Alichosema Ismail Jussa

Acheni majungu, pandeni ulingoni tuanze kazi tarehe 20 hadi october 30. Tuone nani ananguvu, tunapigana vikumbo weeeee wakati tunao muda wa kuwaeleza watanzania yote, kama mnataka kufanya kampeni za majungu hazilengi mabadiliko bali ni kutaka kuwasogeza mbele ccm ili washinde kirahisi.

Mi sitaki haki kuzinguana na huyu jamaa anataka tuache mageuzi, lakini cha msingi ni utaifa mbele dini nyuma.
 
Someni pia makala ya Ansbert Ngurumo ya wiki hii. Muafaka wa CCM na CUF si visiwani Zanzibar peke yake. CUF itatumika mainland katika jitihada za kuipaka tope Chadema. Yameshaanza. Rev. Kishoka, ubarikiwe.

Chadema inawaumiza watu vichwa Mkuu Jasusi, wapo watu hivi sasa hawalali ! Bahati nzuri Chadema ilipofikia haishikiki tena na mbinu zozote za kukipaka matope zimechelewa kwani tayari wana kinga ya wananchi ambao hawatakubali tena kudanganywa kirahisi. Subirini tu kampeni zianze rasmi, mtashuhudia ukweli wa aliyosema Ansbert Ngurumo na wapo watu wataugua ugonjwa wa moyo.
 
Ni matusi kuwaambia watanzania eti Slaa amuunge mkono Lipumba. It's a joke of the highest order. These guys are simply narcistic and they are out of touch. Acha wananchi wakaamue.
 
Ni matusi kuwaambia watanzania eti Slaa amuunge mkono Lipumba. It's a joke of the highest order. These guys are simply narcistic and they are out of touch. Acha wananchi wakaamue.

Ndoa ya CCM na CUF tutasikia mengi sana mwaka huu wa uchaguzi!
 
What did you say about "wachumi"? Naona ungefocus kwenye mada rather than kwenye discipline za watu. Please apologize to all Economists.
 
Sasa mlimtegemea huyu Mheshimiwa Jussa aseme nini? Yeye ni mwanachama wa CUF na anataka chama chake kishinde. Mpingeni hoja zake kama alivyofanya Mkandara na si kuingiza mambo ya kutupiana matope.

Amandla....
.
 
Mnaolumbana mmejiandikisha kupiga kura? Napata wasiwasi hapa
JF wengi hawajajiandikisha hata kupiga kura lakini huwa wanashabikia
tu hizi mada. ukiipoteza nafasi ujue huipati tena mpaka baada ya miaka
mitano kama utakua hai.
 
Kuna mtakao kasirika na wengine kufurahia au hata kulalamika. Huu ujumbe wa huyu jamaa wa CUF nimeusoma mahali na nimeona ni heri tuusome wote.

Rev. Kishoka shukrani kwa kutupatia huu waraka ambao kwa mtazamo wangu unasaidia kutuonyesha jinsi washindani wa Chadema wanavyokiona chama hicho. Mimi nadhani waraka huu utawasaidia sana Chadema wenyewe kwa sababu unawapatia fursa ya kuona ni jinsi gani washindani wao wanavyowaona.

Nikiuangalia waraka huu nadhani kuna ukweli ndani yake na pia kuna maeneo ambapo mwandishi amepotosha ukweli ama ameongeza chumvi ili kukiinua chama chake na hii nadhani ni kawaida kwa mwandishi ambaye ni mkereketwa wa chama fulani. Simtarajii Makamba, kwa mfano, kukisifia chama cha CUF au CHADEMA na kukiponda chama chake kinachompa ulaji. Kwa sababu ya muda nitaangalia yale ambayo nadhani mwandishi amezidisha chumvi.

Ni kweli kuwa Professor Lipumba ana uzoefu mkubwa wa masuala ya uchumi wa nchi na kimataifa lakini pia amekuwa kiongozi wa CUF kwa muda mrefu hivyo ana uzoefu wa kuongoza chama. Lakini siyo kweli kuwa Dr. Slaa hana uzoefu wa uongozi zaidi ya kuwa whistleblower kama mwandishi anavyodai. Ila ni kweli pia kuwa Professor Lipumba hajawahi kugombea na kushinda nafasi yoyote ya uwakilishi wa wananchi ukiondoa uchaguzi wa Mwenyekiti wa CUF pekee.


