Alikula kiapo akinisaliti afe, Ila bado nina mashaka

Alikula kiapo akinisaliti afe, Ila bado nina mashaka

Duh, pole sana ase...yani kwamba ulipomuuliza mzazi mwenzake akimuhitaji waoane wakati mpo naye naye akajibu ndiyo yupo tayari kukuacha kama mzazi mwenzake angemtaka waoane wakati mpo naye,serious nawe ukaona ni fursa,kweli tunatofautiana mawazo mbali sana(kwa upande wangu mm hiyo kauli ndio ingekuwa tiketi yake saiyo saiyo)
 
Nilimwambia hivyo,majjbu yake eti namuonea na nikimuacha tu nijiandae kuzika wawili kwa wakati mmoja,yeye na mtoto wetu,na hii kauli huwa anairudia mara kadhaa kila ikitokea tofauti kati yetu,Sasa sijui ni mikwara au ni kweli anaweza kufanya hivyo.
Hapo ameshakuweka kwenye ''roba'' kali sana. Hili la kusema ''ukiniacha basi jiandae kunizika mimi na mtoto wako'' wanalitumia sana wanawake wengi ambao wana tabia mbaya na hawataki kubadilika lakini hapo hapo wanataka ndoa iendelee.

Na wengi wanakuwa wameshapima na kuona unampenda sana mtoto hivyo akisema hivyo atakupandisha PB. Ila wewe umeyataka mwenyewe kabisa. Kama alikuambia jamaa angetaka kumuoa angekubali kwani hataki kuwa na watoto kwa baba tofauti, basi ilitakiwa wewe ujiongoze kwani ilikuwa inaonyesha kabisa hakupendi bali alikutumia kama tairi ya spare tu.

Nachoona sasa: atakuwa anakazwa na huyo jamaa kila akipata nafasi na roho yake iko huko. Wewe anakutumia tu ili aitwe ''mke wa fulani''. Inaendelea post ya chini....
 
Hapo ameshakuweka kwenye ''roba'' kali sana. Hili la kusema ''ukiniacha basi jiandae kunizika mimi na mtoto wako'' wanalitumia sana wanawake wengi ambao wana tabia mbaya na hawataki kubadilika lakini hapo hapo wanataka ndoa iendelee. Na wengi wanakuwa wameshapima na kuona unampenda sana mtoto hivyo akisema hivyo atakupandisha PB. Ila wewe umeyataka mwenyewe kabisa. Kama alikuambia jamaa angetaka kumuoa angekubali kwani hataki kuwa na watoto kwa baba tofauti, basi ilitakiwa wewe ujiongoze kwani ilikuwa inaonyesha kabisa hakupendi bali alikutumia kama tairi ya spare tu. Nachoona sasa: atakuwa anakazwa na huyo jamaa kila akipata nafasi na roho yake iko huko. Wewe anakutumia tu ili aitwe ''mke wa fulani''. Inaendelea post ya chini....
Ukweli mtupu mkuu ,nilibugi mwenyewe nilitakiwa kumbwana mapema kabisa baada ya kutamka hayo,na kuhusu mtoto ni kweli nampenda sana naye anajua.
 
duh,pole sana ase...yani kwamba ulipomuuliza mzazi mwenzake akimuhitaji waoane wakati mpo naye naye akajibu ndiyo yupo tayari kukuacha kama mzazi mwenzake angemtaka waoane wakati mpo naye,serious nawe ukaona ni fursa,kweli tunatofautiana mawazo mbali sana(kwa upande wangu mm hiyo kauli ndio ingekuwa tiketi yake saiyo saiyo)
Hicho kitu huwa kinaniuma sana Mkuu,ndio maana nimeamia salama yangu ni kutafuta mchepuko tu.
 
Nilimwambia hivyo,majjbu yake eti namuonea na nikimuacha tu nijiandae kuzika wawili kwa wakati mmoja,yeye na mtoto wetu,na hii kauli huwa anairudia mara kadhaa kila ikitokea tofauti kati yetu,Sasa sijui ni mikwara au ni kweli anaweza kufanya hivyo.
Hili la ''jiandae kuzika'' huwezi kulipuuzia. Kuna visa vya wanawake wengi wamewahi kujiua na watoto wao ili tu kumkomoa baba. Nina experince kidogo: Ndugu yangu alizaa na dada mmoja baade akageuka ''paka shume''. Yaani dizaini ya shangingi fulani hivi, kutwa kucha yeye na mashoga zake, mara vikoba, mara biashara zisizoeleweka ili mradi tu hasikii wala hatii kauli ya mume.

Kila akiambiwa waachane anajibu ameshapozewa muda wake na kuzalishwa hivyo akiachwa tujiandae kuzika mama na mtoto. Na mtoto ndiyo kabisaa anang'ang'ania kuwa mtoto wake haendi popote wakati alikuwa hana hata muda wa kumwangalia. Tulikuwa tunamjua akili zake na tukaona anweza kufanya kweli. Ikabidi aishi naye tu ki-mgogoro na nyumba ilikuwa haikaliki kwani alikuwa anafanya anavyotaka yeye. Alitumia ujanja mmoja tu.

