Umeshapinduliwa hapo.Huyu mdogo wako alikuwa 'karibu' sana na mme wako ndiyo maan akampakia maneno mengi kirahisi hivyo
Mzee Tupatupa
Tatizo halitaisha na litaimarika. Believe me or not.Unajua kuwa watanzania huamini kuwa hasira nyingi hutokana na ukweli wa habari iliyokuhusu? Ingawa si kweli,hiyo ndiyo imani tuliyonayo.Ndiyo itumikayo na kuendelea kutumika na mme wakosiwez kuongea na huyo mdogo wang kabisa kabisa
Ni wa kike wapendwa
pole kwa ulio pitia!
Ila ukitaka kumsaidia ndugu usimkaribishe kwako!
Naongea out of experience!
Ungemuuliza anataka kufanya nn na umpe kamtaji kidogo aanzi hapo!
zaid ya yote ni Dume!!!
mwambie hutaki arudi kwako ila mumeo sasa atahisi ulio kuwa wafanya ni kweli!!!!
Msaidie huko huko aliko!
Ndugu kazi saaanaaa!
Tatizo nini si kasema kweli. Acha kupokea vizawadi unajirahisisha. Jirekebishe tatizo si wewe?
huyo msichana kurudi kwangu haipo nae anafahamu lakin nachofikiria ni jinsi ya yeye kujua how i feel kwa kitendo alichofanya
dawa ya huyo mdogo wako ni kumrusha roho hadi imtokee dirishani. mpigie simu kila mara umpe progress yenu. Muambie shem wako anakusalimia jana tumecheka sana tulikuwa tunaangalia movie tukakukumbuka. then muambie mie na shem wako tunaenda shamba this wknd, na kesho atakuja kunisaidia kwenye biashara nna shida moja. :A S 103: usimuulize lolote kuhusu maneno ya udaku aliyokusemea. ila akitaka kuja kwako urudi hapo tukufundishe jinsi ya kumtoa nishai. nimesahau, jumapili mkitoka church na shemeji mpigie ndugu yako msalimie, afu muambie shemeji yako huyu hapa msalimie, mshikishe simu shaaaaa.
kwa upande wa mumeo, muweke wazi. prove ur innocence kwa kuwa open zaidi na kumshirikisha kwenye maamuzi ya biashara. biblia inasema yeye ajidhaniaye kuwa amesimama, na aangalie asije anguka. jifunze kutovuka mipaka na wateja.
Hapo nakataa kabisa hajakuwa karibu nae kiivyo nina uhakika asilimia 100
Hii meseji aliyonitumia sasa hivi sijamuuliza chochote
( Dada naomba nisamehe najua nimekuhudhi kwa namna moja ama nyingine xo sina budi kukuomba radhi kwan mm x mkamilifu nisamehe yote yaliyo tokea na tusiwekeane kinyongo kwan haya ni maisha tu
Well said,Ukitaka ndoa idumu ishi wewe na mumeo,watu wengine wakihusika lazima kutakuwa na chokochoko!
Nitaanza na kukupa lawama si tabia nzuri kuzoeana na wanaume wengine angali we ni mke wa mtu kwamaana hio wewe hapo umekosea,inawezekana aloyasema mdogo wako si yote yana ukweli ndani yake,lkn jishushe kwa mumeo na ukiri makosa yako na huyo mdogo wako mnafiki alitakiwa akupe taarifa hizo wewe na si azunguke nyuma ya mgongo wako kwa maana hio hapo kuna njama inachezwa!
Sikushauri uendelee kuishi na huyo mdogo wako maana keshaleta hitilafu,wanaadamu ni viumbe dhaifu sana hatuaminiki,na usifikirie kwasababu ni nduguyo atapenda maendeleo yako!Watu wengine hawafurahii kuona wengine wameendelea na wao wapo chini!THEY WILL WANT TO TAKE YOU DOWN WITH THEM OR TAKE OVER YOUR SPOT!!
Naamin hamjambo na mnaendelea vzr na kutusaidia ushaur sisi wenye matatz ya hapa na pale.
ni miezi minne imepita toka nimchukuwe mdogo wangu (mtoto wa baba mdogo) kijijini baada ya yeye kufeli form four na kuzalisha mtoto nikaona nimchukue nije nae mjini kwenye biashara yetu angalau apate pesa za maziwa ya mtoto
basi tumeishi vizuri siku zote na juz ndiyo akaniaga anataka arudi nyumbani akamuone mwanae,nikamwambia hakuna tatizo jiandae nkamwandalia pesa za safari vzr bas akaondoka jana.
baada ya kuondoka mume wangu akaniweka kwa mazungumzo nanukuu( mdogo wako kanieleza mambo ya kusikitisha umekuwa na mazoea mabaya na wanaume pale kwenye biashara wengne wanakuja kila siku,wengne wanaenda china wanakuletea zawadi unanidhalilidha,umekuwa malaya kwa kuzoeana na wanaume lukuki pale kazini na maneno meng sana)
Ukweli n kuwa hayo aliyoeleza mengne ni kweli nimezoeana na hao watu ni wateja wetu wazuri lakn hakuna cha zaidi hata huyu mdogo wangu anaelewa ukweli kwani muda wote nipo nae kazini.
nimemweleza mama yangu hajaamini kashangaa sana yani.
nafikiria najiuliza au huyu mdogo wangu alitumwa na mama yake kuja kuniharibia ndoa au ni kipi nilichomkosea au kosa langu kumsaidia had sasa amekuwa nae mtu anaonekana?au. ni kipi bado sielewi
mpaka sasa mume wangu ana kinyongo,
Huyo mdogo wangu cjamuuliza kitu chochote
nafikiria nimwambie neno gani ajue jinsi amenikosea au ninyamaze?
nishaurini wapendwa nifanye nini?