Alichonifanya huyu dada, sintokaa nisahau

Alichonifanya huyu dada, sintokaa nisahau

Makaura

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
892
Reaction score
295
Wadada badilikeni jamani, uongo wenu utawamaliza. Kuna mdada tumefahamiana siku 1 baada ya hapo tukawa tunawasiliana, hi leo tukakubaliana kuonana maeneo ya Feri-Kigamboni(alipenda hapo mana anakaa Kibada-kigamboni pia lengo kuu ilikua just kufahamiana). Nikamuambia aamue muda gani ni convinience kwake itakayo faa kuonana, hatimaye ka sugest kua ni saa 12:30 jioni. Ilipofka saa kumi jioni nikanza safari nikitokea Mbezi, nkafka posta, nkapanda Bodaboda mpaka Fery, nikavuka(muda wote nampa update ya safari). Nlipoanza kuvuka aka niupdate kua naye ndio anatoka home, bada ya kuvuka nkanza kumsubiria mpaka saa moja kamili, ikabdi nimpgia akasema amefka geti jeusi(kituoa jirani na feri), ikafka saa mbili dakika 5, nkapgia tena akasema amefka na yupo karbu na standi ya daladala. Nkamwambia nami nipo hapo, akakata simu, bada ya dak 5, akanitext "please wait kidogo" saa mbili na 30 nkapga simu akaniambia hvi "SAMAHANI NISAMEHE NIMESHNDWA KUJA". In short imeniuma sana na wadada kweli mmenikatsha tamaa na nimewachukia sana, nimeteseka sana na daladala muda huu ndio nafka geto! kibaya zaidi ni mara ya pili hili likinitokea! Wadada! wadada! wadada!
 
Jiangalie kwanza kwanini wanakufanyia hivyo,sera zako pengine tatizo.
 
Pole sn yaani kweli kila mtu ana mnyonge wake mi ukiacha mke wangu nina michepuko ambyo mi naipanga lkn ww mmmmm
 
Mmmh una deal na watu wa namna gani???

mbona hopeless
facebook???maana umasema hamjuani

nunua mkate kwa mangi upike chai unywe ulale.pole
 
Wadada badilikeni jamani, uongo wenu utawamaliza.

Wewe ndo unatakiwa ubadilike. Ukishabadilika hutadanganywa tena. Kosa lako unalijua?

Nikamuambia aamue muda gani ni convinience kwake itakayo faa kuonana.

Hilo ndo kosa lako.
 
Laiti ungejua ulvo nitia hasira. Kwani wewe ulianzeje kufahamiana na mumeo/boyfriend wako? Ama kweli wote akili sawa. masai dada
Mmmh una deal na watu wa namna gani???

mbona hopeless
facebook???maana umasema hamjuani

nunua mkate kwa mangi upike chai unywe ulale.pole
 
Last edited by a moderator:
Shukrani kwa majibu yenye hekma, matajiri wengi wamefanikiwa kwa "networking", pia mke/mume hupatkani kwa njia hii Khantwe
Mkuu hata mabinti ni mambo ya msingi....tupo duniani tunahitaji marafiki,tunahitaji network na tunahitaji kuanzisha familia pia. Af wewe unaliona hili dogo???? Au na wewe ndo tabia yako?
 
Last edited by a moderator:
Unaweka miadi kwenye feli kweli jamaa yangu....? Enewei usiumize kichwa hizo ni changamoto katika mapenzi...

Mi nilijua wangekutana Karambezi........au basi hata sehemu yenye ice cream.......ferry......?.......aisee......dada kakuona umekaa kimjomba sana ndugu yangu Makaura........
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom