Imeshakula kwake mwache ajutie maamuzi yake
Haya maelezo ya Tabby kumhusu Zitto yamenikuna sana. Nimeona niyakopi tena hapa. Kkwa wale ambao mlikuwa hamjui, tatizo la Zitto ndio hili hakuna kingine! Anapenda KUABUDIWA, KUPIGIWA MAGOTI. Bila shaka ndio maana ACT wakijua hilo wakampa uspreme leader ili asiwe chini ya mtu mwigine. Tabby kamcharacterise Zitto ifuatavyo:
Zitto yuko talented lakini hayuko organized, hajielewi na ametawaliwa zaidi na ubinafsi, kiburi na show!. Zitto unaweza kumhamisha kwenye mission yake kwa kumsifia na kumpamba. Ameonyesha kukosa sifa za uongozi kwa sababu haonyeshi nia ya dhati ya kufikia malengo wala uchungu wa kutokufikiwa malengo.
Hayuko tayari ku sacrifice personal interests kwa maslahi ya public ambayo baadaye ingemlipa satisfactions mara mia na historia ya nchi siku zote ingemtaja kuliko kiburi, maringo na kujaribu kuharibu maslahi ya umma bila chembe ya hisia. Anaamua kusaliti mission kwa sababu tu amekosa kuabudiwa kwa kiwango anachotaka ama amepata recognition kubwa hata kama ni flattering upande pinzania, na hivyo kuwa tayari kuwageuka na kuwaua Watanzania wote ili mradi atumikie kundi haram linalomsifia hata kama ni kwa njia haram.
Baada ya matusi kwa ukawa, anataka kujiunga nao ama kwa kuwa anahitaji kuendelea kuwa ndani ya adui ili aweze kummaliza vizuri, ama anajisikia kusalitiwa na waliokuwa wanamwabudu kwa kuwa hawezi kufanya madhara zaidi kwa CHADEMA na sasa UKAWA na hivyo anaamua kuwageuka, au anarudi baada ya kuona anakuwa mpweke kwa kutengwa na hivyo anatafuta peers, au inaweza kuwa sababu yoyote.
Lakini katika mazingira ya vita vya ukombozi, watu kama Zitto hakuna mtu generali mwenye akili timamu anaweza kuwaamini kwa lolote kwa sababu hawaaminiki. Zitto amejidhirisha ni namna gani hawezi kuthamini wala kujali commitments. Ni mtu irresponsible na hawezi kuwaza mara mbili kabla hajaamua kusaliti haki kwa sababu kwake KUSIFIWA NA KUABUDIWA ndivyo vya kwanza, mengine hayana thamani.
NINAOMBA UKAWA, KAMA KUNA SABABU YA KUMJIBU, NINASHAURI MU ACKNOWLEDGE RECEIPT YA MAOMBI YAKE, LAKINI MWAMBIENI MTAJIBU MWAKANI KWA SASA MNA TIGHT SCHEDULES KIASI CHA KUKOSA UWEZEKANO WA KUINGIZA mchakato wa USAJILI WA WANACHAMA WAPYA WA UKAWA