Alitafuta mshiko wa kutosha akaongea na wale mashoga zake kwa kirefu na kuwalipa. Akawaambia wam-brain-wash na kumwambia kuwa kuna maisha mazuri kama akitengua ndoa na kumtoa mtoto kwa baba yake kwani atapata muda kufanya shughuli nyingine. Kweli akaingia line na hapo ndipo ilikuwa pona yake japo baadae alitakuja kuleta fujo akitaka apewe mtoto lakini hakufanikiwa.
 
Kuna jamaa humu alikuwa anatafuta single maza amuoe.
Mawasiliano ya wazazi huwa hayafi milele.
Jiamini, fanya mambo yako. Wakigongana potelea mbali kwasbb ni msalaba ulioamua kuubeba mwenyewe.
"Ikitokea baba mtoto amerudi, akaomba msamaha mrudiane. Mapenzi yatakuwa mwisho kwasbb hataki kuzaa watoto baba tofauti kwasababu anampenda sana"
Hapo anapompenda sana ndiyo na mchezo atapewa
Ya kimila
 
Ufala Ni wako mwenyewe,, tangu kutamkiwa atarudi kwa mzazi mwenzie ilitakiwa ujikatae hapo hapo we ukajifanya wajua kupenda acha ukome
 
Nilianza mahusiano naye akiwa na mtoto mmoja ambaye kwa wakati huo baba yake alikuwa hajulikani,Mwaka mmoja baadaye baba wa mtoto akajulikana na kujitambulisha rasmi.
Baada ya utambulisho nikawa na wasiwasi kuhusu hatima ya mapenzi yetu,nikamuuliza mwenzangu,Je ikitokea jamaa akataka kukuoa nawewe uko na mimi itakuwaje? akaniambia ikishakuwa hivyo basi mahusiano ya mimi na yeye yatakuwa yamefika tamati.
Nikamuuliza Kwanini ? Akajibu kwasababu hataki kuzaa watoto wa baba tofauti tofauti,kwakuwa nampenda Sana nikaendelea kusubiri maamuzi ya mkwezi mwenzangu,miezi ikaenda ghafla mawasiliano ya wazazi wenza yakawa yamedhoofu hatimaye kufa kabisa,hakuna cha pesa kwa ajili ya mtoto wao wala chochote.
Kwangu mimi ikawa ni shangwe nikaitumia hiyo nafasi vizuri sana, nikatia mimba mtoto akazaliwa jana katimiza miaka minne na tukamfanyia kasherehe uchwara kwa ajili ya kutimiza 4yrs.
Tukiwa kwenye sherehe kuna mtu kanitonya mzazi mwenza wa yf ameanza kutoa huduma kwa mwanaye kuanzia mwaka jana mwezi wa pili,usiku wa jana tumekesha tukizozana,nilimuuliza Kwanini wanawasiliana kimyakimya hanishirikishi? Yf anadai kwamba nisiwe na shaka yoyote mawasiliano yao ni kwa ajili ya mtoto tu hakuna kingine zaidi,"si ulishaniapisha nikaapa nikifanya usaliti nife hapohapo kwenye tukio! Bado uniamini?unataka nifanye nini kingine zaidi ya kiapo? nipo tayari kwa lolote kwa ajili ya uhai wa ndoa yetu.
Nikamwambia,Unatakiwa usitishe mawasiliano na huyo mtu kwakuwa mtoto yupo kwa bibi yake na ndugu zako wapo basi mpe namba zao, atakuwa anawatumia wao hizo pesa, akaniambia nduguze sio waaminifu pesa haziwezi kumfikia mlengwa la sivyo nimwambie baba mtoto awe anakutumia wewe.
Mimi nikagoma,Ushauri wenu ndugu zanguni mapigo ya moyo yananienda mbio sana nahisi naibiwa sina raha sina amani, chakula hakiliki maji hayanyweki.
Pole sana
 
Ufala Ni wako mwenyewe,, tangu kutamkiwa atarudi kwa mzazi mwenzie ilitakiwa ujikatae hapo hapo we ukajifanya wajua kupenda acha ukome
Pamoja na kuniita fala bado nakubaliana nawewe Kweli nilibugi
 
Kuna jamaa humu alikuwa anatafuta single maza amuoe.
Mawasiliano ya wazazi huwa hayafi milele.
Jiamini, fanya mambo yako. Wakigongana potelea mbali kwasbb ni msalaba ulioamua kuubeba mwenyewe.
"Ikitokea baba mtoto amerudi, akaomba msamaha mrudiane. Mapenzi yatakuwa mwisho kwasbb hataki kuzaa watoto baba tofauti kwasababu anampenda sana"
Hapo anapompenda sana ndiyo na mchezo atapewa
Lakini tayari keshazaa na mimi mkuu,mtoto katimiza miaka minne jana
 
