Aliko mgombea mwenza wa Dr Slaa 2010

Heading ya thread imeshajibiwa; kuna waliosema yupo pre-form one, wengine yupo anauza genge. Yote kheri, kama angekuwa yuko anaiba au anafanya ujambazi nk hapo ningelaumu, lakini kwa kuwa yupo anafanya yaliyo halali, sioni tatizo.
Hivi hao walio na elimu zaidi ya std 7 ambao kwa sasa wako wanaifisadi nchi tuwapongeze kuliko huyu anayeuza gengeni?
Ebu tupanue mada, hivi wagombea urais walikuwa wangapi; je wagombea wenza wao wako wapi?; je wagombea wenza wao wanafuatana nao kila mahali. Mgombea wa NCCR mageuzi alikuwa Kigoma, je alifuatana na mgombea mwenza wake?
Mengine yanayojibiwa humu yanatokana na mleta mada kutumia neno kioja. Kama darasa la saba ni kioja basi vioja wako wengi nchini; na katika nchi nyingine tayari mmeelezwa hata wale ambao hawakufika darasa la 7. Tuache kukejeli elimu za watu, eti kuwa std 7 ni poyoyo, si ajabu baba yako naye akawa poyoyo!
 
katika uchaguzi mkuu wa Tanzania 2010 kulikuwa na kioja kimoja ambako mgombea mwenza wa Dr Slaa ambaye alikuwa na elimu ya darasa la saba hii ni ajabu sana kwa chama chenye kujivunia wasomi lukuki! huyu bwana yuko wapi asa hivi mbona hasikiki? na mbona kwenye shughuli mbalimbali za chama haoenekani?? unajua laiti Slaa ,yule mgombea mwenza wake angeshida angeingia kwenye kumbukumbu za dunia" a standard seven leaver being the vice president" kama sikosekei mtu mwingine mwenye elimu ya msingi ambaye aliweza kushika nafasi za juu za nchi katika ukanda wetu huu ni Idd Amin

Tungekuwa tunazingatia ELIMU kiongozi mkuu wa waislamu Mufti Shaaban BIN Simba ambaye ni darasa la saba asingechaguliwa na waislamu kuwa mufti wao.
 
..kwa uelewa wangu Chadema walikuwa wanamtaka Juma Duni au Hamad Rashid kwa nafasi ya mgombea mwenza.

..huyo waliyemsimamisha alichukuliwa dakika za majeruhi baada ya juhudi za kuwashawishi hao wawili kushindikana.

..siwezi kuwalaumu sana Chadema ktk hili, ni vigumu kupata Mzanzibar atakayesimama against CCM au CUF.

..pia kabla ya uchaguzi Chadema kilionekana kama chama kidogo kisichokuwa na future yoyote ile ktk siasa za Tanzania.

NB:

..Chadema wasirudie makosa waliyoyafanya 2010 kwa nafasi ya makamu wa raisi wa muungano.
 
NAJUA NI DR. BUT KAFANYA NINI KWA TAIFA NA UDOKTA WAKE AU KUTOA MEMO tUUU!


Kafanya kama walivyofanya wasomi wa Tanzania, kuacha profession na kujiunga na mradi wa kupata fedha haraka, mradi wa siasa.
 
Muheshimiwa huyu hapa mimi wasiwasi wangu hillo shati la CUF iiiiii.jpg
 
..kwa uelewa wangu Chadema walikuwa wanamtaka Juma Duni au Hamad Rashid kwa nafasi ya mgombea mwenza.

..huyo waliyemsimamisha alichukuliwa dakika za majeruhi baada ya juhudi za kuwashawishi hao wawili kushindikana.

..siwezi kuwalaumu sana Chadema ktk hili, ni vigumu kupata Mzanzibar atakayesimama against CCM au CUF.

..pia kabla ya uchaguzi Chadema kilionekana kama chama kidogo kisichokuwa na future yoyote ile ktk siasa za Tanzania.

NB:

..Chadema wasirudie makosa waliyoyafanya 2010 kwa nafasi ya makamu wa raisi wa muungano.


Mambo mengi yanazuia CHADEMA kufuata ushauri wako juu ya kumpata mtu wa aina unayoitaka. Wasomi wapo wengi lakini si unajuwa Wazanzibari hawawezi zogo na kwenye maandamano yao hupeleka wanawake mbele,wataweza kweli kupambana na dola?
 
