Alichosema Ismail Jussa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alichosema Ismail Jussa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Aug 16, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kuna mtakao kasirika na wengine kufurahia au hata kulalamika. Huu ujumbe wa huyu jamaa wa CUF nimeusoma mahali na nimeona ni heri tuusome wote.

   
 2. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Still I will vote for Dr Slaa
   
 3. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Huyu jamaa ni naona ameandika kiushabiki zaidi, kijuu juu naona amesukumwa na mapenzi yake aliyonayo kwa chama cha Chake (CUF), pamoja na dini yake. Inaelekea jamaa ni mbaguzi wa kutupwa. CHADEMA hawana uhusiano na LIKUD hata kidogo,Na nivema akatambua kwamba hata wao CUF wanahaki ya kutafuta vyama RAFIKI popote duniani, Mkiona HAMAS au HEZIBOLAH kinaendana na sera zenu ni vema mkaungana nao na sio kuendeleza siasa za kizushi hapa.

  Kama CUF imetapakaa na kukubalika Tanganyika kama alivyohisi ungetuambia mna wabunge wangapia Huku Tanganyika? Kama nyie sio wadini Mlimfanya nini Rwakatare?. naamini hata uchaguzi wa mwaka huu hamtapata kiti hata kimoja TANGANYIKA.


  Kuna demokrasia gani ndani ya CUF, Si juzi hapa Prof safari alikuwa analalama amechezewa mchezo mchafu? Si busara hata kidogo kusingizia chadema ni chama cha kifamilia hata CCM mara nyingi wana wahusiha wazee ktk kusuluhisha mamabo yao, Mtei wanahusishwa pammoja na wazee wengine kama wakina Makani mbona huwataji?

  Amejisahau kwamba CUF ni maarufu ZNZ kutokana na U unguja na Upemba? wenye macho tunasubiri siku atakapo Ngatuka Seif na ndo mwisho wa CAF, Muda ndo utatuambia kama hata haka kajamaa JUSSA katapata huo Ubunge, ni vema ukajifunza alipokufa kisiasa Mrema leo hii wako wapi wakina MBATIA; LAMWAI wa miaka ya 1995?

  Walichokifanya wabunge wa CHADEMA kwenye hili bunge lililopita nadhani historia ya taifa letu itawatambua na kuwaenzi,
   
 4. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mfa maji haachi kutapatapa kabla ya kukata roho!
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Du! bado kuleta lile la Mrema la kama Slaa alitimiza nadhiri tatu za upadri. Ukiyataka haya yako mengi tu wewe piga simu mtanzania
   
 6. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Well said Jussa, huo ndio ukweli mengine ni porojo na ushabiki bendera kufuata upepo.

  Btw. Rev umeinyofoa wapi hii nataka nika peruzi nami naona kuna vichwa na mijadala yenye afya huko.
   
 7. Wa Mjengoni

  Wa Mjengoni JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sikutegemea mtu kama Jussa kutushambulia (kwa umbea) kiasi hiki,wakati tupo kambi moja ya upinzani. Huu ni umbea kwani hakuna ukweli kwa yote aliyosema.All in all Dr Wilbroad Slaa ndiye rais mtarajiwa 2010-2015 na hizi ndiyo changamoto za kuingilia Ikulu. Still we'll vote for Slaa! Go Slaa go.......
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hizi ni moja katika sababu zinazonifanya nisite kuipigia kura Chadema na nashangaa kwanini hawaziaddress zaidi kung'ang'ania ufisadi ufisadi tu wakati kuna maswala mbali mbali yanahitaji ufumbuzipia
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Someni pia makala ya Ansbert Ngurumo ya wiki hii. Muafaka wa CCM na CUF si visiwani Zanzibar peke yake. CUF itatumika mainland katika jitihada za kuipaka tope Chadema. Yameshaanza. Rev. Kishoka, ubarikiwe.
   