Hicho kitu huwa kinaniuma sana Mkuu,ndio maana nimeamia salama yangu ni kutafuta mchepuko tu.
Bado hiyo siyo salama ,kikubwa tafuta mke mwema mwenye maadili haijalishi hata kama ana mtoto sio dhambi kikubwa ni upendo na maadili,mwanamke mwenye upendo wa dhati hawezi kukwambia hiyo kauli
 
Hili la ''jiandae kuzika'' huwezi kulipuuzia. Kuna visa vya wanawake wengi wamewahi kujiua na watoto wao ili tu kumkomoa baba. Nina experince kidogo: Ndugu yangu alizaa na dada mmoja baade akageuka ''paka shume''. Yaani dizaini ya shangingi fulani hivi, kutwa kucha yeye na mashoga zake, mara vikoba, mara biashara zisizoeleweka ili mradi tu hasikii wala hatii kauli ya mume. Kila akiambiwa waachane anajibu ameshapozewa muda wake na kuzalishwa hivyo akiachwa tujiandae kuzika mama na mtoto. Na mtoto ndiyo kabisaa anang'ang'ania kuwa mtoto wake haendi popote wakati alikuwa hana hata muda wa kumwangalia. Tulikuwa tunamjua akili zake na tukaona anweza kufanya kweli. Ikabidi aishi naye tu ki-mgogoro na nyumba ilikuwa haikaliki kwani alikuwa anafanya anavyotaka yeye. Alitumia ujanja mmoja tu. Alitafuta mshiko wa kutosha akaongea na wale mashoga zake kwa kirefu na kuwalipa. Akawaambia wam-brain-wash na kumwambia kuwa kuna maisha mazuri kama akitengua ndoa na kumtoa mtoto kwa baba yake kwani atapata muda kufanya shughuli nyingine. Kweli akaingia line na hapo ndipo ilikuwa pona yake japo baadae alitakuja kuleta fujo akitaka apewe mtoto lakini hakufanikiwa.
Duu ndio maana tunakufa mapema,maisha magumu mahusiano magumu.
 
Amegoma kabisa hataki zitumwe kwao mkuu,ndoa imeingia doa.
Bora iingie doa uwe salama ndgu yangu.
Hiyo pesa wala haitumii kwa matumizi ya mtoto bali ni ishu zake binafsi ndio maana hataki akose hiyo fursa ya kuzitafuna.

Wewe binafsi jiulize anawallipa nini hao wanomelelea mwanae?? Hata kama ni wazazi wake, wazazi kazi yao ilikua kumlea yeye na sio mtoto wake hapo ni lazima apeleke chochote kitu.

Sasa kama hawaamini aliowaachia mtoto ana akili kweli huyo?
Muulize huwa anamsaidiaje huyo mtoto huko? Yeye yupo mbali nae ni nani anaempa mahitaji yake ya kila siku kama sio hao anaowagomea kuwapa hiyo hela.

Pole kwa utakayoendelea kuyapitia mkuu, jiandae kwa kufumania.
 
Anadai kuwa rafiki yake anayemuamini ambaye atakuwa anamtumia hizo hela,Ila hataki kuwaunganisha rafiki yake na mzazi mwenzake.
 
Kama unampenda, kaa naye chini mueleze jinsi unavyojisikia vibaya.
Ukiona anazidi kuwasiliana na baba wa mtoto. Kuwa bize na mambo yako. Rudi nyumbani usiku muda wa kulala, asubuhi amsha. Usimsahau kumuona mtoto mara moja, kula naye chakula.
Huenda akajirekebisha.
Lakini tayari keshazaa na mimi mkuu,mtoto katimiza miaka minne jana
 
Anadai kuwa rafiki yake anayemuamini ambaye atakuwa anamtumia hizo hela,Ila hataki kuwaunganisha rafiki yake na mzazi mwenzake.
Daah pole sana mbona hapo ni wazi kua unapigiwa we jamaa, yaani hugutuki tuu??

Yaani ana wivu na ex wake pmbav kabis huyo. Pole yako lakini.
 
Kama unampenda, kaa naye chini mueleze jinsi unavyojisikia vibaya.
Ukiona anazidi kuwasiliana na baba wa mtoto. Kuwa bize na mambo yako. Rudi nyumbani usiku muda wa kulala, asubuhi amsha. Usimsahau kumuona mtoto mara moja, kula naye chakula.
Huenda akajirekebisha.
Nampenda sana tu ila najipenda zaidi mimi kuliko yeye,nikizikusanya faranga nanunua samani kadhaa namtafuta mchepuko akae,badala ya kurudi usiku nitakuwa narudi hata baada ya wiki.
 
Wanaume mabwege kumbe bado wapo licha ya matukio yote yanayotokea haya kila siku.
 
Back
Top Bottom