo pesa, akaniambia nduguze sio waaminifu pesa haziwezi kumfikia mlengwa la sivyo nimwambie baba mtoto awe anakutumia wewe.
Mimi nikagoma,Ushauri wenu ndugu zanguni mapigo ya moyo yananienda mbio sana nahisi naibiwa sina raha sina amani, chakula hakiliki maji hayanyweki.