 10. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Well, I pity Jussa. He is such a brilliant young guy but caught up in a political mess. I wish he could have analyzed the goodies of CUF and end there. But his trial to discredit Chadema has tainted his rather clever way of clearing CUF from diminishing trend.
  Jamani, Mcnhanyato wa Chadema wote twaujua Kuna Wachagga, Wabarabaig, wahaya, waha, wakurya, wajaluo, mpaka wanyalukolo. Wamo Waislam, wakiristo, wakibwetele, mpaka wakwere wa Bagamoyo.

  Migongano ya ndani ya chama mbona ndiyo afya ya chama chochote kinachofanya kazi! Wote mkifikiria kwa njia moja, kuna sababu gani ya kuwa na chama?

  No wonder alipokea ubunge wa kuteuliwa na JK dakika za lala salama. He is a good person but serving bad ideas.
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Lakini huyu Jussa ni swahiba mkubwa sana wa fisadi No 1 hapa nchini - RA. Anatuambia nini? Ni yeye ndiyo anacoordinate contributions to CUF from RA, pesa ambazo ni za wananchi alizoiba BoT. Na ndiyo maana kama mtakumbuka Mengi alipowataja mafisadi papa, Lipumba alitoa statement ya kumshambulia Mengi huku anajua wazi kwamba baadhi ya mafisadi papa hao waalipelekwa mahakamani. Kuyumba kwa Lipumba kuhusu ufisadi kulishangaza wengi na ni influence ya RA through Jussa.

  Na kilichomkimbiza Lwakjatare kutoka CUF mnakijua? Ni michango hii ya kifisadi wanaopokea CUF kisirisiri kutoka RA, michango ambayo viongozi wa chama hicho walikuwa hawataki kueleza chanzo. Hizi habari ni za uhakika kabisa -- kuna siku Lwakatare atakuja kumwaga yote hadharani -- tena kwa ushahidi.
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  no he has never been good boy! Amelewa kuteuliwa ubunge na ndugu yake jk.
   
 13. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Ila bajameni isije kuwa pia huu mjadala umeletwa hapa na hawa watu walioshindwa kazi yao (Uhasama wa Taifa) ili kuharibu hata kauwezekano ka CUF na Chadema kushirikiana hata katika ngazi za ubunge na udiwani, ikiwa imeshindikana kushirikiana katika ngazi ya urais. Nanusa kitu hapa. Tiumesikia kuna mipesa michafu imemwagwa kwa waandishi na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ili kumrarua Dr. Slaa. Mtawaona kuanzia tarehe 20 wiki ijayo.
   
 14. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Tatizo lenu kuambiwa ukweli hamtaki.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,

  Kwanza kama ingekuwa mimi ningemjibu mkulu kwa kuhitaji mifano na takwimu zinazodhihirisha aloyasema yote.
  Kwa mfano swali la kwanza:-
  1. Prof. Lipumba is more competent and more exposed in both local and international affairs and leadership than Slaa whose experience is merely of a whistleblower.

  Jibu:- Sio kweli kabisa, tumemwona Obama mwenye experience ndogo akiwa joined na kina J. Biden, Clinton na the whole bunch of experienced fellas ambao wamempa tafu. Anachoshindwa kuelewa huyu jamaa yetu ni kwamba kiongozi anayetakiwa ni yule mwenye Uzalendo, vision na Mbunifu wa kile anachokitaka ku accomplish at the end ili kuondokana na matatizo/mahitaji tulokuwa nayo - now, how to achieve all this, ndipo anachagua watu wa kuwa naye na sisi tunasemea Lipumba is one of them...
  Pili Lipumba ni mchumi sii mbunifu wala hana vision....huyu ni sawa na mpangaji wagharama za matumizi na mapato. Mara zote wachumi sii wabunifu ila wazuri kwa kukadiria matumizi na mapato pia njia bora za kuwezesha hivyo - Ni Lipumba anayemhitaji Dr. Slaa.

  2. CUF ni chama cha kitaifa wakati Chadema iko Tanganyika tu;

  Jibu:- Je CUF imeshinda majimbo mangapi bara?
  Kwani tunapozungumzia chama cha kitaifa, kinachohesabika ni uwakilishi wake sio kuhesabu wingi wa vibanda vyake mikoani.