Chadema hawakufanya vile kwa kupenda, Ile ni kutokana na utaratibu wa kawaida uliopa kwa vile tz ni jamuhuri ya muungano rais akitoka upande mmoja basi makamo atoke upoande mwengine. Chadema wao hawana suporter ZNZ ndio wakakosa mwanachama wa chadema alokuwa msomi kutoka ZNZ ili kuchukua hiyo nafasi.
Tukizungumza ukweli basi tutaona kwamba chadema hakina sifa ya kuiongoza TZ as union republic, ila kinaweza kuiongoza Tanganyika tu. mimi nadhani katiba ijayo inapaswa kuweka wazi ili chama kiwe na sifa ya kuiongoza TZ ni lazima kiwe kimepata atleast nusu ya kura kutoka kila upande wa jamuhuri. na kuwe na serekali tatu ili kama chadema kitachaguliwa tanganyika kiachiwe kuiongoza tanganyika pekee bila kuathiri muungano, na kikikosekana chama chenye uhalali wa kuiongoza TZ basi vyama vishirikiane kuunda collition gvt ilimradi kwenye hiyo collition ipatikane supoet kutokapande zote za muungano.
 
Kwa kweli uongozi si lazima elimu, ila kiongozi mwenye elimu nzuri ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kama akiamua kuliko kwa yule asiye na elimu hasa katika karne hii ya 21.
 
Hivi uongozi unahitaji elimu ya chuo au busara? Angalia baraza la mawaziri lina wasomi wakubwa wangapi na wamekufanyia nin mpaka sasa cha muhimu? uongozi ni karama wala hauhitji elimu.Yeye haonekan kwasabab hana nyazifa kitaifa lakin dr. slaa ni katibu taifa
 
Kama tunapenda maendeleo ya demokrasia katika nchi yetu basi ni vizuri tupongeze pale ambapo chama cha siasa kinafanya vizuri na pale wanapokosea tunawakosoe. Nilisikitika sana, ingawa sikuwa na la kufanya. Education is civilazation, vipi tuongozwe na uncivilized person. Sijui chadema walifikiria nini, mpaka wakafikia hapo. Ni bora kama hakuna mtu basi nafasi iwe wazi, kama vile Egypy ya Mubarak au wangetangaza, vijana tungejitokeza. Tungependa tuwe na chama kimoja kikuu cha upinzani, kama vile marekani. Lakini kwa kuwa na VP wa elimu dunia hatuwezi kufika. Mimi nina mfano hai, mbunge wangu ni STD 7 ingawa sikushiriki kumchagua, wananchi wameanza kujutia. Chadema wasije rudia kosa kama hilo. Hatupendi kuweka historia za kijinja" Hati VC P la saba"

Kunatouti kubwa sana kati ya kuelimika na kusoma,....*(kunawasomi wengi tu, waonyesha wameonyesha madudu matupu katika uongozi) Naomba ifahamike kuwa uongozi ni WITO, ni KUJITOA katika kutumikia watu bila manung'uniko.

Napingana na wewe ,unaposema darasa la saba (mwenye cheti cha darasa la saba) hawezi kuwa Kiongozi(Hiyo sio sahihi wala siyo jambo la msingi kuongelea cheti cha MUTU).
Mafisdi wangapi niwasomi wanaotambulika Kimataifa,wametupeka kubaya, au tuwataje majina..., wengine walitumia elimu zao hata kumdanganya Hayati baba wa Taifa.
Nadhani na ewe ni moja wapo ya wale walioenda chuoni kuchukua shahada/ stashahada ya kitu fulani....../ hukuenda kusomea, maana unadhani kuongea kiingereza ni kustaarabika, P/se edit:civilisation not civilazation.Ingekuwa swala ni kusoma wacheza disco wasingeku viongozi,ingekuwa katia siasa lazima usome polical science na sio vinginevyo.
 
Itahwa, unanishangaza sana! Elimu sio kigezo muhimu katika uongozi japo yaweza kusaidia. Kwanza, uongozi unahitaji hekima zaidi kuliko elimu. Lakini pia utambue kwamba elimu sio lazima uende darasani! Pia usifikiri kwamba kusoma ndio kuongoza! Wangapi wanaojiita ''wasomi' wameshindwa kuongoza hata ofisi ndogo ya watu watatu! Ronald Reagan alisoma kitu gani kikubwa kuwaongoza Wamarekani? Bill Gates an elimu kiasi gani kuendesha kampuni kubwa yenye mafanikio kama Microsoft? Mzee Kawawa (RIP) alikuwa na elimu gani? Mzee Karume alikuwa na elimu gani? Amefanya makubwa gani kwa nchi hii Zanzibar?
Natumaini bado unaogelea kwenye lindi la kasumba ya Watanzania ya kuabudu "usomi"! Wengine wakisikia mtu anaongea kiingereza tu wanajua mtu huyo kasoma.
Labda nikuambie tu hakuna guarantee kwamba ukiwa msomi basi ndio utafanya vizuri kiutendaji. Tena kwa uzoefu wangu wasomi sio watendaji wazuri. Hata kwenye mafanikio ya kimaisha wasomi wako nyuma kuliko hao wanaonekana sio wasomi.
 
Back
Top Bottom