Dr. Slaa amekuwa mbunge wa kuchaguliwa wa jimbo la Karatu kwa miaka 15 na amefanya mambo ambayo yamemjengea uhalali jimboni na kuwa kikwazo kwa CCM kumwondoa jimboni. Ukiongea na watu wa Karatu watakwambia kuwa amefanya mambo mazuri huko na ndio maana watu wanamwunga mkono. Kwa sisi ambao si wakazi wa Karatu tunamtambua Dr. Slaa kama mbunge mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na ametumia uwezo huo kuchangia kwa kiwango kikubwa mijadala muhimu karibu yote iliyopita bungeni. Lakini pia amekuwa mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali za mitaa na yote hii imempa uzoefu wa kiuongozi.

Ni kweli kuwa kuna tuhuma za ukabila kwenye chama cha Chadema na hizi kwa kiasi kikubwa zimekuzwa na chama tawala ili kukiondolea uhalali chama cha chadema. Tuhuma hizi pia ziliwahi kuongelewa na Marehemu Chacha Wangwe. Mimi nadhani Chadema wanapaswa kuliangalia na kulitolea ufafanuzi hili ili lisije likatumiwa na wapinzani wao kama mtaji wa kuwashambulia wakati wa kampeni.

Lakini nimeshangaa kuzisikia tuhuma hizi na hasa ya udini toka kwa mtu wa CUF kwa sababu hata nao wana tuhuma kama hizo zikitolewa na watu wa CCM. Kwa mtazamo wangu CUF hawajafanya lolote kuondoa hisia hizo. Chama cha CUF kinatuhumiwa kuwa na upemba, udini na vurugu (mapanga shaa). Ukiangalia wabunge wake wengi wanatoka Pemba na wachache sana Unguja na Tanganyika. Hivyo kudai kuwa chama hiki ni cha muungano kuliko Chadema wakati kimewekeza sehemu moja ya muungano ni kutokuwa mkweli.

Mwandishi amekishambulia chama cha Chadema kuwa hakina Demokrasia na kuwa viongozi wake wanateuliwa na familia ya Mtei/Mbowe. Na ametoa mfano wa uchaguzi wa mweyekiti wa CUF ambapo Prof. Safari alipewa fursa ya kugombea. Kwanza siamini kuwa chama cha chadema ni chama cha familia ya Mtei/Mbowe kama ambavyo siamini kuwa CUF ni chama cha Maalimu Seif Shariff Hamad. Ninachofahamu ni kuwa Prof. Safari alilalamika kuwa hakukukuwa na demokrasia kwenye uchaguzi ule na kuwa alifanyiwa mchezo mchafu. Sasa kuwa na mchakato wa kuchaguana pekee hakutoshi kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.

Tofauti za maoni au mitazamo kati ya wabunge wa Chadema haiwezi kuchukuliwa kuwa ni udhaifu. Kuna msemo kuwa ukiwa na watu kumi kwenye kikao na wote wakakubaliana na mawazo yanayotolewa na mmoja wao kwa asilimia mia moja bila kuwa na kipingamizi ina maana kuwa unahitaji mtu mmoja tu (mtoa mawazo) na kuwaondoa tisa waliobaki ili uwapate wengine wa kuchangia na kuboresha mijadala. Tofauti za mawazo na maoni ni kitu kizuri na chenye kujenga na kwa lazima kiungwe mkono na wapenda mabadiliko. Ni katika tofauti za maoni ndipo huzaliwa wazo zuri zaidi linalozingatia maslahi ya makundi yote yanayowakilishwa na watu wanaojadiliana.
 
Rev. Kishoka,

Kwanza kama ingekuwa mimi ningemjibu mkulu kwa kuhitaji mifano na takwimu zinazodhihirisha aloyasema yote.
Kwa mfano swali la kwanza:-
1. Prof. Lipumba is more competent and more exposed in both local and international affairs and leadership than Slaa whose experience is merely of a whistleblower.

Jibu:- Sio kweli kabisa, tumemwona Obama mwenye experience ndogo akiwa joined na kina J. Biden, Clinton na the whole bunch of experienced fellas ambao wamempa tafu. Anachoshindwa kuelewa huyu jamaa yetu ni kwamba kiongozi anayetakiwa ni yule mwenye Uzalendo, vision na Mbunifu wa kile anachokitaka ku accomplish at the end ili kuondokana na matatizo/mahitaji tulokuwa nayo - now, how to achieve all this, ndipo anachagua watu wa kuwa naye na sisi tunasemea Lipumba is one of them...
Pili Lipumba ni mchumi sii mbunifu wala hana vision....huyu ni sawa na mpangaji wagharama za matumizi na mapato. Mara zote wachumi sii wabunifu ila wazuri kwa kukadiria matumizi na mapato pia njia bora za kuwezesha hivyo - Ni Lipumba anayemhitaji Dr. Slaa.