  3. Kwa performance ya kisayansi na si ya kukusanya watu kwa helikopta, CUF ina nguvu zaidi Bara na Zanzibar, kigezo ni kila uchaguzi CUF imekuwa mara zote inashika nafasi ya chama cha pili na hivyo kukipa sifa ya kuwa chama mbadala - angalia matokeo hata ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ambapo pamoja na magazeti kuibeba sana Chadema, bado CUF imeshika nafasi ya pili (kumbuka huu uchaguzi ulikuwa Bara peke yake)

  Jibu:- Uchaguzi wa Kitaifa kulikuwa namajimbo 181 bara na Chadema ilipata ushindi wa viti 5 hali CUF hawakupata kitu. Zanzibar CUF walipata viti 22 kati ya viti 50. Kwa hiyo ushindi wa pili wa CUF unatokana na viti 22 vya visiwani na sio Bara. CUF haina nguvu bara sawa na Chadema isivyokuwa na nguvu visiwani.
  pili, Uchaguzi wa sewrikali ya mitaa Chadema hawakushiriki na kusema kweli yalikuwa makosa makubwa. Hawakufanya hivyo kutokana na kuvunjika kwa umoja mlokuwa mmeanzisha hivyo wakaweka mawazo yao sehemu nyingine.

  Swali la 4. jibu:- kuhusiana na CUF kujijenga zaidi ya Chadema. jamani lets not kid ourselves.. CUF imejijenga vipi?.. CUF na Chadema kitaasisi ni vyama ambavyo havina uwezo kabisa yaani wote wanabangaiza tu. Hili sii swala la kuhitaji mjadala kwani CUF na Chadema bado kabisa wamebanwa vibaya na CCM kiasi kwamba kujitangaza kwao kunategemea imani ya wanachama wake. Wote waliohama CUF wamepitia mitihani kama ya Chadema na vyama vingine vyote vidogo. Kumbuka kuhama kwa Lwakatale CUF ilitokea kipi.. fact is Hakuna aliye na afadhali.

  5. Chadema kimeshindwa kujivua gamba la ukabila na udini na sasa ndiyo kinazidi kutopea huko wakati CUF imetanda kila pembe ya Tanzania;

  Jibu:- Duh mkuu wangu, marafiki zangu wakubwa ni member waCUF damu, na kijiwe changu kikubwa ni pale K tea shop mjini Chagga st... ninawajua CUF kuliko unavyofikiria. Chadema kama ni Wadini au Wakabila, ni CUF pekee ndiyo ingeweza kuwaondoa ktk fikra hizo kama zipo kweli na mngewa join, lakini sio kuzungumzia nje hali CUF yenyewe inaonekana kusongwa na matatizo hayo hayo. Ushahidi wangu:- Why CUF imejikita kwa maswala ya Zanzibar zaidi ya bara?.

  6. CUF kina mtandao wa chama wenye muundo uliokamilika wa uongozi uliojipanga kitaasisi wakati Chadema hakina muundo na huishia kuokota wajumbe wa vikao mitaani kupata uhalali wa vikao.

  Jibu:- Chadema sii wajuzi wa kila kitu, vitu kama hivi ndivyo CUF could have bring in kama mchango wao. haiwezekani Chadema kuhitaji kuungana na chama ambacho hakina ubora wowote.

  7. CUF kimeonyesha umakini mkubwa katika uongozi na hata katika Kambi ya Upinzani Bungeni kimeonyesha ukomavu tofauti na Chadema ambao hata wale wabunge wake 11 tu wanashindwa kuelewana..

  Jibu:- Bungeni sio mahala pa kuonyesha unyenyekevu. Ni sehemu ya kuvuana nguo na sio kubebana kama CCM wanavyofanya ili mradi kulindana. Bungeni wajumbe wanakuja kuwakilisha wananchi na sio kuwakilisha chama. Kutoelewana ndio inaonyesha ukomavu wa watu kuona tofauti au matatizo ya bajeti inaposoimwa na sio kukubali kila unachoambiwa.

