Mwaka jana mwishoni Zitto alifanya mahojiano na gazeti la mwananchi na alihojiwa mambo mbali mbali likiwemo la mstakabari wake kisiasa. Mwandishi pamoja na mambo mengine alitaka kujua Zitto kwa nini asihame toka Chadema na kuhamia vyama vingine. Zitto alisema kuhama chama siyo jambo rahisi, akasema ukihama chama utapata headlines za magazeti kwa wiki mbili mpaka mwezi mmoja alafu unakufa kisiasa.
Kiukweli alichotabiri Zitto ndicho kilichomtokea, baada ya kufanya ziara ambayo haikuwa na mafanikio makubwa pamoja na kuhudhuriwa na watu wengi. Zitto alipata headlines kweli kwenye magazeti na mitandao ya kijamii, lakini baada ya mikutano hiyo Zitto hasikiki tena. Mikutano yake mikubwa sijui kama ilikuwa na faida maana alishindwa kumchukua hata mwenyekiti wa mtaa awe wa Chadema hata CCM.
Nashawishika kukubaliana naye kwamba alichokuwa anaogopa 'kupata headlines za wiki mbili na kufa kisiasa' alikuwa sahihi kabisa. Kujenga chama si mchezo, hata angepewa miaka mitano kujenga chama chake Kigoma tu bado ni kazi ngumu sana. Zitto ni kijana ninayemwamini kwamba ana akili na uwezo mkubwa, ilikuwaje akaingia mkenge wa wapiga dili kwamba wanaazisha chama ambacho 'eti' wabunge wengi watajiunga nacho baada ya bunge kuvunjwa? Si amuulize Mpendazoe alivyoingizwa mkenge na CCJ 2010?