2. CUF ni chama cha kitaifa wakati Chadema iko Tanganyika tu;

Jibu:- Je CUF imeshinda majimbo mangapi bara?
Kwani tunapozungumzia chama cha kitaifa, kinachohesabika ni uwakilishi wake sio kuhesabu wingi wa vibanda vyake mikoani.

3. Kwa performance ya kisayansi na si ya kukusanya watu kwa helikopta, CUF ina nguvu zaidi Bara na Zanzibar, kigezo ni kila uchaguzi CUF imekuwa mara zote inashika nafasi ya chama cha pili na hivyo kukipa sifa ya kuwa chama mbadala - angalia matokeo hata ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ambapo pamoja na magazeti kuibeba sana Chadema, bado CUF imeshika nafasi ya pili (kumbuka huu uchaguzi ulikuwa Bara peke yake)

Jibu:- Uchaguzi wa Kitaifa kulikuwa namajimbo 181 bara na Chadema ilipata ushindi wa viti 5 hali CUF hawakupata kitu. Zanzibar CUF walipata viti 22 kati ya viti 50. Kwa hiyo ushindi wa pili wa CUF unatokana na viti 22 vya visiwani na sio Bara. CUF haina nguvu bara sawa na Chadema isivyokuwa na nguvu visiwani.
pili, Uchaguzi wa sewrikali ya mitaa Chadema hawakushiriki na kusema kweli yalikuwa makosa makubwa. Hawakufanya hivyo kutokana na kuvunjika kwa umoja mlokuwa mmeanzisha hivyo wakaweka mawazo yao sehemu nyingine.

Swali la 4. jibu:- kuhusiana na CUF kujijenga zaidi ya Chadema. jamani lets not kid ourselves.. CUF imejijenga vipi?.. CUF na Chadema kitaasisi ni vyama ambavyo havina uwezo kabisa yaani wote wanabangaiza tu. Hili sii swala la kuhitaji mjadala kwani CUF na Chadema bado kabisa wamebanwa vibaya na CCM kiasi kwamba kujitangaza kwao kunategemea imani ya wanachama wake. Wote waliohama CUF wamepitia mitihani kama ya Chadema na vyama vingine vyote vidogo. Kumbuka kuhama kwa Lwakatale CUF ilitokea kipi.. fact is Hakuna aliye na afadhali.

5. Chadema kimeshindwa kujivua gamba la ukabila na udini na sasa ndiyo kinazidi kutopea huko wakati CUF imetanda kila pembe ya Tanzania;

Jibu:- Duh mkuu wangu, marafiki zangu wakubwa ni member waCUF damu, na kijiwe changu kikubwa ni pale K tea shop mjini Chagga st... ninawajua CUF kuliko unavyofikiria. Chadema kama ni Wadini au Wakabila, ni CUF pekee ndiyo ingeweza kuwaondoa ktk fikra hizo kama zipo kweli na mngewa join, lakini sio kuzungumzia nje hali CUF yenyewe inaonekana kusongwa na matatizo hayo hayo. Ushahidi wangu:- Why CUF imejikita kwa maswala ya Zanzibar zaidi ya bara?.

6. CUF kina mtandao wa chama wenye muundo uliokamilika wa uongozi uliojipanga kitaasisi wakati Chadema hakina muundo na huishia kuokota wajumbe wa vikao mitaani kupata uhalali wa vikao.

Jibu:- Chadema sii wajuzi wa kila kitu, vitu kama hivi ndivyo CUF could have bring in kama mchango wao. haiwezekani Chadema kuhitaji kuungana na chama ambacho hakina ubora wowote.

7. CUF kimeonyesha umakini mkubwa katika uongozi na hata katika Kambi ya Upinzani Bungeni kimeonyesha ukomavu tofauti na Chadema ambao hata wale wabunge wake 11 tu wanashindwa kuelewana..

Jibu:- Bungeni sio mahala pa kuonyesha unyenyekevu. Ni sehemu ya kuvuana nguo na sio kubebana kama CCM wanavyofanya ili mradi kulindana. Bungeni wajumbe wanakuja kuwakilisha wananchi na sio kuwakilisha chama. Kutoelewana ndio inaonyesha ukomavu wa watu kuona tofauti au matatizo ya bajeti inaposoimwa na sio kukubali kila unachoambiwa.