  8. CUF kina misingi ya kidemokrasia na ndiyo maana hata Prof. Safari aliachiwa kushindana kwa uwazi na Prof. Lipumba kwenye nafasi ya Uenyekiti wakati Chadema kina uongozi wa kiimla wa muasisi wa Chama mwenye uwezo wa kumuengua mgombea Uenyekiti ili mkwewe apite bila ya kupingwa:

  Jibu:- Kugombea kiti cha Uenmyekiti sio swala la demokrasia. hakuna kifungu chochote cha demokrasia kinacholazimisha au kushauri vyama kupitisha uchaguzi inapofikia swlaa la Mwenyekiti.. Na pengine huelewi kwamba Chadema mwenyekiti ni Mbowe na anayegombea Urais ni Dr.Slaa wakati CUF mwenyekiti ndiye mgombea kiti cha urais!

  Yaani Rev. mkuu wangu huyu jamaa majibu tyake ni rahisi sana naweza kuyajibu pasipo hata kufikiria..Ila sidhani kama yeye yupo tayari kupokea maswali kutoka upande huu!.
   
 16. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #16
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu jusu analeta propaganda walizopewa na ccm kupunguza nguvu za dk slaa na chadema kwa kuwa wapewa danganya toto ya serikali ya mseto ambayo itaifanya ccm iendelee kutawala milele zanzibar na lawama za kero za wananchi na ufisadi watazibeba pamoja, jusa anachowaza sasa ni ulaji tu ndani ya serikali ijayo ya mseto kwani anajua kuwa lazima atakuwa waziri sasa ndo amekuwa mkuu wa kitengo cha kina tambwe hiza kwa kuponda upinzani na nguvu itakayokifuta cuf kwenye list ya vyama vya upinzani! Hiyo jeuri jusa kaipata wapi ya kutotambua mchango wa chadema na wabunge wa chadema wakati mwenyekiti wake pr. Lipumba wiki iliyopita alikili bayana kuwa dr. Slaa amefanya mambo makumbwa na mazuri kwa taifa letu, sasa haka kajusa kanaungea utumbo gani? Kwa maada hiyo hiyo lipumba alisema dr. Slaa alichelewa kutangaza nia laiti kama angetangaza mapema kabla ya cuf hakijaweka mgombea kungekuwa na makubaliano.

  Huyu bwana jusa nadhani ana upungufu wa fadhili na kupuuzia support ya chadema kwa cuf kwenye chaguzi zilizopita ambapo chadema wamekuwa wakiunga mkono vyama vyenye wagombea wenye nguvu, ukianzia mwaka 1995, chadema hawakusimamisha mgombea bali waliwaunga mkono nccr-mageuzi bara na cuf zanzibar, 2000 chadema waliunga mkono cuf bara na zanzibar, na mwaka huu 2010 to show goodwill wanamuunga mkono cuf zanzibar kwa kuwa sharif hamad anakubalika, hivyo chadema ni chama kilichokomaa na kinamalengo ya mda mrefu sio kugombea uraisi tu hata kama haukubaliki,
  vile vile napenda kumfahamisha jussa kuwa chadema kimekuwa na viongozi tofauti toka pande zote za taifa letu kwa vipindi tofauti, kulikuwa na wenyeviti kama bob nyange makani, ni msukuma wa shinyanga, mtei, na sasa ni mbowe na mda wa mbowe ukisha atakuja mwenyekiti mwingine, haya kuna zito kabwe mha wa kigoma, kuna akina tumbo wasukuma, kuna slaa wa arusha, tunamwomba bwana jusa asipandikize propaganda zake kwa sababu ccm imekwisha imaliza cuf kwa kukubali kuunda serikali ya mseto hivyo cuf sio chama cha upinzani kama ilivyokuwa awali hivyo hatushangai kuona mtu kama jusa kuropoka mambo asiyoyajua, ili kukipaka chama makini matope. Bara sio zanzibar wanakoendesha siasa za uunguja na upemba kama jadi yao! Jusa asifikilie kuwa kuna chama kinachotaka kufaidika kisiasa kwa kuwagawa wananchi kwa makabila rangi na dini, hilo cuf na ccm wamefanikiwa zanzibar kwa sababu ya kijikundi cha watu kama jussa ndo wanafaidika kupata madaraka na wazanzibari wataendelea kusota kwani watu waliodhani kuwa watawakomboa wamekwisha nunuliwa na kutengenezewa ulaji kwenye serikali ya mseto hivyo hawaoni aibu kuunganisha nguvu na kuwakomboa wananchi! Ningependa sana bwana jusa akatueleza cuf ina historia ipi ya kushirikiana na kuwaunga mkono wapinzani wenzao kama chadema? Au nichame kilichojaa ubinafsi na chuki! Wanavyoona chadema inaungwa mkono na watanzania wanaumia sana mpaka huyu bwana anayejiita mpinzani ana amua kupika majungu!