8. CUF kina misingi ya kidemokrasia na ndiyo maana hata Prof. Safari aliachiwa kushindana kwa uwazi na Prof. Lipumba kwenye nafasi ya Uenyekiti wakati Chadema kina uongozi wa kiimla wa muasisi wa Chama mwenye uwezo wa kumuengua mgombea Uenyekiti ili mkwewe apite bila ya kupingwa:

Jibu:- Kugombea kiti cha Uenmyekiti sio swala la demokrasia. hakuna kifungu chochote cha demokrasia kinacholazimisha au kushauri vyama kupitisha uchaguzi inapofikia swlaa la Mwenyekiti.. Na pengine huelewi kwamba Chadema mwenyekiti ni Mbowe na anayegombea Urais ni Dr.Slaa wakati CUF mwenyekiti ndiye mgombea kiti cha urais!

Yaani Rev. mkuu wangu huyu jamaa majibu tyake ni rahisi sana naweza kuyajibu pasipo hata kufikiria..Ila sidhani kama yeye yupo tayari kupokea maswali kutoka upande huu!.


Kaka I wish wengine nao wangejaribu kujibu hoja kama ulivyofanya na sio hizi name calling na cheap propaganda zinazoendelea halafu wanataka watanzania wawaamini kuwa wao ni mbadala wa CCM....

Tabia ya kukimbilia kuattack majina inaonyesha kuwa wengi wa washabiki wa UTUME WA SLAA wangependa kuwauzia watanzania mbuzi katika gunia bila ya kuwapa nafasi ya kumkagua mbuzi huyo. Na pia wanasahau kuwa kama wenzao hasa CCM ndio walio na upper hand katika strategy hiyo dhidi ya wao.

Ni wazi kuwa Jussa amejibu kishabiki na kuvutia kwake lakini wafuasi wa Slaa nao inabidi waonyeshe umakini na umahiri katika kujibu hoja ili kuwaondolea wasiwasi baadhi ya watanzania ambao bado wanashindwa kuiamini CHADEMA na pia UTUME WA SLAA...

Tanzania makini haiwezi kujengwa kwa style ya ujanjaujanja....

omarilyas
 
Ni matusi kuwaambia watanzania eti Slaa amuunge mkono Lipumba. It's a joke of the highest order. These guys are simply narcistic and they are out of touch. Acha wananchi wakaamue.

Just like saying Prof Lipumba ammunge mkono Dr Slaa.....

Kaka ukweli ni kuwa jinsi mnavyowaona CUF ndivyo ambavyo nao wanavyowaona lakini zaidi hata kwetu wengine tunaona nyote mna tatizo la kuwa simplistic, out of tocuh na zaidi insensitive...

omarilyas
 
Blow aliyoitoa mwandishi (labda kweli ni Jussa) inaitwa "UPPERCUT",,,inawauma lakini ndio mchezo
MS upo?
 
Hivi mpangilio wa KUDUMU wa Prof Lipumba na Maalim kuwa Mwenyekiti na Katibu Mkuu na ule wa kuwa wagombea URAIS wa JMT na Nchi ya Zanzibar utahitimishwa lini? Ni mpaka kieleweke?
 
sikutegemea mtu kama jussa kutushambulia (kwa umbea) kiasi hiki,wakati tupo kambi moja ya upinzani. Huu ni umbea kwani hakuna ukweli kwa yote aliyosema.all in all dr wilbroad slaa ndiye rais mtarajiwa 2010-2015 na hizi ndiyo changamoto za kuingilia ikulu. Still we'll vote for slaa! Go slaa go.......

..mwamba ngozi huvutia kwake. Run, dr slaa run!
 
Tatizo la Jussa na CUF yao ni kwamba wakati wao wanapigana na CHADEMA kuitafuta nafasi ya pili(kuwa chama kikuu cha Upinzani), CHADEMA wao washatoka huko na sasa wanapigana na CCM kuchukua utawala wa nchi.......poor CUFs
 
Tatizo la Jussa na CUF yao ni kwamba wakati wao wanapigana na CHADEMA kuitafuta nafasi ya pili(kuwa chama kikuu cha Upinzani), CHADEMA wao washatoka huko na sasa wanapigana na CCM kuchukua utawala wa nchi.......poor CUFs

Tatizo la CHADEMA wanapenda kujidanganya........ama kuwazuga wapenda mabadiliko ya kweli
 
Kwa wale ambao hupenda kukimbilia kutowa misimamo kutoka na sehemu ya kile kinachobandikwa hapa bila ya kuchunguza mazingira na upeo wa "ukweli" huo nawashauri waende katika facebook page ya Ismail Jussa na kufuatilia mtiririko wa mjadala huo na jinsi gani ulifikia mahala Jussa akatoa maoni yake hayo na kwa style hiyo. Hi mambo ya kukimbilia conclusions bila ya utafiti ama tafakari haina tofauti na ile mihadhara ya mitaani inayofikisha watu kushikana mashati.......

omarilyas
 
Back
Top Bottom