  Bwana jusa wewe ulikuwa mbunge wa kupewa na karume kama mlivyokuwa mmeomba umetoa mcango gani wa kulisaidia taifa letu kama zitto kabwe tu! Bila hata ya kukuletea dr. Umefanya nini watanzania tusichokiona? Au chama chako cha cuf kimefanya nini kwa maslahi ya taifa? Nyinyi si ndio chanzo cha watu kibao kuuwawa ili wewe upate ubunge na hatimaye mpewe madaraka yasiyokuwa na memo kwenye serikali ya mseto zanzibar, uhuni mnaoufanya malipo ni hapa hapa duniani, wapemba waliwaamini kuwaletea mabadiliko lakini mmewasaliti na kuwajoin ccm kutafuna rasilimali za nchi hii. Tunaomba huo ujahidina wako na ubaguzi uishie huko huko zanzibar, dhambi ya ubaguzi itawatafuna! Mmemalizana wapemba na wa unguja sasa unataka kuteletea na sisi, nyinyi wabaguzi sana mmekwisha jitangazia kuwa zanzibari ni nchi! Lakini bado tunawabeba kwenye jamhuri wa muungano, hivi tukiwa na srrilikali tatu mtaweza kulipa gharama za serikali ya muungano?
  Bwana jusa ni na mengi ya kukutaarifu lakini ningepata namba yako ya simu ningeweza kujadili nawe kiungwana kwani umeonesha wazi kuwa wewe sio kiongozi makini wa chama cha siasa ila una lako jambo,, na huo msetu unaopigia chepuo utakutokea puani kwa kuuwa demokrasia na kupaka matope chame chenye sera, itikadi na mtandao wa kutosha, nchi nzima, jussa unaelekea wivu na chuki mlizojijenge znz zinakusumbua kwa maana hata helikopta ya chadema umezungumzia sasa hutaki chadema wawafikie wananchi wengi kwa haraka na kueneza hizo sera. Cuf imechemka sasa ndo tunawaona their true colour, serikali ya mseto imewapa kibuli wamesahau who was there to support them, ni wagumu wa kufikiri na wepesi wa kusahau,,,,,,,,,,,,,,,, mmejimaliza kwani seif atakuwa makamo wa pili wa raisi asiekuwa na kazi yaani pambo flani tu, na nyinyi mmelizika kwa kuwa mtapata nafasi ya kula kivuli jasho letu, nakwambia damu ya mtu hailiwi yakhe! Watu walimwaga damu kupata ukombozi lakini mmewasaliti, jussa wewe hufai kwenye siasa za huku bara nende zanzibar kwenye siasa zetu ya kiswahilina na ubaguzi ambayo chama chako ndicho kinafaidika nazo na mnasema mnanguvu zanzibar hilo ni bomb anytime litalipuka
   
 17. D

  DRV Member

  #17
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kuna haja sana ya kuwa makini na hii thread. Nimekuwa na moyo mzito kukubali kuwa huu ni mchango wa Jussa. Hatujapewa source na ni vigumu sana kuthibitisha kwamba kweli huu ni mchango wake. Kwa observation ya haraka haraka kumeonekana kuwa na dalili za kumkubali Dr.Slaa kama msimamo wa chama cha CUF (if the expression of the chairman truly represents the party's perspective). Hatahivyo nahisi CUF wamekosa umakini kwa kiasi kwa kuachia mianya ya kuendelea kujenga na kupanua mutual distrust between the two parties (as in the case of Mwera na usikute wamefanya kujibu mapigo ya Lwakatare pale bukoba bila kutambua tofauti kubwa ya kiamzingira iliyokuwepo).
   
 18. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Fedha za kampeni za Ikulu zimeanza kutumika vizuri. Kama kweli hii makala ni huyo Jussa hapa alikuwa anabomoa tu chama chetu kwa kashfa zilezile wanazojaribu kuzipaka siku zote kwa Chadema, Mtei ni mwasisi wa chama hilo halina ubishi. Chadema hakuna ukabila wala udini. Hizi ni siasa za kiCCM za kutaka kila mara kuwagawa watanzania kwa dhana ya ukabila, ukanda, na udini.

  Swala la kuungana ni muhimu sana kwa ajili ya kuongeza nguvu, hata hivyo sio lazima kwani ni ukweli usiopingika kila chama kina malengo yake, mtazamo na uongozi wenye nia na uwajibikaji tofauti.

  Tangia kuanzishwa kwa chadema kimekuwa na viongozi mbalimbali kutoka pande zote za Tanzania. Kumekuwa na wazee wa chama wenye busara, na wanaheshimika kwa busara zao sio uasisi wao. Chama katika kipindi cha Mbowe kimekuwa kwa kiasi kikubwa, Mbowe amefungua milango na kuwafanya maadui kuanza kutupa mawe kutoka kila kona.

  Chadema kimejengwa kama taasisi, na kweli kwamba kina kuwa tutapitia hatua mbali mbali, tunapokea wanachama na mawazo mapya kila siku. Tunamwomba mtoa mada azingatie zaidi uimara wa Chadema na aachane na majungu. Viongozi wa chadema wanaelewana vizuri tu kiongozi, wabunge wa chadema wamekuwa wakielewana vizuri bungeni na hapajakuwa na matatizo kama mtoa mada anavyotaka kuuleza uuma. Na kazi zao umma wa watanzania ni mashuhuda.

  Tukiwa kwenye kipindi cha kampeni tunajua mengi yatasemwa na mwembe wenye maemba utashambuliwa sana kwa mawe.

  MPIGIE KURA DR. W.P SLAA. wAPIGIE KURA WABUNGE WA CHADEMA, ICHANGIE CHADEMA. TUJENGE NCHI
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi sio mshabiki wa dr slaa wala lipumba wala JK ina ni shabiki wa mabadiliko.
  • Competent- labda watu walioelewa wanifafanulie ana maana gani. katumia vigezi gani.Lakini natambua Taasisi huru ya kupima perfomance za wabunge imempa Dr slaa rate ya juu kabisa.
  • Exposer kama nimeelewa ok let assume kweli lipumba anamzidi Dr slaa Je anamzidi JK pia. Lakini tusisahau hata serikali ya sasa tuna watu wana exposure zanazoaminika lakini hawajafanya wala kusikia wakitetea maslahi ya taifa.wengi wamekuwa watetesi wa maslahi ya kisiasa Dr slaa sio mmoja wao.Kinadharia kweli hata JK, Chenge na Lowasa wanamzidi lakini kivitendo Dr Slaa anamzidi Lipumba
  • Whistleblower- Nadhani kwa position yake ya bunge au upinzani hii ni moja ya mambo watanzania wanataka wasikie . Kafanya kazi kubwa.Je huu hauwezi kutumika kama udhaifu mtu kam lipumba kutokuwa na habari mapema na za kashfa kama EPA wakati yeye ni ndani ya eneo lake la taaluma. Vile vile Kwangu ni udhaifu sio kwa CUF bali wabunge wake hakuna aliye Whistleblow kitu chochote kile cha kitaifa
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Kwa maneno haya wakati tunataka kuiondoa CCM madarakani ni lazima tujue kuwa sisi watanzania ni....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...